Ushauri: Ninunue nyumba au kiwanja?

Ushauri: Ninunue nyumba au kiwanja?

Banjuka

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2021
Posts
1,007
Reaction score
1,922
Salaam Jamiiforums,

Naombeni msaada wa mawazo, niko na njia mbili ila sijui niifate ipi?

Nimeitiwa mahali kuna kiwanja kinauzwa milioni 20, wakati huo huo nikaitiwa sehemu nyumba inauzwa milion 35. Je, niache kununua kiwanja ninunue nyumba?

Naombeni msaada wa mawazo.
 
Nunua kiwanja, jenga nyumba unayoitaka wewe

Angalia mahali kiwanja na nyumba zilipo je wapi panakufaa?

Kuna nyumba watu hutumia vifaa hafifu katika ujenzi

Kuna nyumba umeme haujaungwa vizuri
 
Inategemea location, kilicho kwenye location nzuri (miundombinu, ukaribu na huduma na mahitaji muhimu) ndicho unachoswa kuchukua.

Vv
 
jenga nyumba mwenyewe, hii itasaidia kujenga nyumba yenye standards unazozitaka
hizo za kununua ni zile za mfuko wa dangote mmoja unatoa blocks 100
 
1. Ubora wa nyumba
2. Location ya vyote
3. Mfuko wako
4. Personal preferences

Hapa hamna mtu ataweza kukupa ushauri nini cha kufanya, lazima uwe na KPIs zako
 
Nunua nyumba wacha kupoteza muda aisee!! Wenzetu wazungu hawana muda wa kupoteza kujenga nyumba....una-bargain kama ni 35M unashuka nao mpk 25-28 ,unanunua...unaendelea na mishe nyingine.
 
Angalia location kwanza maana sahivi ukipata nyumba hata Kama ni ya tope Kama hipo sehemu nzuri unaweza kufanya Makubwa Sana.
 
Nunua nyumba,Kama Kuna biashara unafanya ,ikopee benk,zungusha ela kwenye biashara,nunua kiwanja ,jenga nyumba ya ndoto zako
 
Kama nyumb ipo eneo ambalo unalitak na nyumb inakukiz nunua nyumba usije potez muda na mafundi
 
Inategemea na sehemu na pia hiyo nyumba ya 35m huenda inaweza kuwa zile nyumba za mfuko mmoja wa cement matofali 50
 
Back
Top Bottom