Ushauri: Nifanye nini niweze kuthibiti pesa?

Ushauri: Nifanye nini niweze kuthibiti pesa?

Kutumia natumia kunizoea naona ndo imegoma [emoji23][emoji23]
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Itakua huibembelezi pesa, na unavyoitafuta unatakiwa uifanye kama mtoto unaibembeleza na unapoitumia unaiambia sasa tunakula bata
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Itakua huibembelezi pesa, na unavyoitafuta unatakiwa uifanye kama mtoto unaibembeleza na unapoitumia unaiambia sasa tunakula bata
Kuna kuibembeleza tena! mweeh kweli utajir ni shughuli kuufikia [emoji2]
 
Kuna nyakati huwa hazikosekani zitakuja tu, Utapungukiwa hata buku utaliona kubwa!!!
Nyakati zile ndo zinafundishaga wengi, keep waiting the right time its on the way, Utajifunza tu[emoji3][emoji3][emoji3]
Au manasemaje wadau??
Au basi.
 
Hiyo ni chumaulete inaweza ikawa, maana kutumia pesa pasipo kujua imetumikaje kupotea pasipo taarifa hiyo ni chumaulete na sio matumizi mabaya
Wala huyo dada si suala la chuma ulete. Ni kwamba atakuwa ana kipato cha uchumi wa kati na ameamua kuishi maisha ya uchumi wa kati pia ( middle class lifestyle).

Unakuta kipato chake kwa mwezi inaweza kuwa kati ya 1.5M -2.5M. Hapo yeye haoni shida kuishi nyumba ya kupanga kuanzia 300-500K. Na hapati shida ya kutumia angalau 100K kwa ajili ya saloon kwa mwezi. Kwa mwezi angalau hakosi kupita KFC mara mbili au tatu hivi. Shopping za Mliman City anafanya angalau mara 1 au 2 kwa mwezi.

Kwahiyo unakuta mwisho wa siku:Total income = Expenditures, au pengine expenditures zimezidi kidogo. Savings inakuwa 0. Hii ndio lifestyle ya watu wengi wanaoishi maisha ya uchumi wa kati.

Ambapo wenye kanuni zao za savings wanasema ukiwa na kipato cha kati basi uishi maisha ya chini ndio utafanikiwa baadae kutokana na savings. Na ukiwa na kipato cha juu angalau uishi maisha ya uchumi wa kati ili ubakize savings. Sasa wengi wetu kufuata hizi kanuni za kwenye maandishi ni ngumu sana maana mtu anachagua kuishi maisha mazuri leo. Siyo umwambie habari za eti jishushe ili uishi kwa kujibana ufanye savings ikusaidie hapo baadae.
 
Back
Top Bottom