Ushauri: Nimeokota wallet yenye Tsh. 50,000 pamoja na risiti za miamala ya pesa nyingi nahofia kurudisha nahisi naweza bambikiwa kesi

Ushauri: Nimeokota wallet yenye Tsh. 50,000 pamoja na risiti za miamala ya pesa nyingi nahofia kurudisha nahisi naweza bambikiwa kesi

Cha kuokota sio cha kuiba mkuu.

Tumia hio Fedha kiasi kwa kuwasaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu inayobaki fanyia mambo yako.

Hapo utakua umejitakasa kwa sababu ukiirudisha unaweza kubambikiziwa kesi nzito kama ukabaji ama kuvunja na kuiba
Natamani kupata namba Yako nikupe Walau vocha kwa ushauri mzuri tatizo hela imeshaisha😂
 
Shida unaweza ukawa mwema kuripoti police ukadakwa wwe kesi ikabakia kwako.
Jamaa yangu juzi kaokota simu ya million moja mwenye simu akampigia kapokea akampa maelekezo alipo mwenye simu alipofika kesho yake kuchukua simu yke hata kusema neno Asante au kumuachia jamaa hata teni kapiga kimya.
Ukishaamua kurudisha basi kubali kua unafanya wema. Jamaa angemwambia tu kua nakuletea simu yako ila andaa kichache sasa hajaongea analalamika nini tena.
 
Ukishaamua kurudisha basi kubali kua unafanya wema. Jamaa angemwambia tu kua nakuletea simu yako ila andaa kichache sasa hajaongea analalamika nini tena.
Kimazoea ili siku ingine awe na moyo mengine yanaua uaminifu
 
Kimazoea ili siku ingine awe na moyo mengine yanaua uaminifu
Hamna hiyo kitu mzee, kama yeye karudisha kwa wema na uaminifu malipo ya nini?? Mwema ni mwema tu kama ni muumini basi hapo hamna baraka aliyopata maana karudisha kwa kinyongo.
 
Nimeokota wallet ina pesa kiasi cha elf 50,000 ila ina risiti ya miamala ya Milioni 45 pamoja na Milioni 10m. Tarehe ni siku niliookota, ndani kuna pia kitambulisho cha bima, nk.

Nahofia kurudisha anaweza kunibambikia kesi ya kupoteza pesa zake!

Nahisi anaweza kusema wallet ilikuwa na pesa hizo.

Naombeni ushauri.
Nini maana ya kuokota! Kuokota ni kujimilikisha kitu ambacho sio chako eti kwasababu umekikuta katika mazingira yanayoonyesha hakina mwenyewe! Lakini ukikuta kitu kina viambatanishi vinavyoonyesha jina, anuani, namba ya simu basi hapo sio kuokota ni wizi. Una njia mbili: moja ni kupita tu na kukiacha kitu hicho (hii ndo njia salama kabisa), njia ya pili ni kukipeleka polisi na kutolea maelezo (hii njia sio salama) sababu hujui mazingira yaliyonyuma ya kukutwa kwa kitu hicho hapo. Kama ulikuwa na njaa ya pesa basi dokoa kiasi sepa!
 
😀😀😀
Ilishawahi kunitokea zamani, tena nipo ofisini mastory ya pesa za majini. Sasa kutoka nje naenda washroom nikaiona bahasha ina elfu 10 nyingi niliingia wenge la kufa mtu. Niliiokota bahasha huku natetemeka.

Siku nyingine nipo Posta soko la kisutu nakatisha barabara nikaiona dola 50 na shilingi 9000 sikuwa na wenge aisee ile hela niliikota 🤣🤣🤣
Una nyota nzuri mkuu.🤣🤣
 
Kuna uhusiano mkubwa wa kuwepo roho nyuma ya kuokota hela! Kuna kipindi nimepigika choka mbaya nilikuwa naokota mara, 10k, 5k, 2k, 1k na jeto, 200, 100, hadi 50. Sasa baada ya kujipata, sijawahi kuokota hata mia mbovu. Hapo ndo nikajua kupigika kwangu kulikuwa na mashetani yamekaa katika mlango wa kuzuia kipato. Yakiona vipi yananiachia hivyo vijisenti! Sasa mbona baada ya kujipata siokoti? Hata hivyo sitaki kuokota! Nataja za jasho langu
 
Mimi nikiona coins huwa siokoti 😀
 
Nimeokota wallet ina pesa kiasi cha elf 50,000 ila ina risiti ya miamala ya Milioni 45 pamoja na Milioni 10m. Tarehe ni siku niliookota, ndani kuna pia kitambulisho cha bima, nk.

Nahofia kurudisha anaweza kunibambikia kesi ya kupoteza pesa zake!

Nahisi anaweza kusema wallet ilikuwa na pesa hizo.

Naombeni ushauri.
Nimeokota wallet ina pesa kiasi cha elf 50,000 ila ina risiti ya miamala ya Milioni 45 pamoja na Milioni 10m. Tarehe ni siku niliookota, ndani kuna pia kitambulisho cha bima, nk.

Nahofia kurudisha anaweza kunibambikia kesi ya kupoteza pesa zake!

Nahisi anaweza kusema wallet ilikuwa na pesa hizo.

Naombeni ushauri.
Kwani unataka kurusha wapi?
 
Nenda polisi Mkuu waambie wampigie simu muhusika aje kuchukua vitu vyake achukulie hapo polisi. Ila polisi usiwaachie wenyewe hiyo wallet na wao ni binadamu kama kweli una nia ya kumrudishia basi wampe muhusika ukiwepo
Kama aliuawa kwa ujambazi then vitu vimetupwa makusudi ili wasihisiwe kwenye tukio, unaujua msemo wa 'anayekutwa na ngozi........ .
 
Hata akiipeleka polisi, hiyo hamsa polisi watatia kwapani kisha mwenyewe ataitwa aje kuchukua maratasi yake.

Muhimu hapo chukua hamsa yako, hiyo wallet mpe bodaboda wale wanaovaa ndala moja inaning'inia(vishandu) mwambie apite kituo cha polisi na ukali kisha aitupie kituoni halafu atembee na ukali.
Hahahahaha,🤣🤣🤣
Nimecheka sana aiseee,
 
Hatokuja bahatika Tena,katu
Yaani elfu 50 ni kubahatika!!!!! Watu mna roho ngumu. Ingekuwa hata hela unayoweza kununua jumba sawa. Hiyo ukipanda daladala masaa mawili imeisha!!!

Siku za nyuma mtu alikosea akatuma laki moja kwenye namba yangu. Nikiangalia,namba ni ngeni. Nikajiuliza nani huyu ananipa hela ya siku kuu, na nilivyopinda hivi. Sikuitoa. Baada ya kama nusu saa, akapiga mdada, anaomba samahani, na kwamba alikuwa anamtumia mama yake mzazi hela ya siku kuu. Akaomba nikate 20k basi nimrudishie 80k. Nikafanya hivo. Badae roho ikakataa. Hii pesa si harari yangu, hujui kaipatapataje, na yenyewe nikamtumia. Hakuamini. Hatufahamiani, ila sometimes salamu salamu.

Kuna vitu vingine ni vidogo siyo vya kukushushia hadhi, na wakati mwingine unaweza kukuta kitu kidogo kama hicho kimekufungulia mlango.
 
Back
Top Bottom