Ushauri: Oda za wateja zimezidi mtaji nilionao

Waambie wakupe advance fikishia baadhi wakikupa full fikishia wengine, kuwa muwazi itakusaidia kulinda reputation na clients wako, usikope kwa riba ita kucost
 
Weka wazi usaidiwe capital au uingie share na mtu muwe pamoja,

Kama hela unayoitaji haizidi milion 1 nitafute tuyajenge, tuone tunapambana vip

Mi nishavurugwa na TRA
 
Point ya pili imekaaa ki mtego kuna watu watalia hapa
 
1. NNdhani ni kosa wewe kukubali kushi dwa ku deliver. Ukikiri tu, hutakaa upate tena wateja
2. Nenda kwa supplier wako, ongea nae kiutu uzima upewe mali kauli ufanye delivery on time na ukilipwa straight kampe hela yake
 

Usiogope kukopa kama una uhakika na biashara hiyo. Nenda kakope… kosa kubwa utafanya kwenda kuwaambia wateja wako kuhusu financial difficulties zako, utajuta, wata yeya wote.
 
Unafanya biashara gani mkurugenzi! Maana hakuna biashara mpya kwa sisi wabongo. Hivyo sitegemei unifiche.
 
Kama partner aje na mtaji kiasi gani na atanufaikaje?
Asante
 
jamaa anakomaa kuficha code ya biashara yake wakati ushaishiwa mtaji. we wazi utashauriwa kulingana na aina ya biashara
 
kama mtaji NI mdogo kuliko oda za wateja, nakushauri ufanye yafuatayo/ Moja Kati ya yafuatayo;
1.Omba mkopo Kwa taasisi zinazotoa mkopo Kwa wajasiliamali(mfano bank)
2.Anzisha mpango wa wateja wako kulipia pale wanapoweka oda/kabla ya kupata bidhaa( bila shaka wateja wako wengi ambao wanaweka oda wameshajenga uaminifu na wewe,sasa cha kufanya wasiliana nao na uwaambie wafanye malipo ya bidhaa mara wanapoweka oda/ kabla ya kupata, bidhaa,washawishi Kwa sababu za msingi! Mfano unaweza kuwaambia kuwa hii nikutokana madiliko kidogo ya kampuni ninayofanya nayo Kazi au sababu yoyote inayoeleweka, wanaweza kulipa fedha yote au nusu ama asilimia kadhaa za gharama,alafu wewe utaitumia kununua bidhaa zinazokidhi haja ya uhitaji.Sio wote watakubali Ila watakao kubali fanya nao KAZI, jitahidi unakuwa Makini usipoteze mteja hata mmoja Kwa sababu Tu ulivunja uaminifu Kwa kumuahidi atapata bidhaa alafu akakosa Kwa Muda mliopangiana, ikitokea umeshindwa kuwakamilishia oda zao basi wape taarifa mapema na utoe sababu nzuri ili next time wakuamini tena.
3.Wasiliana na mahali ambapo wewe huwa unalangua bidhaa zako,na uwaambie kuwa wakupe bidhaa kisha utawalipa ndani ya MDA fulani,waeleze Hali halisi kuwa idadi ya oda za wateja ni kubwa kuliko kiwango unachoweza ku-afford.Naweza kukupa ushauri bure wasiliana na Mimi;
Raphael Mathew Kalolo (mwanafunzi wa shahada ya Kwanza ya biashara Katika chuo cha biashara CBE dar es salaam)
phone:0756401790
email: raphaelmathewkalolo@gmail.com
Instagram: raphaelkalolo23
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…