real lyf 2015
Senior Member
- Aug 13, 2015
- 166
- 27
Habarini za asbh wana MMU
kuna rafiki yangu anahitaj ushauri nimeona nilete kwenu mtamsaidia, amechukua mkopo benki wa tshs 8000000 (milion nane) ambazo atakatwa kwenye mshahara wake kwa muda wa miaka miwili, lkn mpaka sasa yuko kwenye dillema hajui afanye kitu gan na hzo pesa, hana kiwanja, anataman kufungua biashara. Lkn mi nikamshauri aachane na biashara kwanza kwa sbb pesa itaweza potelea yote huko na atapata maumivu ya kukatwa mshahara kwa miaka miwili.
Naomba mumshauri na nyie jaman.
Kiokote
Ushauri mzuri kabisa, achukue hizo pesa arudishe, wale tu ka interest kidogo hako katakakokua kamebaki awe kajifunza.. Huwezi chukua mkopo bila kua na plan, unaanzaje plan ukishapata mkopo?? kama ni plan mbovu je?
Arudishe pesa ya watu isije potea akajuta, akae apange plan vizuri biashara gani atafanya, itamcost vipi, risk zake ni zipi, market yake ni akina nani, competition yake ni ipi, plan nzima iandikwe vizuri then ndo aende akaombe mkopo au ajaribu kutafuta njia nyingine za kutafuta pesa na sio kujiingiza kwenye madeni tu...
Azirudishe benki kisha awaombe msamaha kwamba alichukua pesa bila kujua cha kuzifanyia!
Kama hajui la.kufanya ni hatari kukaa na hizo pesa maana matatizo yatajitokeza na atazitumia tu.
Mi nina ushauri wa aina mbili:
1. Anunua kiwanja au shamba pembezoni mwa mji. Kwa hakika hili hatakuja kujutia hata siku moja maana viwanja vinapanda thamani kwa kasi na faida yake kwa mwaka ni zaidi ya ile ambayo angeipata kwa kufanya biashara halali. Halafu anaweza kuishi kwa kiasi kidogo cha mshahara anaopata akifanya utafiti wa nini cha kufanya.
2. Anaweza pia kununia vipande vya UTT. Uzuri ni kwamba navyo vinapanda thamani na kuna uwezekano wa kuchukua hela yake endapo ataihitaji soku za usoni kwa kuwauzia vipande hao UTT wenyewe na akapata pesa yake ndani ya siku 10. Pia ana uwezo wa kukopa kutoka kwenyw benki yao ya UTT asilimia 80%ya thamani ya vipande vyake huku vipande vikiendela kuo gezeka thamani.
Duh hapo pagumu
Mwambie aje twende Vamizi Island tukale bata.......mil 8 tunakwenda na kurudi inatosha kabisa..........chenchi tunakwenda Serengeti kuangalia wanyama.............
amechukua mkopo kabla ya kujua hizo fedha atazifanyia nini?
Ni maajab kwa kweli
Hivi mtu unakopaje wakati hujui pesa unaenda kufanyia nn?
Business idea comes first then we think of sources of capital.
Mwambie akatoe sadaka kanisani
Kweli??? Nilidhani kwenye seriousness watu hupeana constructive ideas, wengine wana mitaji ila hawajui waanzeje...wasaidieni bwana..!!
Yeah ni wazo zuri though mi nilimshauri anunue kiwanja kwanza ajenge nyumba yake ili siku moja aushi kwakwe
Akinunua kiwanja nje ya mji akajenga hata chumba na sebule na akaacha kulipa kodi itamsaidia kupunguza gharama za maisha na itampatia nafasi ya kujipanga vyema.