Ushauri: Nimefanyiwa sperm analysis ikagundulika siwezi kumpa m/mke ujauzito

Ushauri: Nimefanyiwa sperm analysis ikagundulika siwezi kumpa m/mke ujauzito

mwingne ana pesa hana watto, mwingine ana watto hana chakuwalisha na ndio maana anaitwa Mungu tuendelee kumtukuza kweke kuna njia!
 
Wakubwa najua humu ndani wapo matabibu wanaweza kunisaidia leo nilifanyiwa sperm analysis nikapata majibu yafuatayo.

Sperm mophology imeonekana baadhi ya shahawa kwa kiwango kukubwa zimeonekana zina umbo ambalo si sahihi hazina mkia wala kichwa.

Spem viscocity haipo sawa hazivutiki, sperm color ni yellow dk kanambia kwa matokeo hayo ni ngumu kumpa mwanamke mimba .

Kanambia nirudu kesho ula kabla sijarudi.

Naomba JF doctor mniambie je, naweza kurudisha sperm quality yangu namimi nipate family au ndo siwezi tena.

Msaads tafaadhali.
1465567671425.jpg
 
Jaribu unga wa mdalasini na asali ni maarufu sana kurekebisha ishu ya sperma Bro, lengo tujue kwanza ni lifestyle yako ndo tatizo au ni disable ndo tatizo
 
Mkuu, mimi nafikiri Daktari kwa uzoefu wake anaweza kujua ni kitu gani kinasababisha mophology ya sperms zako zionekane ndio sivyo, kwa nchi za wenzetu walioendelea wangeweza kuchagua sperms ambazo zinaonekana mophology zako ziko sahihi/balabala i.e zenye kichwa na mkia wakazi changanya na yai la mkeo kwenye test tube ili fertilization ifanyike kwenye test tube katika mazingira sahihi, wakisha hakikisha kwamba hilo limefanyika bila matatizo litakalo fuata ni kuhamishia kiumbe kwenye tumbo la uzazi la mkeo.

Usije ukadanganyika kwamba lishe ya aina fulani inaweza kurekebisha mambo, hilo mimi siamini - tatizo lipo kwenze korodani zako hazitengenezi vizuri sperms zako, labda unaweka laptop kwenye mapaja yako kwa muda mrefu (utani-lakini kuna kaukweli ndani yake).

Hilo likishindikana nenda Nigeria kamuone Nabii Joshua akuombee kwa Mungu, mimi ni mtu hasiye amani vitu kirahisi rahisi lakini jamaa huyu namkubali sana, ana wito husio wa kawaida, hata wanawake walio ondolewa fallopian tubes zao zote ana uwezo wa kuwaombea wakaweza kupata mimba tena! Ni ajabu na kweli.
Kweli kwa Mungu yote yawezekana ushauri wako mzuri sana.Aende kwa aliye muumba akaombe tu.Jana tu yenyewe kuna mtu kapata muujiza wa ajabu mpk mwenyewe nikahisi shida zangu zote kwisha kha!!!!!Huyu Mungu kweli anaishi.
 
Kuja huku umekurupuka matokeo yake unadhihakiwa tu hadi na watoto wa shule! Subiri urudi kwa daktari wako atakupa matibabu na ushauri husika wacha kupanick
Sio madaktari wote wanaoweza kukupa suluhu ya tatizo lako,hayajakukuta ya madaktari wa kitanzania. Kuna daktari alishawahi kuniambia nina mayai viza nisahau habari ya kuzaa. Lakini nilikutana na marafiki walionipa ushauri wa kula healthy na mazoezi. Baada ya miezi saba nilipata mimba na nikazaa. Mi namshauri huyo kaka abadilishe kabisa mfumo wake wa chakula. Acha sukari,pombe,kama unatumia sigara acha na ule sana mboga za majani na protein. Pia fanya mazoezi na kunywa sana maji. Kwa maelezo zaidi njoo inbobo
 
Kweli kwa Mungu yote yawezekana ushauri wako mzuri sana.Aende kwa aliye muumba akaombe tu.Jana tu yenyewe kuna mtu kapata muujiza wa ajabu mpk mwenyewe nikahisi shida zangu zote kwisha kha!!!!!Huyu Mungu kweli anaishi.

Hakuna mtu alikuwa mbishi kama mimi linapokuja suala la miujiza - wanasayansi wakati mwingine tunajisahau sana kwa kudhani tuna uwezo mkubwa wa kubuni/vumbua mitambo,madawa,silaha nk vikafanya kazi kama kawa - sasa jeuri hii wakati mwingine inaweza kuwafanya wafikiri uwezo wao unakaribiana na wa Kimungu Mungu hivi - lakini likitokea natural disaster kama: Tsumani, Tetemeko la aridhi, Vimbunga kama Tornado na Typhoon, Volcano eruption kama iliyo tokea Pompeii Italy miaka ya zamani sana mji wote na wakazi wake waliteketea, haya tuje magonjwa ambayo hayana tiba, kifo nk - majanga yote tajwa hapo juu hakuna mtu/Serikali za nchi yoyote including Super Power kama Amerika zenye nyezo za kila sampuli lakini hawana uwezo wa kuzuia
majanga kama hayo - hapo ndipo wanasayansi ukumbuka kwamba kumbe kuna Mungu mweye uwezo kuliko wao.

Kwa nini nasema yote haya? Juzi hapa nilishuhudia miujiza ya Kimungu baada ya Pastor mmoja kutoka Merikani kufanikiwa kurefusha mguu wa kulia wa kilema ambao ulikuwa mfupi ukilinganisha nawa kusoto - aliambiwa akae kwenye kiti anyooshe miguu yake kwa mbele, Pastor alipo anza kuomba tuliona mguu wa kulia ukivutika wenyewe ukakoma ulipo lingana na wa kushoto - baada ya muda kidogo jamaa alisimama miguu yake ikiwa inalingana kabisa!!! Hii ni ajabu na kweli, nimekubali uponyaji kwa maombi/miujiza upo.
 

Hii ni habari njema kwa nchi yetu, kwa kweli tatizo la ongezeko la watu ni changamoto kubwa sana inayotukabili, hivyo angalau wewe hautaongeza mzigo kwenye Uchumi wetu mdogo tuna mapungufu ya kila kitu madarasa hayatoshi, madawati hayatoshi, daladala hakuna hata pa kukanyaga, viwanja vinajaa, hivyo mimi kwangu hii ni Habari njema kwa nchi yetu!
Kama vipi jiue tu mkuu, halafu kaue na wazazi wako ili idadi ipungue kwenye ukoo wenu, labda tuanzie hapo
 
Kwa nini unataka upate mtoto/watoto? Hii nchi imeshajaa hiyo ni habari njema kabisa kwanza ikitokea wanaume wengi kama wewe Mungu ashukuliwe, hakuna njia nyingine ya kupunguza watu!
Thank you
 
Pole sana kaka. Mungu aliyeumba Mbingu na Dunia hujawahi kushindwa na Jambo lolote lile. Changamoto unayopitia ni kubwa na Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kukuvusha hapo. Ningependa kukushauri kuwa nunua kingamuzi chenye Emmanuel TV na uwe una angalia namna ambavyo watu wengine wenye matatizo ya aina hiyo wanatoa shuhuda kwa namna ya ajabu kabisa Mungu alivyowaponya na tatizo kama hilo na sasa wana watoto tena wenye afya tele. Imani yako itazidi kuongezeka kila siku.....Nawe Mungu atakuhudumia siku moja sawa sawa na kiwango cha Imani yako. Usife moyo....take courage....Fanyia Kazi na ushauri huu pia. Barikiwa
Thank you ccta ubarkiwe
 
Jaribu unga wa mdalasini na asali ni maarufu sana kurekebisha ishu ya sperma Bro, lengo tujue kwanza ni lifestyle yako ndo tatizo au ni disable ndo tatizo
Thank you
Akili za kipumbavu na ukosefu wa hekima na ustaarabu zero, mbona mnageuza jf kuwa kijiwe cha ******!!? Mtu anatatizo wewe unaleta komenti zisizo na maana kibinadam, huna empathy wala sympathy, ur merely a wild hog!!

 
Back
Top Bottom