Ushauri: Ndugu wameharibu ndoa ya dada yangu

Mkuu, sehemu zote3 zina mapungufu makubwa katika mgogoro huu.

1. Wewe:
katika mgogoro wa ndoa, nduguyo kakimbia kwa mumewe kukimbilia kwako kupata suluhu, wewe ukamfukuza kabla haujamuita shemeji yako na kukaa nao wote kusikiliza pande mbili kupata cha kushauri na kuamua, kama yangelikuzidi, watu wenye busara hawakosi wangelikusaidia kumaliza tatizo.

2. Mume:
Huyo jamaa kabeba dhima ya mgogoro mzima huo, kwa sababu mke kamkimbia bila kuchukua hatua za kumfuatilia alikokimbilia ili kumaliza tatizo(tatizo humalizwa kwa njia yoyote iwe kwa heri ama kwa shari).

Ni utoto kwa mume, mke aliyekukimbia kwa migogoro kudai arudi mwenyewe kabla ya kumfuata alikokimbilia kwenda kusuluhishwa.

3. Nduguzo anapoishi dada kwa sasa:

Kama waliamua kuweka msimamo wao wa kumhifadhi ndugu yao hadi hapo mgogoro utakapopatiwa ufumbuzi hawajafanya kosa lolote, bali kosa ni kulegeza masharti na kumuacha arudi mwenyewe kwa mume huku akiwa ameishi nje ya ndoa takribani mwaka mzima na tayari ni mja mzito.

Walitakiwa wabakie naye muda wote mpaka mwisho wa shauri.

Sijaona popote ulipowahusisha wazazi, yawezekana washafariki na kama ni wazima, kuimaliza issue hiyo ni jukumu lao la msingi sana.

Lakini sasa kama mmebakia ninyi wazawa, ni jukumu lenu kulinda haki za ndugu yenu.

Cha kufanya:
Ndoa tafsiri yake ni muunganiko wa jinsia mbili tofauti zilizo kubaliana kwa hiyari kuishi pamoja.

Katika muungano huo, mmoja wapo akiamua kuchoka kuishi na mwenzake huwa halazimishwi, ila kuna taratibu za kufuatwa ili kulinda haki ya kila mmoja wa wanandoa.

Mshauri dada yako akaanzie kwa viongozi wa kimadhehebu alikofungia ndoa na kama ni ndoa ya Kiserikali, basi akaanzie kwa mwenyekiti wa Serikali za mtaa huko kwa mumewe ili kuanza kudai haki zake za ndoa toka kwa mumewe.

Kama jamaa atakaza fuvu, Mwenyekiti ataisongesha Katani.

Kama kwenye Kata wakishindwa, shauri watalisongesha mahakamani.

Asikosee kuiruka ngazi hata moja, maana mahakama huangalia sana kama ngazi zote za usuluhishi zilifuatwa.

Huyo shemeji yenu inaonekana alishawadharau, angelikuwa na heshima, hata kama alikosewa na dada yenu vipi, ni upumbafu kiwango cha Sgr kwa mwanaume kupuuzia wito wa suluhu pindi mnapokuwa mmeingia kwenye mgogoro wa kindoa na mkeo.

Yanayoendelea sasa kati ya shemeji yako pamoja na dada yako, yapo juu ya uwezo wenu, jamaa ataendelea kuwapiga dana dana kwa sababu tayari alisha mhukumu ndugu yenu kwamba kabeba mimba nje ya ndoa na kwamba mimba si yake, wakati kuna misingi ya kisheria ya kulitambua hilo na si kwa hoja muflisi kama hizo.
Semina ndeeefu ila points less
 
Doh yani hapo sasa kama hela ipo na wapo tayari kufanya DNA waende tu sababu ukijaribu kuangalia kuna utata hapo mwanaume namuelewa na mwanamke namuelewa ila kuna jambo lazima lifanyike kuweka hali ya kuaminiana tena.
DNA ya nini ndg yg ?..... wewe ulisikia wapi mimba ya binadamu inakuwa miezi 11/12

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
nashukuru kwa majibu mazuri ila nina ushauri moja mdogo tu kama itaonekana inafaa 🐒

Pasina shaka yotote hupendezwi na hali hiyo ya mgogoro wa dada na shemeji yako kuidhoofisha nyumba yao wenyewe 🐒

jishushe pale chini kabisaa mpaka wakuone chizi unaehangaika na mambo ya watu, but focus yako ibaki pale pale kutafuta suluhu ya kudumu na kuwaleta pamoja hao ndugu wanafamilia....

Fanya mkutane physically.

Mawasiliano ya simu yawe tu katika kukumbushana mahali na muda wa kukutana ....

wew pamoja na ndugu yako wa karibu hata kama sio mzazi wako, nae shemeji yako pamoja na ndugu yake wa karibu, singependa pawepo na kiongozi wa kidini au jirani awepo kwa hatua hii ya mwanzo sana....

zungumzeni, wapeni nafasi pia hao wanaofarakana kila moja nae aseme kinagaubaga kwa upole lakini pia kwa upendo.
Make sure Focus ya mazungumzo yenu iwe ni solving the dispute in peace....
Kila anae zungumza hitimisho lake liwe ni Amani,
Hapana makelele na mabishano 🐒

Binafsi yangu na Imani yangu,
kwa Neema na Baraka za Mungu,

Mwenyezi Mungu ataonyesha njia na hatiamae suluhu ya changamoto hiyo itapatikana asilani 🐒
Ikiwa mwanaume anayo akili timamu hakuna jambo la kusolve na mwanamke mzinzi.
 
Mkuu, sehemu zote3 zina mapungufu makubwa katika mgogoro huu.

1. Wewe:
katika mgogoro wa ndoa, nduguyo kakimbia kwa mumewe kukimbilia kwako kupata suluhu, wewe ukamfukuza kabla haujamuita shemeji yako na kukaa nao wote kusikiliza pande mbili kupata cha kushauri na kuamua, kama yangelikuzidi, watu wenye busara hawakosi wangelikusaidia kumaliza tatizo.

2. Mume:
Huyo jamaa kabeba dhima ya mgogoro mzima huo, kwa sababu mke kamkimbia bila kuchukua hatua za kumfuatilia alikokimbilia ili kumaliza tatizo(tatizo humalizwa kwa njia yoyote iwe kwa heri ama kwa shari).

Ni utoto kwa mume, mke aliyekukimbia kwa migogoro kudai arudi mwenyewe kabla ya kumfuata alikokimbilia kwenda kusuluhishwa.

3. Nduguzo anapoishi dada kwa sasa:

Kama waliamua kuweka msimamo wao wa kumhifadhi ndugu yao hadi hapo mgogoro utakapopatiwa ufumbuzi hawajafanya kosa lolote, bali kosa ni kulegeza masharti na kumuacha arudi mwenyewe kwa mume huku akiwa ameishi nje ya ndoa takribani mwaka mzima na tayari ni mja mzito.

Walitakiwa wabakie naye muda wote mpaka mwisho wa shauri.

Sijaona popote ulipowahusisha wazazi, yawezekana washafariki na kama ni wazima, kuimaliza issue hiyo ni jukumu lao la msingi sana.

Lakini sasa kama mmebakia ninyi wazawa, ni jukumu lenu kulinda haki za ndugu yenu.

Cha kufanya:
Ndoa tafsiri yake ni muunganiko wa jinsia mbili tofauti zilizo kubaliana kwa hiyari kuishi pamoja.

Katika muungano huo, mmoja wapo akiamua kuchoka kuishi na mwenzake huwa halazimishwi, ila kuna taratibu za kufuatwa ili kulinda haki ya kila mmoja wa wanandoa.

Mshauri dada yako akaanzie kwa viongozi wa kimadhehebu alikofungia ndoa na kama ni ndoa ya Kiserikali, basi akaanzie kwa mwenyekiti wa Serikali za mtaa huko kwa mumewe ili kuanza kudai haki zake za ndoa toka kwa mumewe.

Kama jamaa atakaza fuvu, Mwenyekiti ataisongesha Katani.

Kama kwenye Kata wakishindwa, shauri watalisongesha mahakamani.

Asikosee kuiruka ngazi hata moja, maana mahakama huangalia sana kama ngazi zote za usuluhishi zilifuatwa.

Huyo shemeji yenu inaonekana alishawadharau, angelikuwa na heshima, hata kama alikosewa na dada yenu vipi, ni upumbafu kiwango cha Sgr kwa mwanaume kupuuzia wito wa suluhu pindi mnapokuwa mmeingia kwenye mgogoro wa kindoa na mkeo.

Yanayoendelea sasa kati ya shemeji yako pamoja na dada yako, yapo juu ya uwezo wenu, jamaa ataendelea kuwapiga dana dana kwa sababu tayari alisha mhukumu ndugu yenu kwamba kabeba mimba nje ya ndoa na kwamba mimba si yake, wakati kuna misingi ya kisheria ya kulitambua hilo na si kwa hoja muflisi kama hizo.
Mke aondoke kwa hiari yake nianze kutafuta suluhu ukweni?
Tabia za kike hizi
 
Kama ni mkristo ajiunge na kanisa la Mchungaji Christiana Shusho Mala..ya mwenzie.
 
Mke aondoke kwa hiari yake nianze kutafuta suluhu ukweni?
Tabia za kike hizi
Mkeo hawezi kuondoka kwa hiari bila ya migogoro bhana.

Na huwa kipindi hicho maelewano kati yake na wewe yameshindikana.

Lazima uelewe kuwa mgogoro unapotokea, kila mmoja hujiona yupo sahihi kwa upande wake hadi pale mtu mwingine atakapowasikiliza na kuchuja naneno ndiyo atagundua mwenye kosa ni yupi, aweza kuwa wewe au mkeo.

Sasa mke anapokimbilia kwao huwa kapima kuwa katika mgogoro huo yeye anakandamizwa, hivyo kwenda kwao huwa ni njia ya kutafuta suluhuhasani.

Hivyo kumfuata kwako kwao siyo tabia ya kike bali ni njia sahihi ya kumaliza mgogoro wenu.
 
Wakuu,

Mwezi Mei mwaka jana, kuna dada yangu mmoja aligombana na mumewe na kukimbilia kwangu. Nilipoongea na mumewe, akasema yeye hana tatizo nae, arudi tu wayamalize.

Nilipomsihi dada arudi wakayamalize, akawa hataki, anang'ang'ania aendelee kuishi kwangu tu. Nikaamua kumfukuza aondoke, kwangu sina nafasi ya kuhifadhi mke wa mtu mimi.

Kumbe alivotoka kwangu akahamia kwa ndugu wengine wakampokea akaishi. Nikawa naskia tu, sasa dada anakaa kwa ndugu flani, mara kahamia kwa ndugu mwingine, kwa mumewe kagoma kabisa kurudi.

Nimewasihi ndugu zangu sio vizuri kukaa na mke wa mtu majumbani kwenu, hawataki kunielewa, wanadai namtetea sana mume wa dada yangu, nataka mpk afe ndo nijue mumewe ni mnyanyasaji wa kijinsia.

Wakasema kama mumewe anamtaka mkewe basi amfate mwnyw ukweni na akaiombe radhi familia, vinginevyo asahau kabisa kama alishawai kumuoa ndugu yao. Nikaamua kujiweka kando na hayo mambo.

Amekuja kurudi kwa mumewe mwezi huu tar 02 (miezi 11 imepita) akiwa na mimba ya kubwa sana. Mumewe kagoma kabisa kumpokea akidai mkewe aliondoka akiwa hana mimba, inakuaje arud kwake akiwa na mimba? Hiyo mimba sio yake.

Nmemhoji dada yangu, anadai ile mimba ni ya mumewe 100% na aliondoka nayo, ila alishindwa kumtaarifu mumewe kutokana na ugomvi uliokuepo kati yao.

Ndugu waliomhifadhi miezi yote hiyo wananipigia kunisihi niongee na shemeji yangu, ampokee mkewe maana ni mjamzito sana anaweza kujifungua muda wowote. Nimewaambia hiyo kazi siifanyi, fanyeni nyie wenyewe mlioyasababisha. Wanadai jamaa hawezi kuwaelewa, walishagombana tayari na hawapokelei kabisa simu zao.

Nmemtafuta shemeji, anachosema ni kwamba, kama kweli mkewe aliondoka na mimba yake ile mwezi Mei mwaka jana walipogombana, basi mwaka huu mwezi January au February alitakiwa awe tayari keshajifungua mtoto.

Sasa hivi ni mwezi March, ni miezi 11 tangu mkewe aondoke bado ni mjamzito hajajifungua, hivyo kwa vyovyote vile ile mimba sio yake. Kaipatia huko huko kwa ndugu zake na kwa tafsiri hiyo, hamna ndoa tena hapa.

Kiukweli mpaka sasa kichwa kimepata moto, sielewi nifanye nini dada yangu akae sawa maana analia muda wote (na hii mimba alionayo nahisi itamletea shida au huenda akajidhuru).

Pia nishauri nini kifayike ikiwezekana arudiane na mumewe, maana jamaa hataki hata kumskia mkewe wala habari zake na kahama kabisa pale nyumbani, kaenda kupanga sehemu nyumba nyingine kabisa.

Nawasilisha. 🙏
Kwa mara ya kwanza umeandika uzi mfupi. Hongera mkuu umeanza ku improve
 
Ilkua sio mara ya kwanza au ya pili,KILA aligombana na mumewe anakimbilia kwangu, This time sikutaka tena huo upuuzi
Wewe ndo mzembe kwa nn usingemuita uyo mume mkaja kuyaongea na kuyamaliza wakiwa pande zote mbili wapo wewe utamwambiaje tu arud kwa mumewe bila kujua sababu zilizomfsnya aondoke
 
Mkeo hawezi kuondoka kwa hiari bila ya migogoro bhana.

Na huwa kipindi hicho maelewano kati yake na wewe yameshindikana.

Lazima uelewe kuwa mgogoro unapotokea, kila mmoja hujiona yupo sahihi kwa upande wake hadi pale mtu mwingine atakapowasikiliza na kuchuja naneno ndiyo atagundua mwenye kosa ni yupi, aweza kuwa wewe au mkeo.

Sasa mke anapokimbilia kwao huwa kapima kuwa katika mgogoro huo yeye anakandamizwa, hivyo kwenda kwao huwa ni njia ya kutafuta suluhuhasani.

Hivyo kumfuata kwako kwao siyo tabia ya kike bali ni njia sahihi ya kumaliza mgogoro wenu.
nasisitiza mwanaume wa ukweli haendi ukweni kutafuta suluhu na mkewe.
 
Wakuu,

Mwezi Mei mwaka jana, kuna dada yangu mmoja aligombana na mumewe na kukimbilia kwangu. Nilipoongea na mumewe, akasema yeye hana tatizo nae, arudi tu wayamalize.

Nilipomsihi dada arudi wakayamalize, akawa hataki, anang'ang'ania aendelee kuishi kwangu tu. Nikaamua kumfukuza aondoke, kwangu sina nafasi ya kuhifadhi mke wa mtu mimi.

Kumbe alivotoka kwangu akahamia kwa ndugu wengine wakampokea akaishi. Nikawa naskia tu, sasa dada anakaa kwa ndugu flani, mara kahamia kwa ndugu mwingine, kwa mumewe kagoma kabisa kurudi.

Nimewasihi ndugu zangu sio vizuri kukaa na mke wa mtu majumbani kwenu, hawataki kunielewa, wanadai namtetea sana mume wa dada yangu, nataka mpk afe ndo nijue mumewe ni mnyanyasaji wa kijinsia.

Wakasema kama mumewe anamtaka mkewe basi amfate mwnyw ukweni na akaiombe radhi familia, vinginevyo asahau kabisa kama alishawai kumuoa ndugu yao. Nikaamua kujiweka kando na hayo mambo.

Amekuja kurudi kwa mumewe mwezi huu tar 02 (miezi 11 imepita) akiwa na mimba ya kubwa sana. Mumewe kagoma kabisa kumpokea akidai mkewe aliondoka akiwa hana mimba, inakuaje arud kwake akiwa na mimba? Hiyo mimba sio yake.

Nmemhoji dada yangu, anadai ile mimba ni ya mumewe 100% na aliondoka nayo, ila alishindwa kumtaarifu mumewe kutokana na ugomvi uliokuepo kati yao.

Ndugu waliomhifadhi miezi yote hiyo wananipigia kunisihi niongee na shemeji yangu, ampokee mkewe maana ni mjamzito sana anaweza kujifungua muda wowote. Nimewaambia hiyo kazi siifanyi, fanyeni nyie wenyewe mlioyasababisha. Wanadai jamaa hawezi kuwaelewa, walishagombana tayari na hawapokelei kabisa simu zao.

Nmemtafuta shemeji, anachosema ni kwamba, kama kweli mkewe aliondoka na mimba yake ile mwezi Mei mwaka jana walipogombana, basi mwaka huu mwezi January au February alitakiwa awe tayari keshajifungua mtoto.

Sasa hivi ni mwezi March, ni miezi 11 tangu mkewe aondoke bado ni mjamzito hajajifungua, hivyo kwa vyovyote vile ile mimba sio yake. Kaipatia huko huko kwa ndugu zake na kwa tafsiri hiyo, hamna ndoa tena hapa.

Kiukweli mpaka sasa kichwa kimepata moto, sielewi nifanye nini dada yangu akae sawa maana analia muda wote (na hii mimba alionayo nahisi itamletea shida au huenda akajidhuru).

Pia nishauri nini kifayike ikiwezekana arudiane na mumewe, maana jamaa hataki hata kumskia mkewe wala habari zake na kahama kabisa pale nyumbani, kaenda kupanga sehemu nyumba nyingine kabisa.

Nawasilisha. 🙏
Anko wangu siku aligombana na mkewe na ulikuwa usiku wa saa sita wanapokaa ni karibu na wazazi wote wa mke na mume.

Walivyogombana mwanamke usiku usiku akaenda kwao akawakuta wazazi wake wamelala akawagongea kuulizwa haya vipi saizi akasema mmewe kampiga kwaiyo kaona bora akimbie asije akafa

Mama mtu akataka kumkaribisha ndani ila mzee akagoma akasema hizo taarifa ni za upande mmoja kwaiyo hawezi kumpokea kwani yeye ni mke wa mtu hata kama ni mwanae, mzee akamtimua japo ni usiku sana.

Anko alivoona mke kaondoka na hajui alipokwenda alienda kutoa taarifa kwa kwa wakwe kwamba mkewe kakimbia hajui alipokwenda na usiku ule basi mzee akamwambia alifika muda huu tukamrudisha huko basi alienda home ila hakumkukuta akaingia ndani akambonji hata dk kadhaa hazikukata anasikia mtu anagonga kufungua ni mkewe mahojiano yakaanza ila baadae walielewana na maisha yakaendelea hadi leo wapo pamoja.

Funzo: hapo hukutakiwa kumpokea kabisa hata kwa sekunde ila ungemwambia aje na mwenzie wajieleze wote ungenusuru ndoa ya dada ako.
 
Uwa nakuona una hekima na busara sana hapa umepotoka pakubwa sana. Umekosea umemtukana na kumdhalilisha mtu bila aibu.
Msamehe,
Nafikiri alichofikiria ni kuwa, huyu mleta uzi ni kaka wa mchongo wa huyo dada, (kaka koko)
Hivyo alimpokea--alimpokea kweli na baadaye akamshauri aende kwa nduguze.
Nje na mawazo hayo amekosea mno

Ushauri wangu ni kwamba ahangaikei afya yake ajifungue salama, akae bench mpaka mme wake atakapofanya sub🤣🤭
 
Back
Top Bottom