Ushauri: Rangi za Bendera ya Taifa zifutwe katika sakafu za ndani ya Bunge

Ushauri: Rangi za Bendera ya Taifa zifutwe katika sakafu za ndani ya Bunge

Au waweke kijanitu bunge zima ndani mpaka nje.
Kwa wanayofanya sasa,

KIJANI ilifaa sana,

Lakini Kwa kuwa pale ni Kwa wawakilishi wa wananchi wote bila kujali vyama, wafuate rangi za Bendera, waweke red carpet.
 
Salaam,Shalom.

Mimi ni Mtanzania mzalendo wa Nchi yangu nzuri Tanzania, naijua thamani ya Bendera ya Taifa LANGU.

Bendera yetu ya Taifa Ina RANGI kuu nne, Bluu, Njano, Kijani na Nyeusi. RANGI hizo za Bendera ya Taifa naziona katika sakafu za ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sitaki kuhoji Uzalendo wa mtoa wazo la kupaka RANGI za Bendera ya Taifa katika sakafu za ndani ya Bunge la JMT, inawezekana, mtoa wazo Hilo alisukumwa na Uzalendo uliopitiliza.

Kwa maoni yangu kama Mtanzania, bendera au RANGI Inatakiwa iwekwe juu, ukutani, au katika nguzo, Si katika sakafu.

Ninashauri yafanyike marekebisho, RANGI hizo ziondolewe chini, ikae red carpet pekee.

MUNGU ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni🙏
Usiwaze ndugu yangu wengi wa waliopo Serikalini/bungeni ni watoto/wajukuu/vinasaba vya walioipigania nchi,baadhi yao kwenye harakati za kudai uhuru na baadhi yao kwenye the kagera war au kwenye nyadhifa kadhaa.Wew na mimi nnan hata tuhoji uzalendo hali ya kuwa wenyew wenye nchi do not mind!Uzalendo upo kwenye kupandishiana posho na mishahara nk sio kwenye rangi za sakafuni ndugu yangu
 
Kama walikuwa wamepigwa upofu wasilione hili,

Mungu amempa Rabbon uwezo wa kuwaondolea wingu Hilo machoni!!
 
Ndio kutaka kusema wale mapopoma wa ccm kama kina msukuma wanazisigina rangi za taifa
 
Wabunge acheni kukanyagwa bendera ya nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
 
Na Leo mnapita juu ya Bendera yetu ya Taifa?
 
Back
Top Bottom