Ushauri: Serikali ni wakati muafaka wa kuwa na "Desalination plants" kutoka baharini

Kwa sasa inaweza kuonekana ni ngumu sana au haiwezekani, Ila tunakoelekea kutokana na mabadiliko ya tabia ya chi ya kila saa, kuna wakati utafika haitakuwepo namna.
Maji ya bahari....inatakiwa kuwa last option kabisa kwa wewe kufikiria.
Kuna Njia nyingi za gharama nafuuu......
Hatujafika huko bado kuwazia kuhusu sea water.
Management tu ya vyanzo vilivyopo tu ni mbovu.
Mfano DAWASA mwaka 2020 alikuwa anazalisha 400k Metre cubic kwa siku....lakini katika hizo non revenue water ilikuwa ni 40% ( kama sijakosea), hapa kuna leakages na Losses zingine ukiwemo wizi.
Kama wangeweza kuzuia hizi, shortage ya water ingepungua.
 
Ni ushauri mzuri sana ila nadhani na naamini ni mradi unaohitaji mapesa mengi sana, vinginevyo it is a good idea na itatuondoa kwenye majanga kama haya ya sasa ya migao migao ya maji na umeme.
 
Kaka kama kuchimba visima tu hapa dar vimetushinda tunategemea chanzo kimoja tu cha Mto Ruvu, hiyo technologia ya ku-treat maji ya bahari (Desalination ) kwa matumizi ya binadamu tutaweza?

Gharama ya kutengeneza plant kubwa ni $250 millioni sawa na Tshs. Billion 575 na ule mdogo ni $80m ni sawa na Billion 184; Weka gharama hizi vs kuchimba visima vikubwa.

 
Desalination plants zitaendeshwa kwa umeme upi?
 
Ni kweli changamoto kubwa inaweza kuwa pesa kwa sababu mradi kama huu unaitaji pesa, kama ulivyosema njia nafuu zipo kama hizo za kukusanya maji kwenye mabwawa, kuvuna maji ya mvua, kuzuia hizo leakeges n.k, hizi njia haziwezi kutufanya tuwe na reserves za maji ya uhakika kwahiyo mgao utabaki pale pale. Baada ya kufanya uchanganuzi wa hizo njia ambazo ni nafuu, kwangu mimi hiyo ndiyo nimeona kama last option ya kumaliza tatizo.
 
Ni mtazamo mkuu, lakini Option bora kwangu ni
Maji ya mvua.
Ground water.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Hilo ni tatizo la serikali. Hivi kweli Tanzania haina uwezo wa kuinvest $250 kwenye mradi?
 
Umenisaidia sana hasa kufahamu gharama za hiyo mitambo kwani kwenye kuchangia nilisema kuhusu gharama na kwa ufahamu wangu mdogo nilijua hiyo mitambo itakuwa ghali sana! Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana wanao imudu ni wale wenye mahela ya mafuta 9wenye petrodollar!), vinginevyo sisi ni shida tu!
 
Mabadiliko ya TabiaNchi yanalikumba karibia Bara zima la Afrika,lakini mbona hapa kwetu ndio mito yote imekauka, mara Wasukuma na mamilioni ya Ng'ombe zao wameanza kulalamikiwa.[emoji848]
Kiukweli mwaka huu hali ni mbaya sana kuhusu suala la maji. Lazima tuwe na mbinu mbadala za kupata reserves za maji ya kutosha kukabiliana na nyakati kama hizi.
 
Pamoja na gharama za hiyo mitambo, hivi kweli kama taifa kwamba tutashindwa mradi wa billion 575.
 
Pamoja na gharama za hiyo mitambo, hivi kweli kama taifa kwamba tutashindwa mradi wa billion 575.
Na nadhani siyo suala la kushindwa, ni suala la wapanga sera kuamua tufanye nini na tuache nini! Na zaidi hapa kwenye kufanya maamuzi na kuamua, wataongozwa na MATUMBO yao siyo matakwa, mahitaji na shida za wananchi, sisi Watanzania, walipa kodi. Hapa ni suala la uroho na ubinafsi ndiyo tatizo la kufikia maamuzi muhimu kama haya. Bilioni 575/= si pesa nyingi!
 
Hapa umeongea ukweli, ndiyo maana nimeshauri tuachane na normalcy bias,lazima tujifunze kukaa tayari muda wote.
Ni kweli UTAYARI ni mbinu muhimu sana kwenye uongozi lakini siyo kwa viongozi wetu ambao hufanya maamuzi mengi kwa jazba na mihemuko na zaidi zaidi huwa wanangalia maslahi yao binafsi. Hili linatugharimu sana as a country!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…