Ushauri: Rais Samia tunaomba utamke kesho kuwarudishia misharaha watumishi walioshushwa mishahara yao

Ushauri: Rais Samia tunaomba utamke kesho kuwarudishia misharaha watumishi walioshushwa mishahara yao

BrownRange

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2020
Posts
927
Reaction score
1,191
Ni ushauri na ombi kwa Mh. Rais, ikimfaa awarudishie mishahara watumishi wote mishahara yao iliyoshushwa. Ni vyema ikimfaa alizungumze hili kesho siku ya mei mosi, ili kujenga umoja wa kitaifa na kujali watumishi,

Tunakupenda sana Rais wetu, jemedari Samia Suluhu Hassan.
 
Mimi naomba Mhe. Rais apunguze mishahara ya makundi yafuatayo;

1. Wabunge
2. Mawaziri
3. Majaji
4. Wakurugenzi
5. Wakuu wa mikoa.

Makundi hayo ndio yanayo lipwa fedha nyingi sana na hivyo kupelekea walio chini kubaki chini.

Makundi hayo pamoja na kulipwa mishahara mikubwa lakini pia wanapewa nyumba, gari, ulinzi na posho kedekede, walio chini wanaendelea kubaki taabani.
 
Kesho ni siku ya kuiimbia serikali mapambio tu hakuna Cha ziada.
 
Mshahara uliopo katika ajira ni makubaliano ya kimkataba kati ya mwajiri na muajiriwa. Katika hali ya kawaida mshahara hauwezi kupunguzwa bila ya kuwepo makubaliano mengine ya kimkataba.

Mshahara ukikatwa bila ya kufuata taratibu za kiutumishi ama muajiriwa kuridhia, basi anapaswa ama kukataa rufaa kwa mamlaka zake za utawala, kuacha kazi mara moja, ama kulifikisha suala hili mahakamani ili lipate ufumbuzi wa kudumu. Hivi inakuaje mtumishi anakatwa mshahara wake pasipo kuchukua hatua stahiki!
Ni ushauri na ombi kwa Mh. Rais, ikimfaa awarudishie mishahara watumishi wote mishahara yao iliyoshushwa. Ni vyema ikimfaa alizungumze hili kesho siku ya mei mosi, ili kujenga umoja wa kitaifa na kujali watumishi,

Tunakupenda sana Rais wetu, jemedari Samia Suluhu Hassan.
Sababu zipi zilipelekea watumishi hao wapunguziwe mishahara yao? Je! Sababu hizo ni za kuridhisha na bado zipo?
Je! Watumishi hao walifungua shauri CMA ama "High Court - Labour Division" kwa ajili ya suala hilo?
 
Mshahara uliopo katika ajira ni makubaliano ya kimkataba kati ya mwajiri na muajiriwa. Katika hali ya kawaida mshahara hauwezi kupunguzwa bila ya kuwepo makubaliano mengine ya kimkataba.

Mshahara ukikatwa bila ya kufuata taratibu za kiutumishi ama muajiriwa kuridhia, basi anapaswa ama kukataa rufaa kwa mamlaka zake za utawala, kuacha kazi mara moja, ama kulifikisha suala hili mahakamani ili lipate ufumbuzi wa kudumu. Hivi inakuaje mtumishi anakatwa mshahara wake pasipo kuchukua hatua stahiki! Sababu zipi zilipelekea watumishi hao wapunguziwe mishahara yao? Je! Sababu hizo ni za kuridhisha na bado zipo?
Je! Watumishi hao walifungua shauri CMA ama "High Court - Labour Division" kwa ajili ya suala hilo?
We jamaa unamjua Magu katika ubora wake
 
Back
Top Bottom