Tychob
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 3,972
- 5,170
Akiuawawa je na vipigo?
Anko wangu siku aligombana na mkewe na ulikuwa usiku wa saa sita wanapokaa ni karibu na wazazi wote wa mke na mume.
Walivyogombana mwanamke usiku usiku akaenda kwao akawakuta wazazi wake wamelala akawagongea kuulizwa haya vipi saizi akasema mmewe kampiga kwaiyo kaona bora akimbie asije akafa
Mama mtu akataka kumkaribisha ndani ila mzee akagoma akasema hizo taarifa ni za upande mmoja kwaiyo hawezi kumpokea kwani yeye ni mke wa mtu hata kama ni mwanae, mzee akamtimua japo ni usiku sana.
Anko alivoona mke kaondoka na hajui alipokwenda alienda kutoa taarifa kwa kwa wakwe kwamba mkewe kakimbia hajui alipokwenda na usiku ule basi mzee akamwambia alifika muda huu tukamrudisha huko basi alienda home ila hakumkukuta akaingia ndani akambonji hata dk kadhaa hazikukata anasikia mtu anagonga kufungua ni mkewe mahojiano yakaanza ila baadae walielewana na maisha yakaendelea hadi leo wapo pamoja.
Funzo: hapo hukutakiwa kumpokea kabisa hata kwa sekunde ila ungemwambia aje na mwenzie wajieleze wote ungenusuru ndoa ya dada ako.