Ushauri: Ripoti ya CAG isirudiwe tena kusomwa hadharani, inatia hasira na kuleta manung'uniko, wanaotuhumiwa hawajawahi kukamatwa

Kusomwa itabidi isomwe tu maana ni takwa la katiba, ishu ifike mahali wachukue hatua na hatua zionekane kuchukuliwa.

Tatizo hata enzi za mwendazake hakuna aliyeshtakiwa
Kama awamu hiyo ndo ilikuwa hovyo kabisa.

Mwendazake hakutaka kabisa hasara zisomwe, alipenda kusikia faidaza uongo tu ili kuwa manipulate wananchi wengi ambao wana akili ndogondogo na za kinyumbu. Ndo sababu akatibuana na Prof. Assad na kumwondoa kwa kuilawiti katiba.

Charles Kichere alipoteuliwa akaona isiwe tabu, akatusomea faida hadi ATCL, plus magawio kibao kutoka mashirika mbalimbali ya umma! Lakini alipoingia mama tu Charles huyohuyo akatusomea hasara ya ATCL kuwa tangu ifufuliwe ni mwendo wa hasara tu. Na in fact ni not shirika la ndege kupata faida ndani ya muda mfupi tu baada ya kuanza kazi. Hata mashirika makubwa duniani yana struggle kwanza. Ila mwamba yeye kwa kujua aliongoza vilaza akawa anawashushia mifaida ya kwenye karatasi tu, na mdogo wake sasa naona anaadapt kwa bro mambo mengi tu.

Tutaendelea kuwa na mambo ya hovyo as long as tutaendelea kutawaliwa na green mamba.

Hizo report mimi nilishaacha kuzifuatilia.
 

Mkuu umezungumza kirahisi mno kama vile sisi hatuijui serikali yetu ambayo ina matatizo yaleyale (kama ufisadi na uzembe) miaka nenda rudi.

Kwa maelezo ya mtoa mada hajaelekeza malalamiko kwa CAG na zoezi lake la ukaguzi, bali kwa wale wanaowasilishiwa taarifa (ambao ndio wenye mamlaka ya kuchukua hatua) hadharani, kwa mbwembwe ambazo mtu akiwa mgeni Tanzania/Africa atadhani kuna mijitu inaenda kunyongwa hadharani, kumbe show imeishia pale.

Na hizo hasara zinazojirudia kila mwaka, sijui ni lini huo ukosoaji, urekebishaji na usahihishaji hufanyika! Au nao ndo tuendelee kusubiri wakati wake haujafika?
 
Umeandika ukweli mtupu !
 
hivi huwa husikii,wapo waliokamatwa na kufikishwa mahakamani,pia ufahamu nchi inaendeshwa kwa kuzingatia sheria,hizo ni audit queries zinatakiwa majibu na serikali huzijibu,na ndipo tunapata zipi ni jinai,zipi ni uzembe na zipi ninafutwa
Wamekamatwa akina nani na wako gereza gani ?
 
Hapana. Endelea kusomwa kwa ajili ya kumbukumbu.
 
Ndugu kaz inafanywa sana si lazima itangazwe.ila kwemye mafail huko kunawaka moto. Unajibu hoja mpaka tumbo linauma na saa nyingine unahamishwa vijijin huko
 
Tuendelee na Mjadala , Teuzi za Hangaya zisitupoteze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…