Peleka BOT pale ule interest kwa mwaka uweke ua miaka 15
Nakumbuka ulikuwa ukiweka 500M kwa Mwaka unapata 80 per year kwa miaka 15
So kama unaweka 700 ina maana kwa miaka 15 kila mwaka una almost 100 zinaingia
So unachoweza fanya ni kwamba hiyo 100 unafanya yafuatayo
wewe unafungua biashara ya kwanza k unapambana nayo unachagua biashara let's say unasema unafungua
LODGE kwa wilayani, kwa 100M
Let's say unafungua lodge pale Makambako ndio pilot plan yako vyumba vyako 10 tu unatengeneza kitu kimoja safi then unasema pale kulala ni 50,000
Chumba hakikisha kina
[emoji117]Kitanda kizuri
[emoji117]Meza nzuri na kiti chake
[emoji117]TV angalau ya inch 50 na dstv full [emoji117]package
[emoji117]Sliding window
[emoji117]Tiles
[emoji117]Mlango wa kadi
[emoji117]Bafuni kuwe na Heater ya maji ya moto
Shower
[emoji117]Toilet safi mnoo
[emoji117]Ndala zisiwe za kukatwa ziwe za kwenu zenye logo zenu hata mtu akiondoka nazo mnaweza zingin
[emoji117]Bafuni mgeni anakuta kuna dawa ya mswaki, mswaki, shower gell, na lotion ya kutumia siku hiyo
[emoji117]Fridge kidogo ambapo kunakuwa na bia 2 , soda 2 na maji mawili
Huduma iwe ni Bed and Breakfast na kwamba Breakfast iwe ni bufee l
Wilayani humo watu tunaosafiri tunakosa lodge zenye huduma hizi
Receptionist awe mrembo haswaa
Room service pia
Parking iwepo hata mwenye DFP yake anapaki
Lodge ikiwa kali unakuwa ni talk of the town
Then unaitangaza kwenye Instagram etc
Unatengeneza na mfumo wa booking unajikuta lodge imekuwa booked full year
Wewe unatengeneza Niche yako Target yako ni wakuu wa idara mbalimbali za kiserikali wanaokuja wilayani humo, wafanyabiashara well off ambao hawapeni kulala lodge za kawaida
So ukiweza pilot wilaya moja next year unahamia wilaya nyingine with the same name so unategneenza Chain ya Lodges za jina lako so kwa miaka 15 unaweza tengeneza Lodges 15
However after 3 successful years ya kwanza ukiwa na history nzuri ya transactions let's kwa siku unalaza let's say 300,000 maana yake kwa mwaka lodge moja transactions ni inacheza 90M so unaweza kuandika proposal la mkopo Bank kujenga chains ya Lodges katika halmashauri 200 nchini unayoyainisha so unaweza lamba 20B ya mkopo bank kwa ajili ya expansion
So all in all 700 inaendelea kubaki bank
Bank una 20B za expansion maana hapa tunaongelea utakuwa na Lodges almost 200 nchini kote katika halmashauri
Kikubwa ni Standard ziwe zile zile
Ukishakuwa available kwenye kila halmashauri unachokifanya ni kifuatacho
[emoji117]Unafanya B2B ya Serikali kuu kwamba popote watu wa serikalini wanapokwenda wanalala kwenye lodge zako hapa unatengeneza offices Dar Es Salaam na Dodoma kwa ajili ya kuwa unafuatilia malipo, invoices maana unaweza introduce mfumo wa kulala na kulipa kila mwezi au annually kama ilivyo kwenye kuchukua mafuta
[emoji117] Unaongea na makampuni mengi ya mjini, mashirika na Taasisi binafsi zilizopo Dar kwa ajili ya kuwa unafuatilia malipo, invoices maana unaweza introduce mfumo wa kulala na kulipa kila mwezi au annually na kwenyewe
Marketing via Insta, Redio Stations (hawa wa redio stations ni sababu una sponsor events mbalimbali mfano lodge yako ndio inakuwa main sponsor wa Tigo tumewasha ya wasafi au fiesta ya Clouds so popote wasanii wakiwa wanaenda wilayani wanalala bure kwenye lodge zako
So watapiga piga picha, wata tag, watasifia
Unapata maillage na sifa