Habari wana JF
Naomba Ushauri, Mimi ni Muhanga wa Kutokukaa na Pesa,ama nikipata pesa zinaisha bila kufanya kitu cha maana au kitu cha kuonekana.
Nimejitahidi saana Kuweka bajeti ya Mwezi nakuifata lakini nashindwa, najitahidi kuweka kumbukumbu ya matumizi yote ya siku ila nafanya kwa siku 2 siku ya 3 nasahu.
Kwa Mwezi kwenye mihangaiko yangu naweza pata faida mpaka ya 1,300,000 kwa mujibu wa daftari langu ka mauzo, Lakini mwisho wa mwezi ukiniuliza hiyo pesa iko wapi naweza nisiwe nayo, ama inakua imebaki kodogo saaana.
Naomba Ushauri, Nifanye nini ili pesa ninazopata kwenye mihangaiko yangu mwisho wa mwezi niione Yote mezani. Natanguliza Shukrani.
1. TAFUTA PESA. Hatua hii kila MTU huipitia. Wengi tunapata PESA kunawakati HATA vichaa na ombaomba pia hupata PESA.
2. TUNZA PESA. Hicho KIDOGO unachokipata jitahidi kukitunza. Kama unashindwa kutunza cash,TUNZA credit au UNAWEZA kukiwekeza kwa KUNUNUA vitu vyenye thamani sawa na hicho KITU. SIKU ukiihitaji hiyo PESA yako utakiuza na KUFANYA Mambo makubwa ZAIDI. Hatua hii huwa NI ngumu KIDOGO coz kunavitu vingi VIZURI na kutamanisha ambavyo UNAWEZA KUNUNUA lakini tatizo lake ni KWAMBA havina UWEZO wa kukurudishia PESA yako. Mf. Mapenzi,ulevi,mavazi,vyakula au WAKATI mwingine changamoto za kifamilia Kama vile magonjwa,sherehe, kuogopa lawama toka kwa ndugu na jamaa nk.
KATIKA hatua hii wengi tunaishia hapa. HATA wake vichaa na ombaomba Wanaishia hapa,madokta na maprof wanaishia hapa. MISHAHARA ya watumishi huishia hapa.
Pia KATIKA hatua hii kunakuilinda PESA kiroho. Ushirikina upo. Watu wakikushindwa kuchukua kimazingara utatengenezewa tatizo ili hiyo PESA ikasovu Hilo tatizo Kisha waipate wao. Soma Kama kwa yeah haupo, kwa kalumanzila haupo kaka yangu sahau kumiliki PESA. Kunakiwango cha PESA UKIWA nacho lazima kunaroho zinaanza kukufuata ili uzitoe.
MFANO. SIKU UKIPATA PESA utashangaa kuona wadeni wako wanakufuata kwa nguvu sana, mchepuko nayo utakuja,mama naye Kyle kijijini utaiona simu take siku hiyo . Jiulize ni Nani kawapa taarifa kuwa leo umepata pesa???
Ukifanikiwa hatua hii MAJINA utakayopewa NI bahili,mchawi,mangi,mkinga,mwanga,Freemason nk. Kama Wewe unapesa na hujapewa MAJINA haya Basi WEWE hutafuti kwa jasho LABDA NI mwizi
3.KUZA PESA.Ili uwe na pesa, kile KIDOGO unachokipata jitahidi kukikuza kwa KUFANYIA biashara FULANI.
KATIKA ulimwengu wa pesa, biashara inakazi kubwa 2 ambazo NI kutunza na kukuza pesa.