Hii ingekuwa vzr saana,
Lingeundwa dirisha maalumu la aina hii ya wastaafu, wanaotaka kuwekeza kwenye kilimo, ufugaji au viwanda vya kuprocess mifugo na kilimo,
Wastaafu hao maalumu wapewe maeneo ya uwekezaji (tena buree), halmashauri husika itengeneze miundo mbinu ya kutosha (maji, umeme, barabara, mahospitali, shule) ku accomodate biashara zao. halafu kama uwekezaji wao haujafanya biashara isimame vzr, then mabenk yawape mikopo nafuu (with less than 10% interest) ili wafanye biashara zao zikomae.
Nina uhakika kila halmashauri ikipata wawezekezaji wa aina hii 100, basi inaweza zalisha ajira rasmi zaidi ya 2000, na ajira zisizo rasmi zaidi ya 100,000.
Kama kila muwekezaji akiwa na mtaji wa 120,000,000. then akapata mkopo wa atleast 80,000,000. Hii inamaanisha halmashauri husika zitapata uwekezaji wa angalau 20,000,000,000 (bilioni 20). Mzunguko huu kwenye halmashauri zetu utasababisha maendeleo ya haraka sana kwenye mashule, viwanda, biashara za kwaida n.k
Zikiptakna halmashauri 20, za aina hii kila mwaka. Basi In 5 tatizo la ajira likauwa limeisha, shule za sekondari, vyuo vya vyeta na vyuo vikuu, vinakuwa havilii tena wanafunzi kukosa ajira au sehem ya kupractise elimu yao.
Kupanga ni kuchagua, na inawezekana tukachagua this type of investment na serikali na mabenk yakasupport haya mambo.