Huyu mstaafu!
Ndie aliyeanzisha ufisadi mkubwa katika nchi hii enzi za utawala wake.
ESCROW,RICHMOND,MEREMETA,SYMBION,IPTL .hizi
Zote ni kashfa za enzi zake!
Sasa ameshikilia Remote bila aibu na anatupelekesha na DP-WORLD!
Hataki kuachia remote akiamini kuwa anao ubavu wa kutupelekesha kwa ushirika na "RA".
Fisadi kubuhu ambaye amerudi kwa kasi ya 5G kwenye awamu hii ya mteule wao maushungi!
Je!
Watanzania mnakubali hali hii mpaka lini?
Nchi inaelekea kugawanyishwa kwa makundi mawili yenye maslahi tofauti.
1-Wapinga mkataba mbovu wa DP-WORLD!
Ambao wana maslahi mapana ya upendo kwa nchi yetu Tanganyika.
2-Waliouleta mkataba baada ya kutundikwa picha zao ukutani huko Emirati.
Kwa maslahi mapana ya matumbo yao mapana yasiyotosheka.
Kama Rais mstaafu analipwa mshahara 80% ya Mshahara wa Rais aliyeko madarakani currently.
Pia anaruhusiwa kutibiwa katika hospitali za kimataifa huko ughaibuni.
Anao walinzi na madereva wa serikali muda wote wa maisha yake.
Huku pia akipewa mgao wa gari mpya kila baada ya miaka mitano.
Amejengewa nyumba ya kifahari na serikali.
Na bado anazo nyumba lukuki za serikali alizojimilikisha toka zile zilizokuwa za serikali.
Walizojiuzia kinyemela....
Yoote hiyo haridhiki nazo na bado anataka kuliyumbisha taifa kwa kutaka mali zaidi!
Sasa naanza kuwaelewa wale viongozi wa Mapinduzi wa Niger dhidi ya Rais bilionea muuza Nickel ...Boughum!
Mungu Inusuru Tanzania [emoji1241] [emoji813]
Moderators....please msifanye yenu kuufuta uzi huu.
Ni kwa maslahi mapana ya nchi yetu Tanzani.
Nawaomba sana ...sana..sana!
AHSANTENI na asubuhi njema.
Maana kwa sasa JF ndio media platform pekee tunayoitegemea.
Huko kwingine kwishney!