Ushauri: Nifanye nini niweze kuthibiti pesa?

Ushauri: Nifanye nini niweze kuthibiti pesa?

Kama unapata hela kidogo kidogo tafuta watu waaminifu mnakuwa mnachangiana wanawake wanaita mchezo au kuna vyama vya umoja mfano umoja wa wagogo waishio tabata (hii wanaifanya sana wahaya)

Tafuta chama chenye katiba na watu wanaojielewa unakuwa unachanga pesa mwaka mzima mkigawana hukosi pesa ya kufanya kitu cha maana.
 
Acha vilevi vyovyote, acha umalaya tulia na mpenzi mmoja, acha maisha ya acting ishi kiuhalisia bila kumwangalia mwenzako anaishije, punguza matumizi yasiyo la lazima kwenye mavazi, usafiri ama chakula - kula chakula cha kawaida tu ili usikonde kiafya, jitahidi kuhudhuria ibada na kuomba msamaha wa makosa yako.

Hii ndiyo dawa, fanya hivi kwa miezi 6 mafanikio utayaona - utanunua kiwanja na Msingi wa nyumba yako utauona.
 
Umelogwa wewe, kama hujalogwa basi akili ya kutunza pesa huna.

Kuweka akiba ni maamuzi binafsi wala sio ya kushurutishwa au kulazimishwa na ni kipaji tu hicho sometimes, labda ulizaliwa ili uajiliwe tu na sio kujiajili.
 
Mimi ndiyo nadondosha sijui ila nimeshafanyia tafiti nikiwa nina hela kuanzia laki ni lazima nidondeshe 30000 au 20000 au hata 10000 yani kuna some missing money gone without noticing mpaka nikae sana nijuulize nilikua na pesa hii mbona sioniii hivyo yani
Hiyo Chuma ulete Mkuu.
 
Kama una account moja, fungua nyingine unatumia kufanya savings tu, hutembei nayo na nyingine unaacha fedha ya matumizi kidogo. Na hapo unaishi kulingana salio lililopo account ya matumizi na unatembea na card ya account ya matumizi tu.
 
Pesa unaipenda ila yenyewe haikupendi. Tafuta mazingira ikupende. Uwe msafi( acha mademu), usikope kwa wagalaliaji wenye riba kubwa, utoe kwa wahitaji ni sadaka.
Mhitaji ni yule mhitaji hasa sio lazima uwe kanisan/ msikitini,

Acha pombe na usitoe ofa ya pombe utabarikiwa.
 
Habari wana JF

Naomba Ushauri, Mimi ni Muhanga wa Kutokukaa na Pesa,ama nikipata pesa zinaisha bila kufanya kitu cha maana au kitu cha kuonekana.

Nimejitahidi saana Kuweka bajeti ya Mwezi nakuifata lakini nashindwa, najitahidi kuweka kumbukumbu ya matumizi yote ya siku ila nafanya kwa siku 2 siku ya 3 nasahu.

Kwa Mwezi kwenye mihangaiko yangu naweza pata faida mpaka ya 1,300,000 kwa mujibu wa daftari langu ka mauzo, Lakini mwisho wa mwezi ukiniuliza hiyo pesa iko wapi naweza nisiwe nayo, ama inakua imebaki kodogo saaana.

Naomba Ushauri, Nifanye nini ili pesa ninazopata kwenye mihangaiko yangu mwisho wa mwezi niione Yote mezani. Natanguliza Shukrani.

1. TAFUTA PESA. Hatua hii kila MTU huipitia. Wengi tunapata PESA kunawakati HATA vichaa na ombaomba pia hupata PESA.

2. TUNZA PESA. Hicho KIDOGO unachokipata jitahidi kukitunza. Kama unashindwa kutunza cash,TUNZA credit au UNAWEZA kukiwekeza kwa KUNUNUA vitu vyenye thamani sawa na hicho KITU. SIKU ukiihitaji hiyo PESA yako utakiuza na KUFANYA Mambo makubwa ZAIDI. Hatua hii huwa NI ngumu KIDOGO coz kunavitu vingi VIZURI na kutamanisha ambavyo UNAWEZA KUNUNUA lakini tatizo lake ni KWAMBA havina UWEZO wa kukurudishia PESA yako. Mf. Mapenzi,ulevi,mavazi,vyakula au WAKATI mwingine changamoto za kifamilia Kama vile magonjwa,sherehe, kuogopa lawama toka kwa ndugu na jamaa nk.
KATIKA hatua hii wengi tunaishia hapa. HATA wake vichaa na ombaomba Wanaishia hapa,madokta na maprof wanaishia hapa. MISHAHARA ya watumishi huishia hapa.

Pia KATIKA hatua hii kunakuilinda PESA kiroho. Ushirikina upo. Watu wakikushindwa kuchukua kimazingara utatengenezewa tatizo ili hiyo PESA ikasovu Hilo tatizo Kisha waipate wao. Soma Kama kwa yeah haupo, kwa kalumanzila haupo kaka yangu sahau kumiliki PESA. Kunakiwango cha PESA UKIWA nacho lazima kunaroho zinaanza kukufuata ili uzitoe.
MFANO. SIKU UKIPATA PESA utashangaa kuona wadeni wako wanakufuata kwa nguvu sana, mchepuko nayo utakuja,mama naye Kyle kijijini utaiona simu take siku hiyo . Jiulize ni Nani kawapa taarifa kuwa leo umepata pesa???
Ukifanikiwa hatua hii MAJINA utakayopewa NI bahili,mchawi,mangi,mkinga,mwanga,Freemason nk. Kama Wewe unapesa na hujapewa MAJINA haya Basi WEWE hutafuti kwa jasho LABDA NI mwizi

3.KUZA PESA.Ili uwe na pesa, kile KIDOGO unachokipata jitahidi kukikuza kwa KUFANYIA biashara FULANI.
KATIKA ulimwengu wa pesa, biashara inakazi kubwa 2 ambazo NI kutunza na kukuza pesa.
 
mi ni mfujaji asee yani nikiwa na elf 50 ni kama nna buku ndani ya dakika sijui hata inaishaje
Hiyo ni chumaulete inaweza ikawa, maana kutumia pesa pasipo kujua imetumikaje kupotea pasipo taarifa hiyo ni chumaulete na sio matumizi mabaya
 
Back
Top Bottom