Tatizo liko kwenye usimamizi, sheria zipo lakini viongozi watendaji ngazi za chini wanaona aibu kusimamia sheria. Mfano kero ya kelele kwenye makazi ya watu, boda boda wanaofunga vyombo vya muziki kwenye piki piki zao...Haya ni mambo yanayoweza kushughulikiwa ndani ya wiki moja watu wakashika adabu....
Siku za hivi karibuni umezuka mtindo wa madereva wa boda boda kuburuza nondo, mbao, milango kwenye lami badala ya kupakia mzigo, viongozi wa Serikali za mitaa wapo wanaona na wanawajua wakiukaji wa sheria, lakini wamefumba macho na masikio, matokeo yake watu wa usalama barabarani na Polisi waneona fursa za kujinufaisha!.