Ushauri: Nichukue gari ipi kati ya hizi?

Mkuu, hizi gari porini huko usiombe yakukute. Ni nzuri sana ila mazingira yetu hayafai kabisa ukipata hitilafu porini.

Kwa sasa nipo kwenye mchakato wa kuvuta JEEP grand cherokee 4.7cc V8 ila sitaingia nalo porini.

Hizo chuma zinauzwa Pesa mbuzi sana hasa ukilikuta la petrol hata ushuru wake TRA upo kawaida ila ndio uwe na kisima cha mafuta nyumbani...

Ni chuma zina nguvu sana....

Kama mafuta siyo tatizo.... go for it... Utaenjoy....
 
JEEP bei yake rafiki kidogo.


Ukiiacha hata mwezi ukija kuwasha haliwaki....

Hapo ujiandae na mipunga mirefu kuita mtu wa kuprogram immo ili liweze kuwaka...

Jeep nyingi zinawapasua watu kwa case hiyo ya immobilizer na case ya limp mode kwenye gearbox...

Ndio maana wanaziuza pesa mbuzi...

Ila ni bonge moja la gari....

Siku nikiwa na kisima cha mafuta nitalinunua tu.
 
Escudo Grand watumie Be Forward no stress. Unalipia kwenye account Yao ya CRDB
 
Escudo Grand watumie Be Forward no stress. Unalipia kwenye account Yao ya CRDB
Bado sijanunua, baada ya kukaa muda nikagundua hizo zote nilizozisema hamna hata moja ambayo ambayo ingefit matakwa yangu
Saivi nipo nafukuzia Pajero
Nimedunduiza hadi saiv nina cash 33M nataka nipambane niangize SUV ya ukweli Fortuner au Pajero
 
Nilikuja kubadili mawazo na sikuchukua hata moja hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…