Wakuu habari, niliomba kazi taasisi flani ya umma (utumishi) sikupata nafasi jina langu likahifadhiwa kwenye database juzi kati kuna mkeka wa kuitwa kazini umetoka na jina langu likiwemo kwenye kazi za halmashauri. Ila kwa sasa kuna taasisi binafsi nafanya kazi ambayo nalipwa vizuri sana nimefuatilia mshahara wa hapa ni zaidi ya mara mbili ya mshahara huo wa serikalini na haki nyengine zote za mwajiriwa napata kama bima n.k ila changamoto ya hapa private mkataba wao ni wa miaka 3 ila unarenew kila mkataba unapoisha hawana shida.
Serikalini nimepangiwa Tabora na mimi makazi yangu miaka yote ni Dar sasa nikienda huko naenda kuanza moja.
Nilifikiria kutoenda huko ila kuna mtu kaniambia nisipoenda utumishi jina langu litakuwa blacklisted na sitopata tena nafasi nyengine ya kuingia serikalini maisha yangu yote.
Kuna ukweli wowote juu ya hili au nifanye nini wakuu I'm so confused nakosa usingizi kabisa.