Ushauri: Nioe yupi Kati ya hawa wanawake wawili?

Ushauri: Nioe yupi Kati ya hawa wanawake wawili?

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,325
Reaction score
7,807
Habari za siku wadau

Kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu katika mapambano ya kutafuta mwenza wa maisha nimejikuta naangukia kwa wanawake wawili ambao wote naona ni bora wanavigezo vile nilivyokuwa nahitaji.

Mimi siku zote nimekuwa navutiwa zaidi na mwanamke ambaye hana tamaa ya vitu vikubwa hapo ndipo nilikuja kumpata binti mmoja hivi miaka 20 mpaka sasa tunamiezi mitatu ya uchumba nilimuhaidi mambo mengi sababu kweli na lengo kumuoa kabisa huyu mwanamke.

Huyu mwanamke hana tamaa halafu ni mzuri sema mazingira ya kwao ni magumu kwa kipato nilikuja kugundua ata chakula kwao hapati milo mitatu nikamuuliza kwanini alikuwa aniambii akasema yeye analizika tu na hali iliyopo mana ndio maisha aliyokulia.

Hivyo nilijitahidi kumpa mahitaji yake yote ambapo pale anaona anakwama ata pale alipoumwa mimi nilikuwa bega kwa bega na huyu mchumb wangu kuna siku alipata homa mama yake akaenda kumchukulia dawa bila vipimo hapo nilipogundua hawakuwa na hela kwenda hospital. Ikabidi mimi nitoe hela akaenda hospital.

Sasa kiufupi huyu binti yeye akiomba hela basi ni ya kusukia tu ama vocha ana aibu Sana ata nikimpigia tuongee huwa haoneshi ushirikiano kuna vitu vingi huwa nahitaji kuvijua lakini hanipi ushirikiano.

Na shida zaidi katika hii miezi mitatu kuja kwangu inakuwa changamoto kila tunavyohaidiana kukutana siku ya jumapili yani sababu lazima itokee mara sijaja sababu ya jambo fulani najaribu tukutane hata sehemu nyingine tofauti na kwangu, bado sababu zinajitokeza ikabidi nimuulize kwanini inakuwa hivi akaniambia mama anavoenda kutafuta anamuachia bibi hivyo anashindwa kutoka.

Sasa huu ni mwezi wa tatu nachojiuliza siku zote yeye yupo bize sitaki kukubaliana na hili mpaka sasa sioni dalili mimi pia nahitaji mahitaji yangu kama mwanaume nahitaji kupata kwa mwanamke naye mpenda.

Mpaka sasa nipo njiapanda sijui nimuache ama niendelee kumpa muda? Mana nimemuuliza kama yupo tayari kuishi na mimi kasema nisijali muda ukifika nitamuoa Imebidi nitafute mbadala ili niweze kupata mahitaji yangu.

Wiki hili nimejikuta nakutana na binti mwingine hapa mtaani ni binti wa huko geita huyu anamiaka 22 huyu naona yupo tofauti Sana na yule mchumba wangu katika hizi siku chache tulizokutana huyu binti amenielewa San.

kila Napo muhitaji anakuja atakama yupo bize na yupo tayari tuanze kuishi pamoja mana inaonekana kaipenda rangi yangu yupo tayari tuzae sasa jana amerudi kwao kusalimia ila nae tumepanga mengi
 
Mkuu,
Binti namba 1, umefahamiana naye kwa miezi 3
Binti namba 2, umefahamiana naye kwa wiki 1
Leo, upo mbele yetu ukiomba tukupe ushauri wa uoe yupi kati yao...

Ushauri:
Jenga mahusiano ya angalau mwaka (yaani si chini ya mwaka), ili uweze tambua tabia ya mwanamke, muda uliokaa nao ni mfupi mno kuweza kuamua yupi wa kuoa...

Unapotaka kuoa, hutizami tabia tu ya mwanamke, unadadisi kujua hadi familia wanazotokea hao unaowahitaji...

Kitu ninachoona kitakuponza, ni kulinganisha binti 1 na binti 2 badala ya kutazama ni vitu gani unavyohitaji mkeo mtarajiwa awe navyo...

Oa mtu unayemfahamu ndani na nje
 
Nilichogundua bado hujajua maisha ya uchumba ni tofauti sana na maisha ya ndoa [emoji3][emoji3]

Anyway nisiende mbali sana ushauri wangu muoe anaekupenda sio unaempenda zingatia sana hayo maneno mawili
 
Ushauri mzuri ila huwa nawaza itakuwaje nitakaa na mwanamke mda mrefu halafu kumbe ana mwanaume mwingine mwanzo wakati tunajuana alinitambulisha rafiki yake siku ndio ilikuwa ndio mwisho wa kuonana wakati tupo pamoja watatu rafiki yake alisema huyu rafiki yangu hana Tamaa kabisa ila atakacho kusumbua huyu ni msiri
 
Na ukioa akapata mwingine.
Ndoa na mahusiano ni risk kila sehemu. Do ur party kuwa na imani hata ya kinafiki kuwa huchapiwi
 
~Kama dini unakurudusu oa wote
~Wewe kinachokuharibia ni tamaa ya mbususu hamna kingine kisa huyu yupo available sana wowote unaona ndio anakufaa haya bwana
~USHAURI wangu kaa nao wote kwa uchumba walau miezi sita kila mmoja ujue tabia zao vizuri halafu ndio uje hapa tukushauri
 
Una rangi gani mkuu mpaka imependwa hivyo? Hakuna kingine kakupendea huyo wa pili?

Una umri gani na unajishughulisha na nini?
Na miaka 26 siwezi kusema moja kwa moja kuwa mwanamke kanipenda sababu ya rangi ila kwasababu nimemuonesha upendo binti huyu nimeona ana utayari anaonesha matumaini pia wakati nimejuana nae nimeongea nae mambo ya muhimu na ya msingi nimemuhaidi mengi kwa hili nazani ndio imepelekea kuvutiwa na mambo mengine ya kawaida kama muonekano wangu wa nje pia
 
Ushauri mzuri ila huwa nawaza itakuwaje nitakaa na mwanamke mda mrefu halafu kumbe ana mwanaume mwingine mwanzo wakati tunajuana alinitambulisha rafiki yake siku ndio ilikuwa ndio mwisho wa kuonana wakati tupo pamoja watatu rafiki yake alisema huyu rafiki yangu hana Tamaa kabisa ila atakacho kusumbua huyu ni msiri

Huo unaoita muda mrefu ndio muda sahihi unaoweza kukupa majawabu kadha wa kadha, kujenga urafiki, kutambua malengo n.k

Hadi sasa umeweza kujua tabia chache mathalani hiyo ya usiri kea huyo binti 1, pengine muda ukisogea unaweza ukajua sababu ya yeye kiwa msiri ni ipi, pengine hana watu anaowaamini...
 
Mwanaume ukifeli kwny kuchagua wakuoa, ujue umefeli maisha.

Umekua haraka mno kufikiria maamuz ya kuoa wkt mahusiano yenyewe na hao wanawake wote bado Sana.

Utakuja kuigiziwa afu uje upigwe kitu kizito, ebu jipe Muda kwanza mkuu.

EPUKA MIHEMIKO NA HISIA, TUMIA ZAID AKILI

Sichelei kusema Ayo maamuz ya kuoa kwa Sasa UMEKURUPUKA[emoji4]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hivyo ndio vigezo vyako vya kuoa bado una safari ndefu sana!!!!
 
Habari za siku wadau

Kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu katika mapambano ya kutafuta mwenza wa maisha nimejikuta naangukia kwa wanawake wawili ambao wote naona ni bora wanavigezo vile nilivyokuwa nahitaji.
Kama uko iringa kama username inavyojitambulisha nakusihi usidanganyike Usioe hata mmoja hata mwenye vinasaba vya watu Wa huko hata kama ww ni MTU wa huko.
UTANISHUKURU
 
Nilichogundua bado hujajua maisha ya uchumba ni tofauti sana na maisha ya ndoa [emoji3][emoji3]

Anyway nisiende mbali sana ushauri wangu muoe anaekupenda sio unaempenda zingatia sana hayo maneno mawili
Mimi namuambia km anataka jufanikiwa maishani mwake amuoe anampenda ikiwa hiyo mwanamke yupo tayari kuolewa na yeye
 
Back
Top Bottom