USHAURI: Naweza kufunga Engine ya 1G kwenye Nissan Fuga??

USHAURI: Naweza kufunga Engine ya 1G kwenye Nissan Fuga??

@Boeing 747 dogo langu huku nae Kuna mtu anataka kumuachia kwa hela ya kawaida ila imepaki na tatizo ndio Kama Hilo lilivyoanza., Akiichukua ntampa maelekezo umpe uelekeo wa wapi jijini Dar atapata Service hio mkuu
Ok mimi naishi Arusha...mwaka 2017 nilisafiri na hili gari kuelekea Dar. .tatizo lilinianzia njiani nilipofika Dar kuna dereva tax mmoja alinitafutia fundi..
Huyo fundi ni chalii mdogo sqna kiumbo ila umri wa kutosha nilitaka kumdharau lakini alinitatulia shida yangu mpaka sasa gari halina shida.
Huyu fundi jirani na lile jengo la mawasiliano...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba utuambie uzuri na ubaya wa hizi gari ,nimetokea kuzipenda sana ule muundo wake wa bodi
Boss kwa uzoefu wangu wa kumiliki gari lampuni ya nissan takribani miaka mitano sasa, naweza nikasema hivi..
1.Uzuri wa nissan spea zake kwa asilimia kubwa ni original hivyo ukifunga ni mkataba wa miaka kadhaa lakini lazima uwe na mbavu nene coz spea za nissan ni expensive kiasi.
2.Zina stability nzuri barabarani

3.Unaweza kupata nissan nzuri yaani latest yenye updated features kwa bei rahisi kuliko toyota.

4.Driving expeeience ya nissan is amazing compared to toyota
5.Nissan ni moja ya magari magumu sana na yenye roho ngumu ukiweza kutii masharti yake.

Ubaya niliouona kwa nissan.
1. Mafundi....mafundi wengi wa tanzania hawajiamini kufungua injini ya nissan...wameshazoea toyota...hivyo mafundi wengi watakuambia nissan hazifai...mara nissan siyo gari.
2. Spare...nissan kwa upande wa spea haitaki janjajanja...you must replace what has broken with the genuine one...haswa spea za sehemu nyeti kama vile engine na gear box...ukifunga spea feki tu utajuta.

3.Nissan nyingi zinakuja na CVT gear box...hapa ukiweka zile hydrolic za automatic gear box za kawaida wala gari haliondoki hapo lilipo.

4.Nissan hazina mfumo wa VVTi hivyo consumption huwa juu kidogo compared to toyota ila performance yake kwa road iko vizuri....kwa sasa nissan wanakuja na technology yao inayojulikana kama VVEL ambayo ni sawa na VVTi kwenye toyota.

Mwisho...hakuna gari baya au bovu...mafundi wetu ndiyo wabaya wamelowea kwenye toyota...gari lolote ukilitunza na kulipa huduma stahiki mfano spea, engine oil za kueleweka na transmission fluid ambazo ni recommended na manufacturer, gari lako utalipenda na kulifurahia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwisho...hakuna gari baya au bovu...mafundi wetu ndiyo wabaya wamelowea kwenye toyota...gari lolote ukilitunza na kulipa huduma stahiki mfano spea, engine oil za kueleweka na transmission fluid ambazo ni recommended na manufacturer, gari lako utalipenda na kulifurahia.
Ahsante nashukuru Mkuu ,ngoja nijichange nivute hii Fuga ,itakua ya mtoko Mara moja moja
 
Back
Top Bottom