Ushauri: Ndugu wameharibu ndoa ya dada yangu

Ndoa ni ya watu wawili ukiweka mtu wa tatu lazima ivunjike...

Mwambie dada yako Aache utoto...
ila mnapenda kukimbilia manyumbani kwenu na kusiko julikana nyie viumbee, njia sahihi sahihi ya changamoto za kimahusiano ni better kila kunapoibuka mgogoro, subini hasira zenu zipoe mnakaa chini na mwenzio baada ya nyote kupoza hasira zenu, kisha mnasolve mambo yenu.

Ila nyie wenzetu sasa, mnautoto wa kila mgogoro kutukimbia kama vile sisi ni mashetani na makatiri wa kutisha sana ........
 
Matumiz na Ela ndogo ndogo namsaidia, na mpk MDA huu tunaongea mke wangu Yuko kwake anamsaidia kumhudumia
 
amejifungua au bado πŸ’

kama tayari ni mtoto wa kike au wa kiume....

ndugu mtoa hoja,
nina maswali madogo mengine ya nyongeza, yenye sehemu A, B na C kama ifuatavyo.....

A. ulipompokea alipokimbia nyumba yake mwenyewe na kuja kuishi nawe kidogo, ulimuona kweli sister alikua mjamzito?

B. Je, sister alikudokezea kinagaubaga kisa na mkasa wa kuikimbia nyumba yake na kukimbilia kwako πŸ’

C. Je, mkeo alilipokeaje jambo hili na alikushauri nini πŸ’
 
Kama ungekuwa ni wewe ungekubali kumpokea?

Hapo hana ndoa tena. Baadhi ya wanawake visirani halafu wanachukulia maisha kirahisi rahisi wakati umri bado wadogo hawajajua Dunia Iko na mambo mengi.

Miezi 11 mtu hayupo kwa mumewe Leo hii analazimisha kurudi na kashibishwa ,ni mwanaume gani anaweza kushawishiwa kirahisi hivyo?

Mhudumieni akijifungua mpeni mtaji achome hata maandazi ajihudumie aishi mwenyewe.
 

A: wakati nampokea hakua na mimba na wala hajawai kunambia chochote khs kua na mimba mpk anarud kwa mumewe

B: Alinieleza kisa Nini, nikaona kisa chenyewe ni kama hakina kichwa Wala miguu, Ni mdomo tu wa dada yangu ndo umepemponza, ila nikamsihi tu arudi kwa Mumewe wakayamalize.

Dada Akadai hawez Kurudi mumewe atamdhuru, Nikampigia shemej yangu, Akasema Ni Mambo madg sn ayo, atayamaliza mwnyw TU Na mkewe, nisiwe na presha. Basi sikuendelea kuhoji sn, Nikamuuliza vp nimlete sahv myamalize kabisa au vp?.

Akasema hata akipumzika kwako Haina shida, ila kesho arud TU nyumbn, Hana tatzo nae Zaid ya mdomo mdomo wake ndo umepelekea kampiga vile. Nikasema POA, atalala kwangu ila kukicha ntamleta. Akasema POA, tumeagana Safi TU.

C: MKE wangu anaumizaa na yanayoendelea kwa wifi Yake, anatamanisha sn nifanye Jambo arudiane na mumewe,maana anaamini ni Mimi pekee kwny familia nnae elewana na yule mmewe
 
Yaan familia ikishakua na wadada wengi, Ni full kulishana ujinga TU afu wakishaharibu uko ndo wanatukumbuka mabrother wao[emoji35]
 
Ndoa ni ya watu wawili ukiweka mtu wa tatu lazima ivunjike...

Mwambie dada yako Aache utoto...
Kwanza,aache kunyonya ndio ataacha utoto, kuna kipindi unatakiwa uzibe masikio, wakati wako wa kusuisha ulishapita, fanya yako
 
Mkuu
Jiweke pembeni kabisa hapo.
Kubaliana na matokeo YEYOTE kwa sababu hata Biblia imeandika MWANAMKE MPUMBAVU HUIVUNJA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE.

Wewe waambie nduguzo watumie hekima kulitatua maana walishasema wanahitaji kuombwa radhi, wamuite shemeji awaombe radhi kisha amchukue mkewe.

Usijiingize katikati ya UPUMBAVU wa mtu wa kujitakia
 
Mwambie shemeji kitanda hakizai haramu [emoji16][emoji16]kuna mdogo wangu alitoroka kwa mumewe, akaenda huko kapata mwanaume mwingine kazaa mtoto, amefikisha mwaka mmoja wameshindana amerudi kwa mumewe wa kwanza amempokea...kuna wanaume wana roho nzuri [emoji1787][emoji1787]
 
Ningekua mi ndo bwashe wako wote ningewatia makofi wewena sister ako.

Muache upuuzi.
 
Doh yani hapo sasa kama hela ipo na wapo tayari kufanya DNA waende tu sababu ukijaribu kuangalia kuna utata hapo mwanaume namuelewa na mwanamke namuelewa ila kuna jambo lazima lifanyike kuweka hali ya kuaminiana tena.
 
Kilichokuondoa ni manyanyaso ya mumewe na kinachomrudisha kwa mumewe ni mimba ya jamaa mwingine.

Mwambie atulize akili avune alichokipanda, na asilaumu mtu yeyote cha msingi asiangalie tena nyuma ili apunguze majuto.
 
nashukuru kwa majibu mazuri ila nina ushauri moja mdogo tu kama itaonekana inafaa πŸ’

Pasina shaka yotote hupendezwi na hali hiyo ya mgogoro wa dada na shemeji yako kuidhoofisha nyumba yao wenyewe πŸ’

jishushe pale chini kabisaa mpaka wakuone chizi unaehangaika na mambo ya watu, but focus yako ibaki pale pale kutafuta suluhu ya kudumu na kuwaleta pamoja hao ndugu wanafamilia....

Fanya mkutane physically.

Mawasiliano ya simu yawe tu katika kukumbushana mahali na muda wa kukutana ....

wew pamoja na ndugu yako wa karibu hata kama sio mzazi wako, nae shemeji yako pamoja na ndugu yake wa karibu, singependa pawepo na kiongozi wa kidini au jirani awepo kwa hatua hii ya mwanzo sana....

zungumzeni, wapeni nafasi pia hao wanaofarakana kila moja nae aseme kinagaubaga kwa upole lakini pia kwa upendo.
Make sure Focus ya mazungumzo yenu iwe ni solving the dispute in peace....
Kila anae zungumza hitimisho lake liwe ni Amani,
Hapana makelele na mabishano πŸ’

Binafsi yangu na Imani yangu,
kwa Neema na Baraka za Mungu,

Mwenyezi Mungu ataonyesha njia na hatiamae suluhu ya changamoto hiyo itapatikana asilani πŸ’
 
kipaumbele cha kwanza mama na mtoto wajifungue salama mambo ya kumtia stess mama mjamzito hayo msije mkaleta shida nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…