Ushauri: NEMC fanyeni haya ili kupunguza kelele za muziki mtaani

Ushauri: NEMC fanyeni haya ili kupunguza kelele za muziki mtaani

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Nafaham upo ugumu mkubwa wa kushughulika na watu wanaoamini KERO ni haki yao!

Yaani kuna watu wanajimilikisha haki ya kuwakera wengine!
Na wanaoamini wako sahihi!

Zamani kukuta spika ya disco kanisani ilikuwa HAKUNA! Na watu waliogopa kucheza sebene kanisani lakini hivi Leo ni kawaida sana!

Miziki mikubwa kwenye bar, makanisa na misikiti imekuwa kawaida na wanaamini ni HAKI YAO!

NEMC FANYENI HIVI KUONDOA TATIZO!
1. Wekeni viwango elekezi vya decibel's ya chombo cha mziki kwa kuzingatia uwiano wa chumba/jengo (Volume ratio) ya chumba na muwape vibari!

Fomu za vibari NEMC zijazwe kupitia serikali ya mtaa na mtendaji wa mtaa (hii itakuwa bure kwa vyombo vyote vidogo vya mziki mfano! Koni spika, na vinanda vidogo (piano)

2. Spika zote kubwa kuanzia decibels elekezi mtakazopanga na kuendelea kutokana na uwiano wa jengo.
Hakikisheni Zinapatiwa kibali maalum kutoka NEMC

MFANO! spika moja kubwa kwa mwaka ilipiwe 10MIL na hakikisheni nakala ya stika ya vibari vyenu vinabandikwa inje ya jengo husika
Vikionesha tarehe, muda wa matumizi, na ukomo!
(Hakikisheni na mkague vibari vyenu VALID kama vimebandikwa inje)

Asilimia 30% ya malipo wapeni mtaa husika kwa maendeleo ya mtaa!

HAKIKISHENI HAKUNA MTU ANAYETUMIA SPIKA KUBWA YENYE DECIBEL'S kinyume na kiwango elekezi pasipo USAJILI!

NA MJIPAMBANUE KWAMBA HAMUWAKATAZI KUTUMIA BALI MNAWASAJILI NA KUWAPA MATUMIZI ELEKEZI! Anaeshindwa aaache!

Nahilo lifanyike kitaifa!

Na hizi ndo ajira zenyewe! Kuondoa kero ni fursa ya pesa kwa serikali na ni ajira kwa vijana!

oparesheni hiyo waibatize jina baya! Mfano!
OPARESHENI TOKOMEZA SPIKA NZIGE MTAANI
 
Research sheria za serikali za mitaa (municipalities )zipo sheria zinazohusu mambo haya including maduka ya kiti moto,utekelezaji ni zero
 
Kweli,
Yaani hawa wachoma cd na makanisa uchwala wanakera sana
 
Kweli,
Yaani hawa wachoma cd na makanisa uchwala wanakera sana
Dawa nikulifanya zoezi kwa ujumla bila kumtaja mtu watajipambanua ndani ya zoezi! Wasipokata kibari tunawasondeka lupango mwezi mmoja na kutaifisha vyombo vya mziki ambavyo havina usajili
 
Sio misikiti tu,hata makanisa hasa huko Mbeya na Arusha
 
Umetisha mzee. Sheria ziongee.
Wapatiwe muda kuhakikisha wanajisajili wote! NEMC Kwa kushirikiana na Wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na serikali za mitaa na manispaa wasaidie kufuatilia hilo
 
Sio Siri mkuu yaani huku mtaani kelele za muziki zimezidi mmnoo, natamani nitafute mahala,niikakae main alone kiumbe asinisumbue.
 
Back
Top Bottom