Ushauri: Nichague ipi kati ya BMW X3 2013 au Subaru Forester 2013

Duksi

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Posts
229
Reaction score
576
Kati ya gari hizi mbili ambazo naona kwasasa zinanunuliwa sana kwenye miji mikubwa zikiwa na namba E, ipi inafaa zaidi kwa matumizi ya kawaida ya mjini.

Zote ni 2.0 AT petrol za mwaka 2013/14 na zote ni all wheel drive/4WD.
Wenye uzoefu na hizi gari msaada.

Budget yake ni kuanzia 43m mpaka 50m kwasasa.


 
Sijui kuhusu Subaru, ila achana na iyo BMW 2.0 achana nayo kabisa, BMW sio wazuri sana kwenye kutengeza 4 cylinders inline.

Nashauri kama utataka BMW chukua ya kuanzia cc 2500 ya 6 cylinders. Kwa huo mwaka itakua BMW F25 2013, 3.0L N52 hii haina turbo au N55 I6 hii ina twin turbo (sikushauri sana).

Ukijipush ya 2014 waliifanyia update kidogo ya muonekano (facelift)
Mfano kabla ya Facelift 2013 ilikua hivi:


Hafu baada ya Facelift ikawa hivi:


Hawa jamaa kwenye 6 cylinders walituliza mabichwa aisee.
 

Kwahiyo mkuu hata X1 1st generation cc 1990 sio reliable? Ndo maana wengi wanazicheua bei ya kutupa
Unakuta mpya kbs namba DV au DZ inauzwa 15 tu
 
Nashauri afuate ushauri huu.
 
Kwahiyo mkuu hata X1 1st generation cc 1990 sio reliable? Ndo maana wengi wanazicheua bei ya kutupa
Unakuta mpya kbs namba DV au DZ inauzwa 15 tu
Kabla haujanunua BMW, angalia mtaani kwenu unaziona namba C ngapi? Au namba D za mwanzo mwazo DA, DB, DC hadi kama DJ kurudi. Kama hamna jiulize zilikua hazinunuliwi au zimeenda wapi? (Hii sio topic kuu just jiulize mwenyewe)

Upo sahihi. X1 ya E84 nayo wana 4 cylinders engine yenye code N46 na wana 6 cylinders engine yenye code N52 na N55 ya turbo.

Oya, N52 engine aisee.

Nikiamini mtu anaenunua gari la Mil 40+ (mtoa mada) hawezi sema ulaji wa mafuta vipi?
 
Nina swali kidogo ndugu yangu kuhusu BMW hasa baada ya ushauri wako juu ya 4 cylinder engine...hata Mimi Nina hesabu juu ya BMW 320i au 328i( 6- inline engine) vipi Kwa uzoefu wako ni ipi itanifaa zaidi
 
Nina swali kidogo ndugu yangu kuhusu BMW hasa baada ya ushauri wako juu ya 4 cylinder engine...hata Mimi Nina hesabu juu ya BMW 320i au 328i( 6- inline engine) vipi Kwa uzoefu wako ni ipi itanifaa zaidi
Ukiona 320i ujue ina cc 1990 kwahiyo ni 4 cylinders inline.

Hapo anzia 323i, 325i, 328i (kama utaipata hizi adimu) izo zote zina cc 2500 na uyo 328i na mwenzie 330i wana cc3000.

Hao wazee ni 6 cylinder N52 na N54 na N55 (turbo) vyunguvya Mjerumani wa Munich.
 
Kitu Forester mwamba🏃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…