USHAURI: Niende kwenye ajira Serikalini au nisimimamie biashara za nyumbani?

USHAURI: Niende kwenye ajira Serikalini au nisimimamie biashara za nyumbani?

Waambiwe wawe wanakupa hyo amount ka ya serikalini ili pia utumie usomi kukuza biashara hyo maana hyo biashara inalipa for future use. Watu hukimbilia serikalini vile wazazi wao hawakuachia kitu.
Yaaa tuliotokea background ya kajamba nani ndo tunapigwa mabao huku serikalini na unakuwa huna option zaidi ya kunywa mtori ukitegemea kukuta nyama chini.
 
Nenda kazini katafute chako .No Partineship&Familly business in Africa.
 
Habari za asubuhi?

Nishaurini katika hili nimepata ajira Serikalini Upande wa afya clinical officer soon tunatakiwa kuripoti kazini .

Upande wa pili wazazi wanamiliki pharmacy 2 na maduka mawili ya jumla ya dawa na dispensary moja , wazazi hawataki niende kwenye ajira ya Serikalini wanataka nisimimamie biashara zao lakini ndugu wamenishauri niende kwenye ajira serikalini kwa sababu serikalini kuna security.

Nisaidieni ushauri mdogo wenu ktk hili .

Ktk familia tupo watoto 2 tu , mdogo wangu bado anasoma.umri nina miaka 24
Ushauri toka kwa mfanya kazi.. Kutambua hizo biashara ziyo za kwako, ni za "kwenu", nakushauri

Kama una intent ya kuprosper kwenye fani, kujiendeleza kielimu na kuipata ile pride ya fani yako, basi nenda kaajiriwe.. Ila kama unataka kuganga maisha kuitafuta sumuni, waambie wazazi
1. Wakulipe mshahara kila mwezi
2. Ubaki usimamie biashara..

Unless kama unatazama migogoro huko baadaye.. of which hata sirikalini ipo sana tu!
Kukimbilia "security" sirikalini ni uoga.

Over!
 
Yaaa tuliotokea background ya kajamba nani ndo tunapigwa mabao huku serikalini na unakuwa huna option zaidi ya kunywa mtori ukitegemea kukuta nyama chini.
Uko sahihi waliotoka from poor background za watoto wa wakulima serikalini ni mkombozi ila ukikuta wazazi walikuwa njema basi unajiajiri na kujifunza technique heri upate stress ya biashara zako kuliko stress' na makero ya makazini, kujiajiri huwa Raha sana na kupiga hatua huwa rahisi SEMA jamii hufundisha uoga.
 
Nenda kazini!! Full stop
Biashara ni ya familia hakuna biashara yako hapo, labda kama ungekuwa wewe binafsi unamiliki duka mojawapo na limesimama haswaa!! Lakin kama ni biashara ya wazazi hata kama wana maduka kumi, nenda fanya kazi kwaajili yako na wazazi pia.
 
Waeleze wazazi wakulipe kama unavyotarajia kwenda kulipwa huko serikalini. Jambo jingine hebu jiulize ulisoma ulichosoma ili iweje? Kama unaangalia security ya kazi basi utakuwa ni muoga wa maisha . Miaka mitano iliyopita kazi serikalini zilionekana hazina any security. Kama bussiness ya home unaielewa Baki simamia.

Simamia hizo biashara ukiwa kazini.. njoo tukusaidie usogee karibu na biashara hizo..

Nakushauri kama ifuatavyo:
Kwanza naamini umepangiwa kituo cha mbali na familia yako inayokutegemea katika usimamizi wa biashara za familia, kama jibu ni kweli nakuomba uende kuripoti katika kituo chako ulichopangwa, fanya kazi upate cheque number na mshahara uanze kuingia, baada ya hapo tafuta konekisheni ya uhamisho ili uhamie karibu na sehemu zilipo biashara zenu, utafanya kazi serikalini na jioni/weekend ,usiku utakuwa katika kusimamia biashara za familia. Madaktari wengi wamefanya hivyo na wamefanikiwa. Hakikisha unatumia muda vizuri wa kazi za serikali na usikubali kuongeza muda wa ziada hata kama kuna extra duty packages ili upate muda mzuri kusimamia biashara.Pia utapata fursa ya wateja ambao watakufuata mpaka kwenye biashara zenu
Hizi ni baadhi ya ushauri unaotakiwa kufanyia kazi.

1. Kama utabaki nyumbani, ni vizuri ukawa unalipwa wewe kama wewe sio kufanya kazi bure. Sasa jinsi ya kumwambia wazee, hayo ni juu yako.

2. Kama ukienda serikalini, basi fanya kazi kidogo na uombe kuhamia maeneno ya nyumbani ili usaidie vizuri wazee. Lakini kuwa na uhakika utazushiwa kwamba unaiba dawa. Kwa maana hiyo jitenge na stoo ya kazini na usiiguse ili isiwepo lawama.

3. Kama bado wewe ni kijana mdogo na maeneo ya hapo pana chuo cha pharmacy. Basi chukua degree ya pharmacy huku unasaidia wazee. Hii itasaidia sana kurun pharmacy ukimaliza masomo.
 
Ndugu walinishauri niombe ajira
Kachukue ajira anzisha biashara zako. Kuwa wawili kwa wazazi kusikufanye uwe na kiburi cha pesa. Ukiajiriwa ukaanzisha biashara yako utaweza kutumia ajira kuendesha (ku boost biashara zako).

Usione watu wana hela zao halafu wanagombania ubunge wa miaka mitano tu.
 
Nijibu haya maswali mkuu harafu ndo nikushauli,katika tumbo lenu mko wangapi,wewe ni mtoto wa ngapi kuzaliwa,je Kama una ndugu wengine wa baba na mama mmoja wako wapi na wanafanya nini(wameajiliwa/wamejiajili)?
Tupo wawili tu Mimi ndio mkubwa Nina 24yrs,wa pili ana miaka 16
 
Ni mbaya sana kutokujua unataka nini Kwenye maisha yako.
Sababu utakuwa unaendeshwa na opinions za watu haijalishi ni positive au ni negative.
You'll be a sheep.

Ni vizuri ujue kujisimamia na kufanya maamuzi binafsi.

Hiyo itasaidia hata baadae usianze kulaumu wengine au kuwa na uadui kwamba wewe ndio uliniambia.
 
Uliomba Ajira kuwabeep Tamisemi, Haya Sasa wammeshakupigia na network ipo full,

Ila vitu vingine jaribuni kuwa serious basii, watu wanalalamika wamekosa halafu wewe unakuja kuomba USHAURI WA KIBOYA HAPA, then biashara zenyewe sio zako

Umeniboa KWA kweli
 
Habari za asubuhi?

Nishaurini katika hili nimepata ajira Serikalini Upande wa afya clinical officer soon tunatakiwa kuripoti kazini .

Upande wa pili wazazi wanamiliki pharmacy 2 na maduka mawili ya jumla ya dawa na dispensary moja , wazazi hawataki niende kwenye ajira ya Serikalini wanataka nisimimamie biashara zao lakini ndugu wamenishauri niende kwenye ajira serikalini kwa sababu serikalini kuna security.

Nisaidieni ushauri mdogo wenu ktk hili .

Ktk familia tupo watoto 2 tu , mdogo wangu bado anasoma.umri nina miaka 24
wabongo kwa kiki
 
Wazazi wako wapo sahihi.Simamia biashara ya familia ikue zaidi na itengeneze ajira kwa wengine na hata kurithisha vizazi vyenu vitakavyokuja. Isiishie tu kwenye hizo pharmacy 2 na maduka 2. Kuna future nzuri zaidi kwenye biashara tena ambayo imeshaanzishwa na ipo "operational " kuliko kukimbilia kwenye hio ajira ya serikalini. Wazazi wako wameliona hilo.Lakini mwisho wa siku inategemea na utashi wako kwenye maisha. Kama utashi wako upo kwenye kuajiriwa, basi usikilize moyo wako
 
Back
Top Bottom