Ushauri: Nimebaki na Tsh. 10,000/- tu baada ya kupokea mshahara, nifanyaje?

Acha pombe
 
Jitathimini.
Umeandika neno moja tu, ila ukilirudia mara mbilimbili liko deep vibaya mno. Ifungue hiyo code mzee!!!
umeaga nyumbani ?ONGEA NA WAZEE WAKO VIZURI
huwenda unashida mahali haingii akilini hili uliloliandika.hapo umeshajingiza kwenye lindi la ufukara
Inaweza kuwa kweli mpaka kuna time nasema lazima kuna tatizo mahali, sababu hii si mara ya kwanza kutokea hii...unakuta unapanga kabisa kuwa nikipata ya mwisho wa mwezi huu sitaki umchezo ila ikija tu nikiishika nikama kuna kitu kinaniingia kinachofanya niwe nje ya akili yangu kabisa..
Hapo naanza sasa kuhama hama sehemu tofauti tofauti za viwanja,..... Na akili inakuja kurudi wakati tayari nimeshabaki na kiasi kidogo kama hivi ndo akili inaanza kukaa sawa sasa kwamba "What Is This...?"
 
unaumri gani?
 
Tafuta mume wa kukulea mwezi mzima hadi utakapopata mshahara mwingine.
 
Kaburudike na wimbo wa JOGOO LIMEWIKA DODOMA!
 
Kama ulivyotikisa gesi ujasema "Ila imekaa muda" basi bahati yako.
 
KATAA KAZI. KAZI NI UTAPELI
 
Kuwa Bosi wa maisha yako,inaonekana unapelekwa hovyo hovyo hujielewi.
 
Ne
Nenda simambwe/galijembe nunua kabichi za buku nne kwanza ukate wenge kisha hakikisha unao unga ndani...mengine yanazungumzika
 
Duuh! pole,wewe unateswa na ulevi,mimi nateswa na betting... naliwa kishenzi,hapa nimeliwa hela yooteee...! daaah! namlaumu sana aliyenifundisha kubeti.
Bila kubeti ningekua na tuhelahela.
 
Mtoa mada ndio wale mnaoletewa bill kama umenunua kiwanja kudadeki
 
Hahahaaa...!!
Mkuu umenikumbusha mbali sana kama miaka 11 iliyopita.
Kipindi hicho nikiwa muajiriwa, nilikuwa mzee wa tungi na bata kwa sana washkaji kama wote. Mshahara nilikuwa naukausha na kuupiga mswaki chap. Kilichokuwa kinaniokoa pale kazini tulikuwa na mfuko wetu wa kuinuana! So nazama chap na cheque mkononi kwa treasurer ili wanidebt mwisho wa mwezi. Uzuri ilikuwa hata ukope 300k riba ilikuwa sh10k tu!
Sasa hii ntakayokopa nakuwa nanidhamu nayo inanisogeza lau katikati ya mwezi. Ikiisha namfata mwanangu mmoja yy alikuwa sio mtu wa masanga na hana baya so ananikatia kama 50k namalizia mpaka siku ya mshahara.

Kwahiyo mkuu usiwaze sana kula ujana na itafikia mahala utaacha tu na mambo kuji tune yenyewe.

Cha kukushauri punguza kampan ya marafiki wa pombe. Kama mtu hana kipato ila anapenda sana monde pasipo kugharamikia, mwepuke chawa huyo. Kula monde kivyako marafiki wawe ni wale unaokutana nao hukohuko batani hawa kiasi flan wanajielewa. Halafu kula monde mbali na mtaa unaoishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…