Ushauri: Ndugu wameharibu ndoa ya dada yangu

Akiuawawa je na vipigo?

 
Ndoa ni ya watu wawili ukiweka mtu wa tatu lazima ivunjike...

Mwambie dada yako Aache utoto...
Aache na tayari ameshayakanyaga. Hapo ndio basi tena. Yaani ukae mbali na mwanaume miezi 11 utegemee aendelee kuamini wewe ni muaminifu kwake?
 
Katika watu wenye viherehere kwenye mahusiano mapya ni ndugu wa kike wa mwanamke especially Mabinamu,dada na wadogo za mke,mama,mama wadogo na mashangazi plus marafiki zake mke.

Hawa watu huwa wanajipa custody ya kuendesha affairs za uhusiano wa mtu utadhani ndoa inawahusu na wao ndani.

Wanawake miaka yote huwa wanahadharishwa kuwa makini na hawa viumbe na kuzingatia swala la faragha ya ndoa. Lakini kutwa kucha wao ni kukazana kuwapa hawa watu siri za faragha za ndoa matokeo yake hawa watu wanageuza maswala ya kwenye faragha ya ndoa yake kuwa public topics na kuharibu ustawi wa hiyo ndoa.

Kosa ambalo utafanya kama mwana ndoa ni kuendekeza kuongea mambo ambayo yanazungumzika ndani ya ndoa kuyapeleka nje ya ndoa. Hili jambo halijakaa sawa kabisa. Kama mwenzako anakubali kukaa chini na wewe kuongea maswala yenu then acha kutoa mambo nje ili upate attention ya kijinga kwa watu ambao hawatakupa msaada wowote ndoa yako itakapovunjika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…