Ushauri: Rais Samia, simama uite viongozi wa dini wamuombe Mungu toba na atuteremshie MVUA zenye manufaa. Hali ni tete kwa Taifa

ToniXrated

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
1,134
Reaction score
2,993
Amani iwe nanyi

Hali ya ukame na ukosefu wa mvua inayoendelea katika sehemu kubwa ya ardhi ya nchi ya TANZANIA sio ngeni hapa duniani. Ukiperuzi historia utaona kuwa dola nyingi huko nyuma zilikuwa zikipata vipindi ya ukame na uhaba wa chakula unaosababishwa na ukosefu wa mvua.

Kwa ambao tunaamini uwepo wa Mungu tunajua kuwa mvua ni neema na baraka kwa viumbe kutoka juu kwa MOLA aliyeumba ulimwengu na kila kitu ndani yake. Mungu anaposhusha mvua yenye manufaa kwa watu basi hakika watu huneemeka maana chakula huzalishwa kwa wingi na ustawi wa maisha ya wanaadamu huwa mzuri na kinyume chake ni kuwa kunakuwa na majanga ya njaa,ukosefu wa mvua na hali ya ustawi wa maisha ya wanaadamu huwa ni mbaya.

Ukosefu wa mvua,ukame na uhaba wa chakula hutasfiriwa kuwa ni adhabu kutoka kwa mola juu ya watu wa jamii fulani kutokana na maovu waliyoyachuma kwa mikono yao wenyewe. Hivyo basi ombi langu kwako Rais Mama Samia usuone haya kukimbilia kwa viongozi wako wa dini na kuwaomba kuwa wasimame KUHIMIZA WATU WAFANYE TOBA YA MADHAMBI YAO KISHA WAMUOMBE MUNGU AITEREMSHE MVUA.

Hali ni mbaya, Mito inakauka kila kukicha, mvua sasa hivi ni mwezi wa kumi la moja na hakuna Mvua za VULI .Umeme unaotokana na maji nao umekuwa wa shida, migao ya maji kila sehemu. Hali ni mbaya Mama.Wanaadamu hatuna ujanja hata wa kutengeneza mvua kutoka mawinguni. Tunahitaji rehema na huruma za Mungu. Bei za vyakula zimekuwa juu huku kipato cha raia wa kawaida kikiwa chini ya dola moja kwa siku.

Hata Firauni alipokuwa kipatwa na majanga ya ukame na njaa alikuwa akikimbilia kwa Mtume Musa kumuomba asimame kumuomba MOLA aiondoshe hali hiyo ya tabu. Mtangulizi wako Rais Magufuli licha ya kuwa na makandokando yake,kila alipoona hali ya taifa inakwenda ndivyo sivyo, haraka sana alikuwa akisimama na kuliomba Taifa lisimame kumuelekea Mungu atuondoshee mabalaa..!!

Huu ni ushauri wangu kwako kama kiongozi mkuu wa Taifa hili la Tanzania,naamini kuwa wasaidizi wako wanapita humu Jamii Forums hivyo watakufikishia ushauri huu.
 
Ao Viongozi waliopata Madaraka kwa wizi wa kura hawana nafasi ya kuomba Mvua labda watubu na kuungama dhambi zao
 
Sio lazima aombe yeye bali anaweza kuwafata waja wema waombe kwa niaba yake. Hata Firauni alimfuata Musa amuombe kwa Mungu ondoe mabalaa ya Njaa katika taifa la Misri.
 
Amani iwe nanyi

Hali ya ukame na ukosefu wa mvua inayoendelea katika sehemu kubwa ya ardhi ya nchi ya TANZANIA sio ngeni hapa duniani. Ukiperuzi historia utaona kuwa dola nyingi huko nyuma zilikuwa zikipata vipindi ya ukame na uhaba wa chakula unaosababishwa na ukosefu wa mvua.

Kwa ambao tunaamini uwepo wa Mungu tunajua kuwa mvua ni neema na baraka kwa viumbe kutoka juu kwa MOLA aliyeumba ulimwengu na kila kitu ndani yake. Mungu anaposhusha mvua yenye manufaa kwa watu basi hakika watu huneemeka maana chakula huzalishwa kwa wingi na ustawi wa maisha ya wanaadamu huwa mzuri na kinyume chake ni kuwa kunakuwa na majanga ya njaa,ukosefu wa mvua na hali ya ustawi wa maisha ya wanaadamu huwa ni mbaya.

Ukosefu wa mvua,ukame na uhaba wa chakula hutasfiriwa kuwa ni adhabu kutoka kwa mola juu ya watu wa jamii fulani kutokana na maovu waliyoyachuma kwa mikono yao wenyewe. Hivyo basi ombi langu kwako Rais Mama Samia usuone haya kukimbilia kwa viongozi wako wa dini na kuwaomba kuwa wasimame KUHIMIZA WATU WAFANYE TOBA YA MADHAMBI YAO KISHA WAMUOMBE MUNGU AITEREMSHE MVUA.

Hali ni mbaya, Mito inakauka kila kukicha, mvua sasa hivi ni mwezi wa kumi la moja na hakuna Mvua za VULI .Umeme unaotokana na maji nao umekuwa wa shida, migao ya maji kila sehemu. Hali ni mbaya Mama.Wanaadamu hatuna ujanja hata wa kutengeneza mvua kutoka mawinguni. Tunahitaji rehema na huruma za Mungu. Bei za vyakula zimekuwa juu huku kipato cha raia wa kawaida kikiwa chini ya dola moja kwa siku.

Hata Firauni alipokuwa kipatwa na majanga ya ukame na njaa alikuwa akikimbilia kwa Mtume Musa kumuomba asimame kumuomba MOLA aiondoshe hali hiyo ya tabu. Mtangulizi wako Rais Magufuli licha ya kuwa na makandokando yake,kila alipooja hali ya taifa ijakwenda ndivyo sivyo, haraka sana alikuwa akisimama na kuliomba Taifa lisimame kumuelekea Mungu atuondoshee mabalaa..!!

Huu ni ushauri wangu kwako kama kiongozi mkuu wa Taifa hili la Tanzani,naamini kuwa wasaidizi wako wanapita humu Jamii Forums hivyo watakufikishia ushauri huu.
Ushauri mzuri,ni matuamaini yangu taarifa hii itamfikia...
 
Dua ya mchamungu mmoja tu inatosha kuliokoa taifa zima
 
ukate miti 2m, then mvua ije kwa maombi kweli

mtakula jeuri yenu watu wa Daslam
 
Acha propaganda , msimu wa masika ndo umeanza, maeneo mengi kwa sasa mvua zimeanza kunyesha japo ni kwa uchache, kufikia desemba mvua zitaongezeka na kila mtu atakuwa amepanda mazao yake, Mungu hutoa baraka hata kwa wenye makosa.
 
Back
Top Bottom