Jick
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 1,327
- 2,041
Nakubaliana na wewe asilimia 100. Tena kuna wakati unaamka asubuhi unakuta uchafu kwenye compound yako.Uchafuzi wa mazingira unaangukia kwenye uhalifu, kuna watu hukusanya taka kisha usiku wanazitupa kwenye sehemu isiyostahili, kuna watu wanapiga muziki kwa sauti kubwa kwenye makazi ya watu nyakati za usiku huku wanaopigiwa kelele hawana pa kushitaki muda huo.
Ila hatuwezi kutatua changamoto hiyo kuanzisha jeshi la mazingira kwa sababu wanaofeli sasa hivi ndio hao hao watakuwa na sifa za kuwa askari wa hilo jeshi.