USHAURI: Ni vema tukajenga utamaduni wa kujisomea vitabu na kuwajengea watoto utaratibu huo

USHAURI: Ni vema tukajenga utamaduni wa kujisomea vitabu na kuwajengea watoto utaratibu huo

"Ukitaka kumficha mwafrika weka ujumbe kwenye vitabu,mie natumia mziki kufikisha ujumbe kwa watu"

"Mie mtoto wa kichaga desturi yangu ku-hustle usinletee upimbi kwenye maswala ya shilingi,sibishani na promoter usipofika dau siimbi"

~~~~~~~~~~~~~~~~~~
KAKA VODA MILIONEA UNAPOTEZA VIPAJI.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
 
nahisi kama tunachanganya madesa hapa. Kama ninimeelewa mada inaongelea umuhimu wa kujijengea tabia ya kusoma - kwamba kuna maarifa mengi kwenye maandiko. Si kwamba mtoto/mtu akijua kusoma ndo atakuwa na tabia njema, ila kusoma ni mojawapo ya tabia njema. Mzazi anatakiwa kulea mwili, akili na roho ya mwanae. Kumfundisha tabia ya kusoma ni moja, kumpeleka ibadani ni kulea roho yake ingawa kuna watu hawajui mlango wa nyumba za ibada lakini wana maadili mema. Mtoto kukimbiza darasani inategemea iq yake inayojumuisha uwezo wake wa kuelewa na kukariri. Kuna ambaye hakimbizi darasani lakini anajua mambo mengi kuliko anayekimbiza. Kuna wanaokimbiza halafu ukiwauliza kitu ambacho hakiko kwenye mtaala anakwambia hicho hatujafundishwa.

Wapo pia watoto/watu ambao wanazaliwa na tabia ya kupenda kusoma ingawa kwao hawakuwahi kuona vitabu wakiwa watoto mpaka walipoingia shuleni. Hawa utawakuta wameishia la saba lakini wana maarifa mengi kuliko wenye digrii ambao hawapendi kusoma. Mmojawapo ninayemfahamu ni mrisho mpoto. Huyu kafika la saba, anapenda kusoma na ana kipaji cha kutunga mashairi na kuhadithia. Lakini mashairi yake yana kiwango cha juu cha ufahamu wa maswala ya kisiasa na kiuchumi ya hii jamii. Kuna msomi ukimuuliza swala flani linalohitaji mtazamo tu wa jumla anakwambia "well, mimi nimesomea hiki, hivyo hayo mambo mimi sijayasomea."
 
hapana hujakutana na wanafunzi hadari ndio maana unasema hivo, hasa kwa level ya chini mwenye akili nyingi na memory kubwa ndio wa mwanzo darasani
mkuu hatuzungumzii tu kuongoza darasani tunazungumzia maarifa kwa ujumla. watu wengi tunafika chuo hatuna maarifa mengine ya dunia sababu maishani tulikuwa tunasoma kwaajili ya kuongoza na kufaulu na sio kwasababu ya kiu ya maarifa.
 
Pale Ubungo bus terminal nilikuta jamaa anauza vitabu shilingi elfu moja moja vitabu vizuri sana nilibeba vitano. Binafsi ninajitahihi kusoma siku hizi karibia kila angle yaani science, social science etc. Jamani tujisomee na tuwajengee watoto utamaduni wakujisomea.
 
mkuu hatuzungumzii tu kuongoza darasani tunazungumzia maarifa kwa ujumla. watu wengi tunafika chuo hatuna maarifa mengine ya dunia sababu maishani tulikuwa tunasoma kwaajili ya kuongoza na kufaulu na sio kwasababu ya kiu ya maarifa.
kwa iyo maarifa yanajengwa kwa kusoma vitabu?
 
vitabu vinaelezea siri ya mitungi na masomo yanaelezea projectile kuna uhusiano gani
mtu kama hawezi kusoma na kumaliza kitabu cha androko na simba usitegemee akienda shuleni atakuwa anasoma nelkon. mambo haya yanahusiana na tabia kujisomea hujengeka polepole.
 
Red Giant;Wandugu age tuliyopo sasa inaitwa information age.

Bila kujisomea hii age itatusumbua sana.

Ilikushindana nayo lazima tuwe watu wa kujisomea na tabia ya kuujisomea huanzia nyumbani.

Mimi ni msomaji sana wa vitabu na credit zote nampa mama yangu. Maza ni la saba na anakazi ya kima cha chini lakini ni mtu anapenda sana kujisomea.

Nyumbani kulikuwa na vitabu kama mwanamalundi, kikosi cha kisasi, tutarudi na roho zetu, dunia uwanja wa fujo, abunuasi, adili na nduguze na vingine vingi na magazeti mengi tu.

Kwa hiyo kitu cha kwanza hakikisha vitabu vipo nyumbani. Watoto ni wadadisi watasoma tu, sasa wewe umejaza bongo movie na series za kikorea halafu unaona ufahari, kabati zima na hamna hata kitabu kimoja.

Dingi hujawahi hata kurudi na gazeti we unarudi na merlin, legend of the seeker na mambo kama hayo unafikiri watoto watapenda kujisomea?

Kama wewe uko hivi nakushauri uchonge shelf la vitabu na uanze kununua vitabu, mbona bei ni sawa na series za jaki bawa.

Jambo la pili ni wewe pia kuweka mfano kwa kujisomea, hata kama haupendi just do it for the sake of your children. Usitegemee wanaokupenda kujisomea wakati wewe mwenyewe ni mtu wa Isidingo na la Mujer.
kaka point taken ila kumbuka kwa nchi kama yetu ambao tabaka kubwa ni maskini na hawajasoma ni ngumu kuelewa hali halisi ya jinsi mambo yanavyoenda,na hata kama watajua basi hawatatilia uzito mkubwa saaana...ndiyo maana tunasema taaluma ya mtoto it is a dual process,both state and individuals are concerned to make it foster...na kaka kumbuka nyakati ambazo umesoma wewe na sisi watoto wa kata are quite different,...kipindi hicho mtoto alikuwa akifeli mara nyingi ilikuwa ni yeye mwenyewe aidha(utukutu uliokithtiri),au(hali ngumu ya maisha nyumbani) au(serikali iwe imeshindwa kumuendeleza).Ila yote kwa yote ujumbe wako ni mzuri lakini mpaka sasa umetufikia sisi watanzania watanzania wachache saaana almost 15 percent wenye umeme na pia 0.000002 wenye access na internet,mathalani siyo watanzania wote tuko jamiiforums...na hata kama tupo basi tumejikita TROLLING kwenye JUKWAA LA SIASA na MAPENZI...IN OTHER WAYS I CAN SAY THIS IS A PARADOX,YOU HAVE ADDRESSED A RIGHT ADVICE TO A WRONG PERSON,..thou some of us have taken it because it does matter.,..
Sasa mkuu RED GIANT illiteracy is a global catastrophy,wewe labda ungetoa ushauri jinsi gani tutawafikia wale wazazi ambao wana watoto but ukali wa maisha umewafanya washindwe kufanya kama mama yetu alivyokujengea mazingira wewe mazuri.
😛eace: :tea:

😛eace:😛eace:

NI KUJUMU LETU SOOOOOOTE.
cheers
 
mtu kama hawezi kusoma na kumaliza kitabu cha androko na simba usitegemee akienda shuleni atakuwa anasoma nelkon. mambo haya yanahusiana na tabia kujisomea hujengeka polepole.
nelkon, beckhouse, or trantor utasoma tu ukifika stage husika hata kama ulikua husomi vitabu, na kuna tofauti kubwa kati ya vitabu vya ngano na vya sayansi, vitabu vingi unavozungumzia ni vitabu vya story za kutunga ambazo ni atractive au zile story zilizotokea zamani. sio watu wote wanapenda hizi story. mtoto akipenda mpe ila akiwa hapendi mfunze mengine sio lazima kusoma kitabu. kitu muhimu mtoto ni kua na good behavior.
 
hivyo vitabu nimevitaja nilikuwa navisoma utotoni siku hizi nasoma vitabu serious na msingi wake ni hizo ngano. nilipokuwa advance topic nyingi nilizisoma mwenyewe kwenye vitabu sababu nilijengewa kupenda kujisomea. hapo kwenye red nashindwa kuelewa utakuwa baba wa namna gani!?
 
"lazy affair dad.
 
Back
Top Bottom