ningekuwa ndio Mimi ningefanya hivi.
Asilimia 60% ya fedha nitaziweka sehemu salama, ambapo hazitapotea Hadi naingia kaburini.
Sasa itakuwa hivi 60% ya fedha yote utapata Tsh 464,719,927/=.Sasa hizi fedha nitazifanya kama financial security kwa maisha yangu yote duniani, nitazifanya zisipotee na ziniingizie fedha ya kucover bills za maishaa hata kipindi nikiwa sijiwezi, au nimetoka kupata ulemavu wa kudumu au maradhi ya kunifanya nishindwe kufanya kazi Tena na kulala kitandani, mfano unaweza kupata ajari na kupelekea kuvunjika UTI wa Mgongo so kwa hizi fedha nitakuwa nacover bills za maisha bila kusumbua ndungu na marafiki.sasa nusu ya pesa nitaziweka mfuko wa bond UTTsawa na Tsh 232,359,963/= kwa pesa hii nitakuwa nalipwa 2,000,000 kwa mwezi. Na nusu ya fedha nyingine nitanunua hati fungani ya serikari ya muda mrefu ya miaka 25, ambapo nitapewa return ya 12% kwa mwaka na nitakuwa nalipwa mala mbili kwa mwaka, kwahiyo Kila baada ya miezi SITA nitalipwa Tsh 13,900,000/=.hii ni system itakayokufanya uishi kama mtumishi wa serikari mwenye mshahara wa 2m plus.
Asilimia 15% ya fedha yote sawa na Tsh 116,179,981.utajenga nyumba ya kuishi, kubwa tu kwa hii fedha na uzoefu, tumejenga nyumba ya three in one,watumishi watatu nyumba Moja..kwa Tsh 90,000,000/= Sasa kwa nyumba ya kawaida unajenga na kusaza.
mpaka Sasa hivi kwa asilimia 75% ya fedha zako zitakufanya uishi maisha ya kati kwa siku zako zote za kuishi duniani utasomesha,utaoa,utakula vizuri,utavaa,utapata bima ya afya yaani utaishi life kama la mkurugenzi Sasa naendelea na mchangua kwa asilimia zilizobaki.
Asilimia 10% ya fedha zote sawa na Tsh 77,453,321/= 5% ya fedha utajenga store ya kuhifadhi mpunga na 5% utakuwa unaweka store ya mpunga kwa Kila msimu, ni biashara ambayo ni low risk na profit unapata.
Asilimia 9% ya fedha zote sawa na Tsh 69,707,989/= utanunua shamba nusu ya fedha na nusu nyingine ya fedha utanunua either mbuzi,au ng'ombe wa maziwa katika fedha hiyo utatenga kiasi kidogo Cha kununua chakula Cha mifugo, na store ya kuweka chakula, na pia fensi kwa ajili ya ulinzi.
asilimia 2% sawa na Tsh 15,490,664/= utamfungulia mke wako baishara ya kumkeep busy ila siyo ya purukushani soft business hapa nashauri anaweza kuwa WAKALA wa NMB,CRDB,M PESA,TIGO PESA,AIRTEL MONEY,HALOPESA hii biashara watoto wako watamsaidia mama Yao kufanya hii business.
Asilimia 4% fedha zote sawa na Tsh 30,981,328./= hapa utanunua gari mbili ya kwako na mke wako ya kutembelea unaweza chukuwa vanguard na mke akachukuwa IST au Carina, safari zako zitakuwa zinaenda vizuri pamoja na za mke wako.
Kwa huo mchanganuo hapo juu nawsilishaa boss wangu kwako na kwa akiri yangu timamu nakiri kwamba endapo utaufata vizuri basi utaishi maisha safi duniani wewe pamoja na familia Yako, na pia utaacha uridhi mkubwa kama uliopwewa wewe kwa watoto wako, sina mengine nakutakia utekelezaji mwema.nikumbuke kwenye ufalme wako boss na endapo utahitaji namba ya Mpesa nitakupatia. Ahsante sana.