Ushauri: Niishi vipi na ndugu wa namna hii?

Hebu anza kumpigia halafu umshirikishe michongo ya kutafuta hela mana umesema unamzidi kiuchumi.

Unajua kuna kipindi inaleta uvivu, yaani mtu anakuzidi kiuchumi halaf anakupia mara kwa mara kukusalimia tu bila kuongelea mpango wa kukuinua kichumi na wewe! Unakuwa unahisi anakuchora tu. Mara akuulize unaendeleaje wakati anajua kabisa unaishi kwa kuunga unga!

Hebu mpe michongo ya hela huyo ndugu yako uone atakavyokuwa mchangamfu ukimpigia.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Utakuwa unamuudhi sana ndugu yako. Hata ukim-block, utampa nafuu wakati ndani wewe unaumia. Mimi pia sipendi mawasiliano yasiyokuwa na maana. Mara vipi? Mnaendeleaje huko? Watoto wanendeleaje na shule... Kama una issue (harusi, ugonjwa, kazi...) nitakusikiliza lakini siyo salamu bila issue yoyote. Huo ni usumbufu.
 
Acha kumaindi vitu visivyo na msingi kwenye maisha. Just get busy with your family, mambo ya kumpigia kila saa kwani yeye mtoto mdogo? I believe mkiwa na ishu ya msingi atakucheki tu.

By the way, give him sometime to miss you pia, don't be too available huyo ni nduguyo tu damu ni nzito kuliko maji.

As you said, kila mtu ana family yake, yawezekana anajaribu kuuweka undugu wenu msije kugombana maana Hawa wake tunaooa huwa sumu pia.
 
Halafu wewe sio brazangu kweli maana Nina ndugu yangu yeye hata saa 12 asubuhi huwa akijisikia anapiga tu simu kusalimia au saa sita usiku.
 
Another thing: Hamna kitu nachukia nowadays kama kuongea na simu muda mrefu bila hoja za msingi.

1 minute or 2 is very enough.

Salamu, taarifa na mambo mengine kama huwezi kupiga simu na kufanya short & brief, please send me text or WhatsApp. Basi!

Nisije nikakukatia simu, ukaniona sio.
 
Well said, I salute!!
 
Karne hii unawezaje kumpigia mtu simu ili hali iyo simu ni ya kusalimia tu kuwa bize na mishe zako wewe binafsi sina mda wa kuwapigia ndugu eti tunapiga stori mara chache sana fanya mambo yako kijana
 
Inakuumiza; unaonekana unapenda watu, endelea kumpenda na kuwapenda wengine pia. Jukumu la kumpenda mtu mwingine ni wajibu wako wewe na ndiyo agizo la Mungu kwako. Jukumu la wewe kupendwa na mtu mwingine siyo lako, na hutakiwi kuhangaika na mtu mwingine just in case anaonekana kutokukupenda wewe, hilo siyo la kwako, ni la kwake yeye anayetakiwa kukupenda wewe.

Kwa mfano, wajibu wako wewe kwa mtu tuseme mke wako, ni wewe kumpenda yeye. Swala la yeye kukupenda au kutokukupenda wewe siyo la kwako, ni la kwake yeye, na ikitokea kama pengine akaonekana kuwa hakupendi, hilo lisikupe shida. Shida kwako iwe ni kumuonea hurumia yeye kwa tabia ya kukiuka agizo la Mungu ambaye ndiye amemwamuru awapende wengine ukiwemo wewe mume wake
 
Mtu wa Mungu uinuliwe na Mungu
 
Pole sana , wewe ni miongoni mwa watu wanaothamini udugu hii kulingana na maelezo yako ila kwasasa dunia imebadirika ndugu hupenda zaidi ukimpigia basi mnaongelea dili za pesa au mambo ya kimaendeleo ila salamu ni kama michosho.

Fanya hivi endelea na familia yako , wapigie ndugu angalau kila baada ya miezi minne mpaka mitano hapo umuhimu wako utaonekana ila mwenye shida akupigie.

Ndugu ni adui kwa dunia ya leo [emoji24][emoji24][emoji24]


Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Asante kwa ushauri nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…