Ushauri pls

Ushauri pls

Habarini za asbh wana MMU
kuna rafiki yangu anahitaj ushauri nimeona nilete kwenu mtamsaidia, amechukua mkopo benki wa tshs 8000000 (milion nane) ambazo atakatwa kwenye mshahara wake kwa muda wa miaka miwili, lkn mpaka sasa yuko kwenye dillema hajui afanye kitu gan na hzo pesa, hana kiwanja, anataman kufungua biashara. Lkn mi nikamshauri aachane na biashara kwanza kwa sbb pesa itaweza potelea yote huko na atapata maumivu ya kukatwa mshahara kwa miaka miwili.

Naomba mumshauri na nyie jaman.
Kiokote

Afu hili ni jukwaa la mapenz..mahusiano wewe unaleta habari za mikopo na biashara
 
Ushauri mzuri kabisa, achukue hizo pesa arudishe, wale tu ka interest kidogo hako katakakokua kamebaki awe kajifunza.. Huwezi chukua mkopo bila kua na plan, unaanzaje plan ukishapata mkopo?? kama ni plan mbovu je?

Arudishe pesa ya watu isije potea akajuta, akae apange plan vizuri biashara gani atafanya, itamcost vipi, risk zake ni zipi, market yake ni akina nani, competition yake ni ipi, plan nzima iandikwe vizuri then ndo aende akaombe mkopo au ajaribu kutafuta njia nyingine za kutafuta pesa na sio kujiingiza kwenye madeni tu...

Hiyo inaitwa kumpa mtu makavu......duuuh
 
asa kama hajui afanyie nini hixo pesa alizichukua za nini?
ka vp mwambie akahongee malaya
 
Kama hajui la.kufanya ni hatari kukaa na hizo pesa maana matatizo yatajitokeza na atazitumia tu.

Mi nina ushauri wa aina mbili:

1. Anunua kiwanja au shamba pembezoni mwa mji. Kwa hakika hili hatakuja kujutia hata siku moja maana viwanja vinapanda thamani kwa kasi na faida yake kwa mwaka ni zaidi ya ile ambayo angeipata kwa kufanya biashara halali. Halafu anaweza kuishi kwa kiasi kidogo cha mshahara anaopata akifanya utafiti wa nini cha kufanya.

2. Anaweza pia kununia vipande vya UTT. Uzuri ni kwamba navyo vinapanda thamani na kuna uwezekano wa kuchukua hela yake endapo ataihitaji soku za usoni kwa kuwauzia vipande hao UTT wenyewe na akapata pesa yake ndani ya siku 10. Pia ana uwezo wa kukopa kutoka kwenyw benki yao ya UTT asilimia 80%ya thamani ya vipande vyake huku vipande vikiendela kuo gezeka thamani.
 
Azirudishe benki kisha awaombe msamaha kwamba alichukua pesa bila kujua cha kuzifanyia!
 
Kama hajui la.kufanya ni hatari kukaa na hizo pesa maana matatizo yatajitokeza na atazitumia tu.

Mi nina ushauri wa aina mbili:

1. Anunua kiwanja au shamba pembezoni mwa mji. Kwa hakika hili hatakuja kujutia hata siku moja maana viwanja vinapanda thamani kwa kasi na faida yake kwa mwaka ni zaidi ya ile ambayo angeipata kwa kufanya biashara halali. Halafu anaweza kuishi kwa kiasi kidogo cha mshahara anaopata akifanya utafiti wa nini cha kufanya.

2. Anaweza pia kununia vipande vya UTT. Uzuri ni kwamba navyo vinapanda thamani na kuna uwezekano wa kuchukua hela yake endapo ataihitaji soku za usoni kwa kuwauzia vipande hao UTT wenyewe na akapata pesa yake ndani ya siku 10. Pia ana uwezo wa kukopa kutoka kwenyw benki yao ya UTT asilimia 80%ya thamani ya vipande vyake huku vipande vikiendela kuo gezeka thamani.

Thanks kwa ushauri mzuri
 
kama alichukuwa na hakujuwa cha kufanyia mwambie awe anauzuria bar na guest na anatoka na mdemu wa kali atakuwa amepata cha kufanyia
 
Mwambie aje twende Vamizi Island tukale bata.......mil 8 tunakwenda na kurudi inatosha kabisa..........chenchi tunakwenda Serengeti kuangalia wanyama.............
 
Duh hapo pagumu

Ngoja nikushauri kwa hasira,kwa niaba ya rafiki yako! Nimetanguliza hasira kwa kuwa mara nyingi resources zinatakiwa kumfuata mtu mwenye vision na sio vision kumfuata mwenye resource...hii ni kanuni ya asili!

Cha kufanya sasa anaweza kuwaona Consnet Group Limited walio Tancot House 1st/3rd Flr. Sokoine/Pamba Rd Dar es Salaam ambao ni wataalamu wa kilimo cha kisasa, mwone ndugu Sanctus Mtsimbe na timu yake watakushauri accordingly kisha utarudi hapa kutupa mrahaba!
 
Last edited by a moderator:
Mwambie aje twende Vamizi Island tukale bata.......mil 8 tunakwenda na kurudi inatosha kabisa..........chenchi tunakwenda Serengeti kuangalia wanyama.............

Kweli??? Nilidhani kwenye seriousness watu hupeana constructive ideas, wengine wana mitaji ila hawajui waanzeje...wasaidieni bwana..!!
 
Hivi mtu unakopaje wakati hujui pesa unaenda kufanyia nn?
Business idea comes first then we think of sources of capital.

Mwambie akatoe sadaka kanisani
 
Yeah ni wazo zuri though mi nilimshauri anunue kiwanja kwanza ajenge nyumba yake ili siku moja aushi kwakwe

Akinunua kiwanja nje ya mji akajenga hata chumba na sebule na akaacha kulipa kodi itamsaidia kupunguza gharama za maisha na itampatia nafasi ya kujipanga vyema.
 
Back
Top Bottom