Ushauri: Serikali itoe fursa ya watumishi waliotumikia kwa zaidi ya miaka 15 kustaafu kwa hiyari

Ushauri: Serikali itoe fursa ya watumishi waliotumikia kwa zaidi ya miaka 15 kustaafu kwa hiyari

Chendembe

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
444
Reaction score
488
Sijuwi leo nililalia ubavu gani! Nimeamka na wazo hilo hapo juu. Ni baada ya wiki iliyoishia jana kupokea simu nyingi mno za ndugu na rafiki zangu kuomba ushauri na misaada mbalimbali.

Elimu yetu Bado haijabadili mitizamo yetu kuwa kusoma ni kuajiliwa haswa Serikalini na si vinginevyo.

Ufike wakati Sasa Serikali Ione znamna ya kuokoa vijana wetu, wamevurugwa.

Serikali ikioendezwa, itoe nafasi kwa watumishi wake kustaafu Kama wanaona wamechoka kwa sababu yoyote ilee.

Nawasilisha
 
Kikubwa fao la kujitoa liwepo tayari muda wowote.

#MaendeleoHayanaChama
 
Yaan hiki kitu kingetokea hata kwa masaa tu wengi wangetoka

Pia ingetengeneza fursa ya ajira kwa damu changa na mawazo mapya
 
Vizuri.
Pia kuajiriwa kungeanzia miaka 18 mwisho iwe 35 baada ya hapo kustaafu iwe miaka 50, iwe kwa hiari au lazima ikifika 50 lazima upishe wengine.
 
Embu We Fikiria ...Zenji Wese halijapanda bei Hapo hapo Wamekula 15% nyongeza ya Mshahara... Huku bara Hisabati bado Kukamilika kweli.?
 
Hii ingekuwa vzr saana,
Lingeundwa dirisha maalumu la aina hii ya wastaafu, wanaotaka kuwekeza kwenye kilimo, ufugaji au viwanda vya kuprocess mifugo na kilimo,
Wastaafu hao maalumu wapewe maeneo ya uwekezaji (tena buree), halmashauri husika itengeneze miundo mbinu ya kutosha (maji, umeme, barabara, mahospitali, shule) ku accomodate biashara zao. halafu kama uwekezaji wao haujafanya biashara isimame vzr, then mabenk yawape mikopo nafuu (with less than 10% interest) ili wafanye biashara zao zikomae.
Nina uhakika kila halmashauri ikipata wawezekezaji wa aina hii 100, basi inaweza zalisha ajira rasmi zaidi ya 2000, na ajira zisizo rasmi zaidi ya 100,000.
Kama kila muwekezaji akiwa na mtaji wa 120,000,000. then akapata mkopo wa atleast 80,000,000. Hii inamaanisha halmashauri husika zitapata uwekezaji wa angalau 20,000,000,000 (bilioni 20). Mzunguko huu kwenye halmashauri zetu utasababisha maendeleo ya haraka sana kwenye mashule, viwanda, biashara za kwaida n.k

Zikiptakna halmashauri 20, za aina hii kila mwaka. Basi In 5 tatizo la ajira likauwa limeisha, shule za sekondari, vyuo vya vyeta na vyuo vikuu, vinakuwa havilii tena wanafunzi kukosa ajira au sehem ya kupractise elimu yao.

Kupanga ni kuchagua, na inawezekana tukachagua this type of investment na serikali na mabenk yakasupport haya mambo.
 
Kustaafu lazima uzeeke, ukiondoka kazini kabla ya miaka 55 hadi 60 hawakulipi mafao........hiki ndo kinakwamisha watu kuacha kazi hata kama wamechoka, vinginevyo baada ya hiyo miaka 15 watoe kiinua mgongo ila pensheni za kila mwezi watoe baada ya kufika miaka 55...
 
Back
Top Bottom