Artificial intelligence
JF-Expert Member
- Jan 28, 2021
- 1,265
- 2,252
Tanzania ni nchi iliyozungukwa na maziwa na bahari, huku ikiwa na mito mbali mbali yenye kutiririsha maji nchini.
Tanzania kwa kiasi kikubwa kuanzia mijini hadi vijijini utegemea sana maji ya mito na mabwawa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na viwandani.
Kutokana na shughuli za binadamu, mabadiliko ya tabia ya nchi, maji upungua kwa misimu kadhaa kwenye mito hiyo na mabwawa, hivyo kuleta athari na kero kwa wananchi hususani maeneo ya mijini, hivyo kuendelea kuitegemea mito tu ni ukosefu wa fikra na kuwa nyuma kimaendeleo na kiteknolojia katika dunia ya sasa.
Serikali ni lazima ije na mpango (au iboreshe kama upo) wa "Desalination plants" kutoka kwenye maji ya bahari ya hindi, hii itasaidia sana pale maji yanapopungua kwenye mito , serikali kuzitumia kama "water reserves" ili kupambana na tatizo la uhaba wa maji hasa kwa jiji kama Dar es salaam lenye shughuli nyingi na viwanda linalozungukwa na bahari. Kukata maji siku moja tu upelekea athari nyingi sana hasa kwenye shughuli za uzalishaji kama viwandani, hali hiyo upelekea viwanda vingi kupata hasara.
Nchi kama Qatar, Kuwait, Bahrain, Saudi Arabia akiwa na desalination plant kama vile Ras Al Khair plant ambayo uzalisha 1,036,000m3/day, UAE yenye Taweelah plant inayozalisha 909,200m3/day, ni mifano ya nchi chache duniani zinazotumia hiyo teknolojia.
Tanzania inasubiri nini na wakati imepakana na bahari yenye maji mengi ya kutosha. Ni muda muafaka sasa wa serikali kuja na "project" kama hii, hili tuwe na "reserves" za maji ya kutumia pale nchi inapokabiliwa na uhaba wa maji. Kuendelea kutegemea mito tu kama vile rufiji, wami n.k ni kuwa nyuma kifikra na kukosa mipango madhubuti.
Hivyo bhasi serikali lazima iendane na wakati na mabadiliko ya tabia ya nchi, iache "normalcy bias" lazima iwe na teknolojia na mbinu mbadala za kukabiliana na changamoto kama hizo.
Kumbukeni maji ni uhai na maji hayana mbadala kusema yakikosekana utatafuta kitu kingine kama maji utumie.