USHAURI: Ni vema tukajenga utamaduni wa kujisomea vitabu na kuwajengea watoto utaratibu huo

USHAURI: Ni vema tukajenga utamaduni wa kujisomea vitabu na kuwajengea watoto utaratibu huo

AfricaUnited

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2010
Posts
2,367
Reaction score
1,293
"Anyone who stops learning is old, whether at twenty or eighty. Anyone who keeps learning stays young. The greatest thing in life is to keep your mind young.Henry Ford"

Ni dhahiri kuwa nchi nyingi za africa na baadi nje ya africa,asilimia kubwa ya watu hutumia mda mwingi kuangalia television,kusoma magazeti ya udaku,na mambo yasiyo yamsingi.

Pia mimi nilishakuwa na tabia hiyo wakati nikiwa kidato cha pili, lakini baada ya kuona hayana msingi sana, basi nkaanza kuwa na utaratibu wa kujisomea vitabu vya ziada na kupata kujua mengi kwa kadiri nilivyoweza kupata maarifa kwenye vitabu hivyo.

Sasa ni muda wa kuyafanyia kazi yale niliyo jifunza, na bado naendelea kujifunza kila siku.

Ni vema pia ukasoma nyuzi hizi: Utamaduni wa kujisomea, kuelewa na siasa za Tanzania & Hivi ndivyo tabia ya kupenda kujisomea ilivyoboresha Maisha yangu. Inawezekana hata kwako pia
 
Inaaminika reading is fun to mental, ila kwa sisi waswahili reading is the mind torturing.
 
Yes kusoma ni muhimu sana haina mjadala!!!!
Ila nini unasoma ndio tofauti huanzia hapo!!!!

Waandishi wamegawanyika "mental window na ideological inclination" ya muandishi zinawafanya waandike mambo fulani kwa nia fulani!!!

Upotoshaji upo,kuficha uhalisia wa mambo na hata de railing ipo sana kwenye uandishi so tuwe makini sababu wenzetu wanajua kuwa ukidumaza/ kuyumbisha akili ya msomaji basi kumtawala ni rahisi sana!!!!!

Lakini pia kujua haya ni lazima uwe msomaji na mlinganishaji pia!!

Waone pia Dark City, NasDaz, Activister gfsonwin, The Boss, King'asti, Pasco, venine, Mbeky, watu8
 
Last edited by a moderator:
kusoma ni muhimu.ila inategemea na nini unasoma. it is not enough to read, but read something that is worth reading. Vitabu vizuri vinapanua uelewa na jinsi ya kufikiri, vinajenga concentration (hii ni muhimu sana especially kwa watoto).

Ila utamaduni wa kujisomea vitabu huwa unajengwa, hauji ghafla. wengi wa watu wanaopenda kujisomea wametokea kwenye families ambazo usomaji unapewa umuhimu/ kipaumbele. ndio maana wazungu wanawasomea vitabu wtt wao tokea wakiwa wadogo, wanawanunulia story books

kuna umuhimu wa kuwajengea wtt wetu utamaduni wa kusoma vitabu, mtoto anayependa kusoma anakuwa na uwezo mkubwa wa ku-concetrate hata kwenye masomo (sio ya lugha na history tu, masomo yote). so, hata unapomnunulia mtt kitabu, jaribu kutafuta kile ambacho kita-stretch imaginations zake, kitamfanya aweze ku-connect anayosoma na real life anayoishi, na hata wanayoishi wengine
 
" Anyone who stops learning is old, whether at twenty or eighty. Anyone who keeps learning stays young. The greatest thing in life is to keep your mind young.Henry Ford"
ni dhahiri kuwa nchi nyingi za africa na baadi nje ya africa,asilimia kubwa ya watu hutumia mda mwingi kuangalia television,kusoma magazeti ya udaku,na mambo yasiyo yamsingi.pia mimi nilishakuwa na tabia hiyo wakati nikiwa kidato cha pili,lakini baada ya kuona hayana msingi sana ,basi nkaanza kuwa na utaratibu wa kujisomea vitabu vya ziada na kupata kujua mengi kwa kadiri nilivyoweza kupata maarifa kwenye vitabu hivyo,sasa ni mda wa kuyafanyia kazi yale niliyo jifunza,nabado naendelea kujifunza kila siku.

Pamoja na kwamba nakubaliana na wewe katika mambo mengi kuhusu hoja yako, naomba pia kukumbusha kuwa siyo masikini tu wanaopenda udaku na umbeya. Ndiyo maana hata hao unaowasifia wamebobea katika udaku na umbeya.
 
Yes kusoma ni muhimu sana haina mjadala!!!!
Ila nini unasoma ndio tofauti huanzia hapo!!!!

Waandishi wamegawanyika "mental window na ideological inclination" ya muandishi zinawafanya waandike mambo fulani kwa nia fulani!!!

Upotoshaji upo,kuficha uhalisia wa mambo na hata de railing ipo sana kwenye uandishi so tuwe makini sababu wenzetu wanajua kuwa ukidumaza/ kuyumbisha akili ya msomaji basi kumtawala ni rahisi sana!!!!!

Lakini pia kujua haya ni lazima uwe msomaji na mlinganishaji pia!!

Waone pia Dark City, NasDaz, Activister gfsonwin, The Boss, King'asti, Pasco, venine, Mbeky, watu8

Uko sahihi mkuu,

Suala la kujisomea linatusumbua. Pia kuna watu wengi hata wakisoma wanashindwa kuwa makini. Na hili husababisha mikanganyiko pale ambapo mtu anapotumia maneno ambayo si sahihi katika maana au matamshi.

Unaweza kukuta mtu mzima kabisa bila aibu anaongelea uchaguzi ila anatumia neno "ERECTION" badala ya "ELECTION"!!
 
kusoma ni muhimu.ila inategemea na nini unasoma. it is not enough to read, but read something that is worth reading. Vitabu vizuri vinapanua uelewa na jinsi ya kufikiri, vinajenga concentration (hii ni muhimu sana especially kwa watoto).

Ila utamaduni wa kujisomea vitabu huwa unajengwa, hauji ghafla. wengi wa watu wanaopenda kujisomea wametokea kwenye families ambazo usomaji unapewa umuhimu/ kipaumbele. ndio maana wazungu wanawasomea vitabu wtt wao tokea wakiwa wadogo, wanawanunulia story books

kuna umuhimu wa kuwajengea wtt wetu utamaduni wa kusoma vitabu, mtoto anayependa kusoma anakuwa na uwezo mkubwa wa ku-concetrate hata kwenye masomo (sio ya lugha na history tu, masomo yote). so, hata unapomnunulia mtt kitabu, jaribu kutafuta kile ambacho kita-stretch imaginations zake, kitamfanya aweze ku-connect anayosoma na real life anayoishi, na hata wanayoishi wengine

Kweli kabisa,

Ndiyo maana hata maginius wa shule za kata wanasumbuka sana kwani hawapati nafasi ya kujisomea mambo ya taaluma na yale ya maisha ya kawaida.
 
Uko sahihi mkuu,

Suala la kujisomea linatusumbua. Pia kuna watu wengi hata wakisoma wanashindwa kuwa makini. Na hili husababisha mikanganyiko pale ambapo mtu anapotumia maneno ambayo si sahihi katika maana au matamshi.

Unaweza kukuta mtu mzima kabisa bila aibu anaongelea uchaguzi ila anatumia neno "ERECTION" badala ya "ELECTION"!!
miss you Babu.

Habari za weekend?

Msalimie Bibi.
 
Uko sahihi mkuu,

Suala la kujisomea linatusumbua. Pia kuna watu wengi hata wakisoma wanashindwa kuwa makini. Na hili husababisha mikanganyiko pale ambapo mtu anapotumia maneno ambayo si sahihi katika maana au matamshi.

Unaweza kukuta mtu mzima kabisa bila aibu anaongelea uchaguzi ila anatumia neno "ERECTION" badala ya "ELECTION"!!

Ha ha ha aaaa babu unanikumbusha tuko form three jamaa kwenye mtihani wa English masuala ya who,whose,which kaacha nafasi finyu na kutuchimbisha visiki kisa kaandika matusi kwa mujibu wa mwalimu!!!!

Jamaa aliandika A boy whose penis red badala ya A boy whose pen is red!!!!!
 
Naafiki kabisa.

Wazazi ni jukumu lao kukuza mazoea na desturi ya kujisomea. Wengi hatufanyi hivyo. Shule zetu zinatakiwa ziwe na mfumo wa kuwazoesha vijana kujisomea.

Mfumo wetu wa elimu, kwa bahati mbaya sana, haujengi kabisa mazoea ya kusoma. Mazoea ya kusoma ndiyo yanapelekea vijana huko mbele kuwa na uwezo mkubwa wa kujitafutia maarifa iwe ni katika sayansi, teknolojia, sanaa mbalimbali, na masomo yote.

Nimepata kuangalia vizuri mifumo ya elimu sehemu nyingine duniani. Watoto wanafunzwa kusoma na kusoma sana. Kutoka shule ya msingi. Wanapoendelea na masomo zaidi, wanasoma mabuku makubwa zaidi katika masomo mbalimbali. Lakini kwanza walifunzwa kusoma kwa kusoma vitu vinavyofurahisha watoto.

Mambo yamekuwa mabaya hapa nchini kiasi kwamba mara kadha nimeenda kwenye duka la vitabu na kuulizia riwaya zilipo nikaulizwa za Form 4 or Form 6. Yaani kusoma huko ni kwa ajili ya mitihani tu. Hapo ndipo ninapoona kwamba taifa limepotea. Ni dalili dhahiri kwamba hakuna kusoma na hatuna mazoea ya kujitafutia maarifa. Nikiangalia mashuleni na vyuoni pia sishangai. Ni madesa kwa kwenda mbele.

Tatizo ni kwamba tunao wataalamu, tena wengine maprofesa, wanapopata nafasi badala ya kuboresha mambo, wanabuni Division 5 au "Ufaulu wa chini" wakati watu wamefeli kwa kweli. Nao wenyewe watoto wao wanaenda kwenye shule ghali.

Jamani, tubadilike.
 
ukitaka kumfichia mtu mweusi hela weka kwenye kitabu...
kweli kabisa.ila ukitaka usiikute basi uweke kwenye gazeti la udaku au kwenye majarida ya mapenzi.humo watu wengi wanayapenda sana hayo na wanaweza kuadisia yote aliyoyasoma.
 
yes kusoma ni muhimu sana haina mjadala!!!!
Ila nini unasoma ndio tofauti huanzia hapo!!!!

Waandishi wamegawanyika "mental window na ideological inclination" ya muandishi zinawafanya waandike mambo fulani kwa nia fulani!!!

Upotoshaji upo,kuficha uhalisia wa mambo na hata de railing ipo sana kwenye uandishi so tuwe makini sababu wenzetu wanajua kuwa ukidumaza/ kuyumbisha akili ya msomaji basi kumtawala ni rahisi sana!!!!!

Lakini pia kujua haya ni lazima uwe msomaji na mlinganishaji pia!!

Waone pia dark city, nasdaz, activister gfsonwin, the boss, king'asti, pasco, venine, mbeky, watu8

ni kweli mkuu maana kuna vitabu vingine vinakuwa vinapotosha,ni vizuri sana kuwa makini.kunafalsafa moja inasema"tatizo si anaedanganya,tatizo ni kwa anaedanganywa"
 
Back
Top Bottom