Ushauri: Rais Samia apumzike Urais 2025

Ushauri: Rais Samia apumzike Urais 2025

Uangalie mastakabali wako wewe kama rais, uangalie mustakabali wa chama chako kilichopo madarakani na mwisho ndio tunaangalia masilahi ya nchi.

Kwamba rais anaweza kufanya kufanya jambo fulani au kutofanya jambo fulani kwa masilahi yake au kwa kuangalia kwanza mustakabali wa chama chake kilicho madarakani.
 
Kwanza niseme wazi Mama ni moja ya Marais bora kabisa kuwai kutokea katika taifa letu. Sijawai kusikia kashifa yeyote ya wizi na ufisadi kutoka kwake, ni Rais mwadilifu kweli kweli.
Mbona unapingana na mada yako mkuu 'technically'.

Tuchukue lipi na tuache lipi?
"...ni moja ya marais bora kabisa..."? Hapana.
 
Mbona mbali sana 2025.

Hata Leo
Nchi inapoteza nafasi ya kwenda mbele, inakalia kusubiri watu wamalize ngwe zao!

Atakayeingia na yeye atapiga kivyake, nchi inarudi nyuma au inasimama, haiendi popote kimaendeleo!

Watu hawajali mradi matumbo yanajaa!
 
Nchi inapoteza nafasi ya kwenda mbele, inakalia kusubiri watu wamalize ngwe zao!

Atakayeingia na yeye atapiga kivyake, nchi inarudi nyuma au inasimama, haiendi popote kimaendeleo!

Watu hawajali mradi matumbo yanajaa!
Nakubaliana na wewe mkuu.

Na atutoendelea kamwe kwa style ya kila raisi anaingia madarakani anakuwa na agenda yake.
 
Mimi ni mlala hoi wewe mlala hio unazijua hizo sababu si uziweke hapa?
Hoja yako imefeli kuonyesha hujui sababu ya znz vitu bei rahisi kuliko bara, hujui mambo ya nchi yaendavyo unafata mkumbo tu,
Huna tofauti na walalahoi waliodanganyika na yule mwovu kua kila alifanikiwa ni mwizi na mchawi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Bila tajiri maskini hana maisha....
 
Nyie waislamu wabaguzi sana nyie ndo mnaleta udini mtu asiambiwe ukweli bila shaka wazanzibar mna lenu
Nani kakwambia mimi muislamu? Harafu acha kuwasingizia waislamu..

Nimefanya observation Rais akiwa muislamu kuna kuwa na chokochoko za kipuuzi na hizi hutoka kwa Wakristo.
 
Ukisema utawala wa kijinga unamhusisha Rais wetu mama, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais Hawa wote ndio walikuwa watawala wetu awamu ya tano..kwahiyo nakukanya ku generalize Mambo..ukome...kama umechoka kuishi Basi Hana nenda nchi nyingine..hatuwez ona mnatukana viongozi wetu tunanyamaza tu..narudia ukome..kama msumeno wa Sheria haujakufikia
😂😂😂Huwa wanatumia busara kumkana.Haujawahi kuwaelewa?
 
Apumzikee Tu. Yaani arest kabisa
Kwa mtazamo wangu binafsi napendekeza Rais wetu Mama Samia apumzike mwaka 2025 kama analo wazo la kuendelea kutuongoza.

Kwanza niseme wazi Mama ni moja ya Marais bora kabisa kuwai kutokea katika taifa letu. Sijawai kusikia kashifa yeyote ya wizi na ufisadi kutoka kwake, ni Rais mwadilifu kweli kweli.

Ila shida yake ipo kwenye kuchukua hatua juu ya watu wanaomzunguka na kufanya mambo ya hovyo katika utawala wake.

Naunga mkono michakato yote ya kodi inayoanzishwa kufanyika Ila shida ipo kwenye matumizi yake ni jinsi gani tunaitumia hiyo pesa inayopatikana kwenye kodi, mfano serikali kwa ujinga imetumia bilioni 629 kwenye zoezi la sensa pekee huu ni ufisadi.

Zoezi lenyewe watu wengi bado hawajahesabiwa mpaka sasa. Leo ni siku ya 6 ndani ya zile siku saba zilizopangwa maana yake kesho ni siku ya mwisho. Zoezi limegubikwa na wizi na ufisadi wakati zoezi lingewatumia mabalozi wa nyumba kumi tu na mwenyekiti wa kijiji lingekuwa limeshakamilika kwa 100%.

wangetumia karatasi za kawaida kujaza taarifa za watu, then kwenye kata ndio wangeweka mfumo wa TEHAMA wa kuingiza zile taarifa kwa kutumia tablet tungefanikiwa kwa 100%

Kukwama kwa zoezi la katiba na tume huru ya uchaguzi kabla ya 2025, ili nalo ni donda ndugu. Watu wanakushauri kwamba utashindwa uchaguzi 2025 ukileta sasa Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Wanakudanganya ungeweka mazingira sawa ya uchaguzi na katiba lazima watu wangukupigia kura 2025 ili kulipa mema uliyowafanyia hata kama wasingekuchagua mema yako yangeandikwa duniani na mbinguni.

Swala ya mfumuko wa bei ndio bomu kuu, watu hawakatai kwamba vitu vinapanda duniani lakini watu wanachokataa ni kwanini vitu muhimu ndio vipande tu kwani vitu vingine ambavyo havipandi vitu havisafirishwi?

Mfano unakuta kiberiti kinauzwa shilingi 100 Tanzania nzima hakipandi bei zaidi ya miaka 10, wakati na chenyewe kinatumia mafuta kuzalishwa. Ila Ngano, mafuta ya kula na sembe inapanda kila muda kila mwaka.

Utasikia usafirishaji, kwanini mafuta ya alizeti yanayozalishwa Rukwa na Singida hapo hapo kiwandani ukiyafuata yana bei ile ile kama unayoinunua Dar es salaam?

Mh. Rais hapa tukubaliane kwamba umeshindwa ku control inflation kwa sasa, mwezi umepita mafuta yanashuka kila siku kwenye soko la dunia kwanini sisi mafuta yanazidi kupanda tu?

Kwanini uwashughulikii wafanyabiashara Ili waache ulafi wa kutaka faida kubwa?

Tofauti yetu na Zanzibar iko wapi, kwanini Zanzibar kila kitu kinachoingizwa kwenye visiwa hivyo bei zake zipo chini, hata bei zao za mafuta zipo chini kuliko sisi au ndio kusema Zanzibar ni taifa tofauti na sisi?

Basi Kama hivyo Rais Mwinyi ana uwezo wa kupambana na mfumuko wa bei vile, bora tumchukue aje atusaidie huku bara baada ya 2025.

Mambo ni mengi, Ila naomba nikushauri kama unahitaji heshima ya milele basi pumzika 2025 aje mtu mwingine afanye kazi ya Urais. Inawezekana watu wanakushauri vibaya kwa sababu haukuchaguliwa na wananchi ili kukuchonganisha kwa watanzania.
Rest
 
Kwanza nikupongeze mtoa post, lakini nikukumbushe Jambo moja .

Tanzania tunatatizo la mfumo wa utawala na uongozi ,pengine rais au ma- rais tumekuwa tukipata wazuri tu Ila baada ya mda kidogo wanaanza kuharibiwa na mfumo.

Kuhusu 2025 , nashauri SAMIA SULUHU HASSAN agombee tena na akifanikiwa kushinda aendeleze miradi ya serikali na kukamilisha baadhi ya mambo yatakaoyo kuwa tayari kukamilishwa .

Ndani ya CCM hakuna mtu wa kumuamini Kwamba ata fanya maajabu , hata hivyo bado tunamuona SAMIA ameniahidi Sana kutengamanaisha nchi ukilinganisha na MAGUFULI , Kumbuka KUPOTEA KWA WATU NA KUKUTWA VIROBA VYA MAITI BAHARINI ,KUTEKWA KWA WATU KM MO,MKATORIKI NK ,KUPIGWA RISASI KWA LISSU,KUPOTEA KWA BENI SAANANE,AZOLE GWANDA NK.

Vilevile kumbuka kwa matajiri na wafanya biashara kuporwa pesa za biashara zao mpaka nchi kuwa mahututi kiuchumi hasa "private sector" bila upendeleo naona SAMIA ameirudisha kwenye mstari private sector.

Nasmshauri Rais aendeleze miradi yote ya maana aliyo ikuta na aliyo introduce chini ya uongozi wake . Na awasimamie kwa karibu sana wasaidizi wake ili wasimzidi unanja huku akiangalia kwa makini mambo yanayo lalamikiwa na wananchi.
 
Inshort hawa ccm akili imefika mwisho walete katiba ikiwezekana tuwe na wagombea huru hivi vyama upuuzi tu.
 
Back
Top Bottom