Mshahara uliopo katika ajira ni makubaliano ya kimkataba kati ya mwajiri na muajiriwa. Katika hali ya kawaida mshahara hauwezi kupunguzwa bila ya kuwepo makubaliano mengine ya kimkataba.
Mshahara ukikatwa bila ya kufuata taratibu za kiutumishi ama muajiriwa kuridhia, basi anapaswa ama kukataa rufaa kwa mamlaka zake za utawala, kuacha kazi mara moja, ama kulifikisha suala hili mahakamani ili lipate ufumbuzi wa kudumu. Hivi inakuaje mtumishi anakatwa mshahara wake pasipo kuchukua hatua stahiki! Sababu zipi zilipelekea watumishi hao wapunguziwe mishahara yao? Je! Sababu hizo ni za kuridhisha na bado zipo?
Je! Watumishi hao walifungua shauri CMA ama "High Court - Labour Division" kwa ajili ya suala hilo?