TheDreamer Thebeliever
JF-Expert Member
- Feb 26, 2018
- 2,490
- 3,593
Habari wadau..!
Leo nilikuwa na ushauri kwa serikali yetu na jeshi letu maana naona wanajipendelea sana,yani jeshi ndio linajipa peke yake jukumu la kulinda nchi wakati jukumu hilo ni la kila raia ,lakini raia tutawezaji kujilinda na kulinda Taifa siku za usoni wakati hatuna mbinu za kijeshi??
Je katiba inasemaje kuhusu ulinzi wa nchi??au kama haisemi kwaba ni jukumu la kila raia basi kuna aja ya kubadili katiba kuhusu ulinzi wa nchi yetu.
Kama jukumu la kulinda nchi ni la kila raia,ss inakuwaje jeshi wao ndio wachukue jukumu hilo peke yao??Binafsi naona hii zana ilikuwa nzuri kwa kipindi hicho lakini kwa ss kunabidi kuwe na mabadiliko ya kifikra na mitazamo ukizingatia hali ya usalama wa dunia yetu tunayoishi imekuwa mbaya sana kuliko hata zamani wakati jeshi linaanzishwa .Sasa hivi ishu kubwa inayosumbua dunia ni ugaidi na tumeshuudia ndugu zetu Kenya,Mozambique na wengine ambao hawakuwa na historia za machafuko sasa wanahaha ,je sisi tunajiandaaje kwa siku za usoni kama mambo kama haya yatatokea?
Wizara yetu ya ulinzi ipo makini sana,nipongeze sana kitendo cha kugoma kupokea wakimbizi wa MZ kwa sababu za kiusalama.Lakini bado siku za usoni tunaweza kuingia kwenye mitego ya watu wabaya.
Swali ,je kwa nini jeshi lisitengeneze utaratibu wa kuandaa wanajeshi wa akiba ambao ni raia yeyote kijana kama wanavyofanya Korea ya Kusini .
Hii itatusaidia sana hata sisi raia ,endapo siku moja yatatokea matukio kama ya ugaidi japo sio swala la kuombea lakini lazima tukubali ukweli sote tunaishi kwenye dunia moja tena dunia ambayo kwa sasa inakumbwa na uharibifu mkubwa na uvunjifu wa amani.
Inaweza ikawa tatizo ni bajeti lakini wanaweza kufupisha mda wa mafunzo hata mwezi mmoja unatosha.
=============================
Usajili nchini Korea Kusini umekuwepo tangu 1957 na inahitaji raia wa kiume wenye umri kati ya miaka 18 na 28 kufanya huduma ya lazima ya kijeshi. [1] [2] Wanawake hawatakiwi kufanya huduma ya kijeshi, lakini wanaweza kujiunga na jeshi. [3]
Uhariri wa Uanzishaji
Msingi wa usajili wa jeshi nchini Korea Kusini ni Katiba ya Jamhuri ya Korea, ambayo ilitangazwa tarehe 17 Julai 1948. Katiba inasema katika Kifungu cha 39, "Raia wote watakuwa na jukumu la ulinzi wa kitaifa chini ya masharti kama ilivyoainishwa na Sheria. "[4] [5] Sheria ya Utumishi wa Kijeshi ya 1949, ambayo ilitekelezwa mnamo 1957, ilibainisha kuwa utumishi wa kijeshi wa lazima unahitajika kwa wanaume wa miaka 19 au zaidi. [6] [2] Usajili unasimamiwa na Utawala wa Nguvu za Jeshi, ambao uliundwa mnamo 1948.