Ushauri: Ndugu wameharibu ndoa ya dada yangu

Ushauri: Ndugu wameharibu ndoa ya dada yangu

Sioni kama ndugu wameharibu bali dada mwenyewe. Kama hakutaka kurudi ndugu wafanye nini?
Binafsi siwezi kumlazimisha dada yangu arudi sehemu ambayo hataki.... Si unasikia mauaji daily? Huwezi jua alichopitia huko ndoani....
 
Sioni kama ndugu wameharibu bali dada mwenyewe. Kama hakutaka kurudi ndugu wafanye nini?
Binafsi siwezi kumlazimisha dada yangu arudi sehemu ambayo hataki.... Si unasikia mauaji daily? Huwezi jua alichopitia huko ndoani....
Sasa Kama ananyanyasika, mbn yalipomshinda sahv analia tumsaidie asamehewe na mmewe?
 
Uwa nakuona una hekima na busara sana hapa umepotoka pakubwa sana. Umekosea umemtukana na kumdhalilisha mtu bila aibu.
Hekima ni pamoja na kuambiana ukweli huyu bwana alikosea kumpokea na kukaa na huyo dada ake tatizo lilianzia hapo
 
Sioni kama ndugu wameharibu bali dada mwenyewe. Kama hakutaka kurudi ndugu wafanye nini?
Binafsi siwezi kumlazimisha dada yangu arudi sehemu ambayo hataki.... Si unasikia mauaji daily? Huwezi jua alichopitia huko ndoani....
Naona alimpiga ndio maana.
 
Mbona hapo cjaona kuw kama ndugu wameshirik kuvunja ndoa

Dada yako ametoka kwa mme wake amekuja kwako ( ukamfukuza ili arudi kwa mumew baada ya kuongea nae na mwanaume alikuw hana shida yupo tayar wayamalze wenyew

Dada ako akagoma akaenda kwa. Ndugu wengine kukaa huko huoni tuu mtu wa kwanz kuvunja ndoa ni huyo mwanamke (yeye BINAFS)


Kwan ni wew maan umetumia uwezo mdogo wa kuchanganua na kutupa rawama kwa ndugu ambao wao ni daraja la 3/4
 
BASI KWENYE MATUKIO KAMA HAYA NDUGU MARAFIKI WANAKUWA BEGA KWA BEGA NA WEWE,
UJIONDOSHE KWAKO KISHA UKAANZE KUTANGA TANGA KUKAA HUKO NA KULE.

YAKITOKEA YA KUTOKEA, WALE WALE WASHAURI WA KUTENGANA KWENU. WANAKUA KIMYA, HAWANA MSAADA WOWOTE HATA WA KIMAWAZO.
UNAKUA UMEHARIBU HUKU KWAO NA KULE KWAKO.
UNAGEUKA KUA MJADALA MIDOMONI KWAO!
 
Wakuu,

Mwezi Mei mwaka jana, kuna dada yangu mmoja aligombana na mumewe na kukimbilia kwangu. Nilipoongea na mumewe, akasema yeye hana tatizo nae, arudi tu wayamalize.

Nilipomsihi dada arudi wakayamalize, akawa hataki, anang'ang'ania aendelee kuishi kwangu tu. Nikaamua kumfukuza aondoke, kwangu sina nafasi ya kuhifadhi mke wa mtu mimi.

Kumbe alivotoka kwangu akahamia kwa ndugu wengine wakampokea akaishi. Nikawa naskia tu, sasa dada anakaa kwa ndugu flani, mara kahamia kwa ndugu mwingine, kwa mumewe kagoma kabisa kurudi.

Nimewasihi ndugu zangu sio vizuri kukaa na mke wa mtu majumbani kwenu, hawataki kunielewa, wanadai namtetea sana mume wa dada yangu, nataka mpk afe ndo nijue mumewe ni mnyanyasaji wa kijinsia.

Wakasema kama mumewe anamtaka mkewe basi amfate mwnyw ukweni na akaiombe radhi familia, vinginevyo asahau kabisa kama alishawai kumuoa ndugu yao. Nikaamua kujiweka kando na hayo mambo.

Amekuja kurudi kwa mumewe mwezi huu tar 02 (miezi 11 imepita) akiwa na mimba ya kubwa sana. Mumewe kagoma kabisa kumpokea akidai mkewe aliondoka akiwa hana mimba, inakuaje arud kwake akiwa na mimba? Hiyo mimba sio yake.

Nmemhoji dada yangu, anadai ile mimba ni ya mumewe 100% na aliondoka nayo, ila alishindwa kumtaarifu mumewe kutokana na ugomvi uliokuepo kati yao.

Ndugu waliomhifadhi miezi yote hiyo wananipigia kunisihi niongee na shemeji yangu, ampokee mkewe maana ni mjamzito sana anaweza kujifungua muda wowote. Nimewaambia hiyo kazi siifanyi, fanyeni nyie wenyewe mlioyasababisha. Wanadai jamaa hawezi kuwaelewa, walishagombana tayari na hawapokelei kabisa simu zao.

Nmemtafuta shemeji, anachosema ni kwamba, kama kweli mkewe aliondoka na mimba yake ile mwezi Mei mwaka jana walipogombana, basi mwaka huu mwezi January au February alitakiwa awe tayari keshajifungua mtoto.

Sasa hivi ni mwezi March, ni miezi 11 tangu mkewe aondoke bado ni mjamzito hajajifungua, hivyo kwa vyovyote vile ile mimba sio yake. Kaipatia huko huko kwa ndugu zake na kwa tafsiri hiyo, hamna ndoa tena hapa.

Kiukweli mpaka sasa kichwa kimepata moto, sielewi nifanye nini dada yangu akae sawa maana analia muda wote (na hii mimba alionayo nahisi itamletea shida au huenda akajidhuru).

Pia nishauri nini kifayike ikiwezekana arudiane na mumewe, maana jamaa hataki hata kumskia mkewe wala habari zake na kahama kabisa pale nyumbani, kaenda kupanga sehemu nyumba nyingine kabisa.

Nawasilisha. [emoji120]
Kwanza hongera kwa kusimama kama mwanaume, pili hongera kwa kupata bwashe anaye jitambua, waulize hao ndugu leo wanataka dada arudi kwa mnyanyasaji? Wekaa pembeni kama mwanzo
Wamalizie ngoma waliyo anza kuicheza
 
Ndoa ni ya watu wawili ukiweka mtu wa tatu lazima ivunjike...

Mwambie dada yako Aache utoto...
Kipindi hauna mimba unabembelezwa unaringa, upo kwa ndugu zako. Unasema jamaa ni mnyanyasaji.
Imepita miezi kadhaa unakuja na mimba kubwa unataka kujifungua😀😀😀😀😀
Hayupo mwanaume mwenye akili timamu na rijali atakupokea Hata ningekuwa mimi, ndugu zako watalea hiyo mimba na mpango na wewe sina hata ungelia machozi ya damu.
 
Wanaume tunapitia mengi sana, imagine huyo dada kapewa mimba na mtu mwingine lkn anataka kumpatia mumewe mzigo wa malezi.
Wanawake wana akili za kitoto sana na huchukulia mambo mepesi hapo ataweza hata kujidhuru ili uamini ni mimba ya jamaa. Amebembelezwa arudi lkn kang'ang'ania kwa ndugu zake, amepata mimba ndiyo anakumbuka arudi kwa mumewe mnyanyasaji 😀😀😀😀
Usiishi na mwanamke kwa kumuonea huruma akishindwa kufuata masharti yako timua.
 
Kipindi hauna mimba unabembelezwa unaringa, upo kwa ndugu zako. Unasema jamaa ni mnyanyasaji.
Imepita miezi kadhaa unakuja na mimba kubwa unataka kujifungua😀😀😀😀😀
Hayupo mwanaume mwenye akili timamu na rijali atakupokea Hata ningekuwa mimi, ndugu zako watalea hiyo mimba na mpango na wewe sina hata ungelia machozi ya damu.
Kumbafu sana, wanaume huwa tunabebeshwa misalaba sana.
Ajifungue wakapime DNA
 
Back
Top Bottom