Ushauri: Niishi vipi na ndugu wa namna hii?

Hachukulii suala la kujuliana hali kwa uzito kama ulivyo, kuna watu wanapenda kuwajulia wenzie hali na kuna ambao hawapo hivyo.
 
Mkuu kwanini uhangaike nae wakati kila mtu anapambania maisha yake kwanini usiachane nae na wewe ukafanya mambo yako. Unataka muwasiliane kila mara ili iweje?
Mimi nina ndugu yangu hapa mjini tunakumbukana kwenye kupeana taarifa za misiba tu zikitokea huko kijijini, tunaenda wote tukirudi kila mmoja busy na mambo yake.
 
ACHA KUKUZA MAMBO. HUYO JAMAA HANA NOMA NI KUWA TU ANAPAMBANA NA MAISHA YAKE.

PIA INAWEZEKANA KUNA KITU AMEGUNDUA KUTOKA KWAKO SASA ANAJARIBU KUKUKWEPA. INAWEZEKANA WEWE NI MBEA MBEA, MCHONGANISHI PIA UNAPENDA KUFATILIA MAISHA YA WATU NA KUYAANIKA HIVYO AMEAMUA KUKUKWEPA.
BANDIKO LAKO TU JF LINAONYESHA WEWE NI MTU WA AINA GANI. HIVI UNATAKA KUMBLOCK KWA KOSA GANI? WEWE UNAKUZA MAMBO TENA INAONEKANA NI MSHARI/MGOMVI!.
 
Hebu rudia kusoma vizuri maandiko yangu.
 
Mambo mengine ni kukocmplicate tu.
Wewe na hiyo nduguyo hamna bond ya pamoja..

Usichokijua ni kuwa ili muwe na mawasiliano ya mara kwa mara basi mngejenga bond kuwa ndugu tu haitishi ..muwe marafiki hapo ndio kunaweza kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara ila kama mwenzio habari hana basi pigianeni simu hivyohivyo kimachale machale .
 
Sasa Kama umemzidi kipato?
 
Binafsi huichukulia simu kama kiungo cha mawasiliano na kupeana Taarifa tu. Haya mambo ya kupigiana simu kila siku eti tunasalimiana tu siyo muumini..

Ninahisi Ndugu yako naye ana Character hizi zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…