Ushauri: Ninunue kiwanja au nifanye biashara?

Ushauri: Ninunue kiwanja au nifanye biashara?

Kama unahakika na mmiliki wa kiwanja hicho kinunue upesi..kama vip niunganishe na muuzaji nilipe ela yake shaa..afu baada ya miez michache nikipige bei mil 5
 
Kama kina ukubwa huo (almost 20m x 20m) kwa bei hiyo kinunue haraka. Probably hakijapimwa na unaweza kufuatilia hati mapema ili kukiongezea thamani. Achana na biashara ya Bodaboda kwa sasa. Itakutia mawazo tu.
Asante sana kwa ushaur
 
tehe...teh....kwa mazingira yako nunua kwanza hicho kwakuwa bado unaogopa kuwahi kijijini lakini zingatia pia yafuatayo:-
je kiwanja kinafikika? isije ikawa kiwanja hakina njia ya kupita, gharama za ujenzi zinaweza kuwaje kama utaamua kujenga kina mwinuko,bondeni, tambalale.? huduma za maji na ubebaji wa maji ukoje wakati wa ujenzi? je mipango ya serikali katika eneo hilo ikoje isije ikawa barabara inapita ndo mana wanauza? kuwa na uhakika na taarifa sahihi za mmiliki.
Poa mkuu nitazingatia kesho mapema tu naenda kukiona na watu wangu wazoefu wa hizi habari
 
Usitake kujua uhalali wa bei mkuu,cha msingi ni kujua hilo eneo anayr limiliki analimiliki kihalali au kimagumashi na kama hakuna mgogoro nadhani haliwezi kuuzwa kwa bei hiyo ,kwa maana nyingine unanunua kesi.
Ngojea nitafuatilia kwa undani zaidi,japo kua ni rafiki yangu wa karibu simuamini sana pia hela yangu nilivyoipata kwa tabu siwezi itoa kizembezembe namna hiyo
 
Nunua kiwanja tafuta zingine endelea na biashara
 
Kuwa mwangalifu na ununuzi wa viwanja ...usiende kichwa kichwa ukakosa bodaboda, kiwanja, na fedha!
 
Kununua kiwanja ambacho hakizalishi chochote ni = kununua liability badala ya asset, lakini pia kufanya biashara ya bodaboda kwa mtaji huo bila wewe mwenyewe kuwa dereva utakuwa unataka kufanya liability bussiness badala ya asset bussiness, hebu fikiria je bodaboda au kiwanja ama kitu kingine, kipi kati ya hivyo kitakuwa asset kwako?
 
Wakuu leo nimeenda kukiona kiwanja,
Kipo mbande ndanindani huko wanapochimba mchanga na kinaukubwa wa mita 18 kwa 18.pia kipo mbali na barabara yani kutoka mbande ili kufika huko inabidi uchukue bodaboda na bei ni ileile 1.3M.
LAKINI NDUGU ZANGU WAKATI WA KURUDI TULIPATA AJALI KIDOGO YA BODABODA WAKATI TUNAPANDISHA KILIMA CHA MCHANGA YANI KILIKUA STEEP NA BODABODA IKABINUKA NA KUTUMWAGA SOTE BUT THANKS GOD I'M SAFE!!
d79b095960a3df85192629c43323dc27.jpg
226b66aa03e98b06850842d0b1d77a9a.jpg
64e25eea936377928f414e069f1b8238.jpg

Cc: Kyawanjubu
Devon sawa
Chiwa
Consultant
Na wengine mnakaribishwa kwa mchango
 
Kununua kiwanja ambacho hakizalishi chochote ni = kununua liability badala ya asset, lakini pia kufanya biashara ya bodaboda kwa mtaji huo bila wewe mwenyewe kuwa dereva utakuwa unataka kufanya liability bussiness badala ya asset bussiness, hebu fikiria je bodaboda au kiwanja ama kitu kingine, kipi kati ya hivyo kitakuwa asset kwako?
Ndugu unaweza nifafanulia kidogo hicho kiwanja kinavyoweza kua regarded as liability
 
Nunua KIWANJA.pia hiyo Bei ni nzuri sana kwako hata kama hakijapimwa.kwa wastani utakuwa umenunua square meter moja chini ya Tsh 840
 
Back
Top Bottom