Nina ndugu yangu analipwa milion 5 salary , ila ni mbahili sana na yeye yupo tayari kutoa pesa asomeshe lakini sio vitu vingine ni mtu wa protocal sana, namkubali sana na tunaelewana sana, shida yake ni mtu wa uchumi sana pamoja na kulipwa hela nyingi anajibana lakini hela yake inapotea pasipo ona amefanya kitu gani, ni ngumu kumjua kama ana hela au lahasha kuna mtu amemkopesha hela nyingi na hajarudishiwa mpaka leo na huyo mtu nilimkanya maana tayari na mimi nilishamkopeshaga, sasa bado yupo anapanga mpaka leo ana kiwanja kikubwa ila hajapiga hatua za ujenzi, so ni vyema ndugu zangu kiushauri mtu uwe na mkakati juu ya pesa unazozipata tusaidie lakini kuwe na mpango wa kukuendeleza wewe binafsi, kutoa ni kitu kizuri chenye baraka ila ni vyema kuwa makini unavyotoa