Ushauri: Serikali ni wakati muafaka wa kuwa na "Desalination plants" kutoka baharini

Tunaamini awamu hii watazingatia sio kama wale waliopita,wameleta shida ambayo tungeweza kuiepuka.
 
Ni kweli unahitaji pesa nyingi, Ila hili ndilo litakuwa suluhisho la uhakika na kweli.
Lakini kumbuka gharama za uzalishaji wa mita moja ya ujazo kwa sasa ni karibu TShs. 2000. Ukiongeza na gharama zetu za uendeshaji itafika TShs. 3000, hiyo ni gharama kubwa sana kwa wananchi wa kawaida. Labda mitambo hii ihudumie maeneo wa watu wanaojiweza kiuchumi!
 
israel wana mitambo inadaka hewa na kuzalisha maji safi ya kunywa! na Tanzania kwa kuwa tuna jua karibia mwaka mzima desalination plant inawezekana tena sana!Miaka 4 iliyopita Waisrael walitaka funga plant ya Desalination maeneo ya Seaclif (Naisi DAWASA wana eneo pale la mradi kama huu) Hawa Waisrael Watergen awakupewa ushirikiano unaotakiwa tukaishia enda nao Zanzibar kula Pweza na Ngisi .Bei yao ipo chini kwa Gallon moja la maji kuliko garama za Dawasa za uzalishaji maji toka Ruvu....maana Dawasa wana bei elekezi ya kununua maji toka kwa private company kama ilivyo Umeme na Tanesco.
 
Tunaamini awamu hii watazingatia sio kama wale waliopita,wameleta shida ambayo tungeweza kuiepuka.
Sijui una umri gani na kama umeishi humu nchini na kuona AWAMU ZOTE, yaani ya kwanza hadi hii ya sita! Nasema hivyo kwani hali kama hii ilishawahi kututokea hapa nchini wakati wa awamu moja wapo! Hali kama hizi hutokea kutokana na tabia zetu binadamu na sababu nyinginezo.
 

Nadhani hili liko ndani ya uwezo wa nchi yetu tunashindwa kuwa na mipango dhabiti.
Hata mradi wa maji toka ziwa Victoria unaweza kuwa extended hadi kwenye jiji kubwa la Dar es Salaam.
 
Unajua Costs za kufanya Desalination ?; Hapo baadae technology inavyozidi kukua cost zitapungua....

Nchi za Kiarabu zina energy ya kutupa ndio maana kwao Desalination makes sense..., Kwa kuanzia kila mmoja awe na desturi ya kuvuna mvua kama anaweza
 
Kipindi cha Mwinyi ukame ulitokea,JK na Sasa kwa Samia,na bahati mbaya hizo awamu hawakuchukua hatua kwa ajili ya kesho ndio haya sasa ya jumba bovu kwa Samia.

Magu alidanganya watu eti gas ya mabeberu wakati ni uongo.
 
Tujiulize kwanza swali moja? Je, kuna maji kiasi gani kwasasa ya mito yanaishia baharini?

Yaani maji safi yanaenda baharini tunavyo ongea hivi halafu tuweka plant ya kusafisha maji ya chumvi?

Tatizo la Tanzania ni maji kupotea
Hivi maji yanayotoka ziwa Victoria tumefanikiwa kiasi gani
 
Je umefanya research ya gharama ya huo mradi wa desalination?
Hizo nchi ulizotaja zipo jangwani sisi Tz tumezungukwa na fresh water lakes, kaskazini lipo Victoria, magharibi lipo Tanganyika, kusini lipo Nyasa bado kuna moto kibao inatiririsha maji mwaka mzima...
 
Unajua Costs za kufanya Desalination ?; Hapo baadae technology inavyozidi kukua cost zitapungua....

Nchi za Kiarabu zina energy ya kutupa ndio maana kwao Desalination makes sense..., Kwa kuanzia kila mmoja awe na desturi ya kuvuna mvua kama anaweza
Niliwai fuatilia hili DAWASA .Technology ya Israel Gallon Moja la maji(5ltrs) ni garama ya chini kuliko Garama za kuzalisha 1 Gallon toka Ruvu hii ilikuwa 4 yrs back
 
Kwa Dar na Pwani na Tanga tungeweza tumia Desalination water.Tena private Investors wangewekeza
 
Niliwai fuatilia hili DAWASA .Technology ya Israel Gallon Moja la maji(5ltrs) ni garama ya chini kuliko Garama za kuzalisha 1 Gallon toka Ruvu hii ilikuwa 4 yrs back
Achana na gharama za mitambo kwanza...., Cost ya kutumia nishati tu ili kupata Lita Moja au Gallon Moja ya Desalinated Water ni kiasi gani ? Tupime kwa energy (KW) na sio Pesa sababu kuna sehemu nishati ni nafuu, mfano nchi za Kiarabu..., tupigie cost ya huu umeme wetu wa Tshs 300 kwa Unit na Umeme wa Mgao....,

Ingawa tukimaliza Bwawa la Nyerere huenda hio ikawa another story..., na hata hapo kwenye nchi yenye vyanzo lukuki na uwezo wa kuvuna mvua n.k. ni cheaper kulinda vyanzo vya maji kuliko kufanya desalination
 

Wewe una walakini. Mwenzio katoa njia mbadala na hata mifano. Na wewe umetoa njia mbalada lakini hukutoa hata mfano lakini unaponda hoja ya mwenzio!!

Kati ya uzi wako na wake, amekugonga konzi za utosi. Ni rahisi zaidi kuona hoja yako ni ya hovyo. Jifunze tu kutoa hoja - mifano na namba!!
 
Desalination system inatumia Umeme wakati unazalisha maji kwa kufanya process ya Reverse Osmosis.Badala ya kutumia Umeme wa Grid unaozalishwa na ges au maji wao wanatunia Solar Power so ROI inakuwa kubwa na bei ya galloni inakuwa Chini. Na OPEX sio kubwa pia kwani ni automatic system yenye hitaji wafanyakazi wachache















 
Na maji yote tuliyobarikiwa itakuwa ni kichekesho duniani tukiunda desalination plant.
 
Mkuu 'NewOrder', ninaweza kukueleza kwa uhakika kabisa kwamba yulipokuwa mwanafunzi, au kama bado wewe ni mwanafunzi ulikuwa na shida kubwa sana katika uelewa wako wa ulichokuwa ukikisoma.

Unasema "mwenzangu katoa njia mbadala na hata mifano." Je, uliposoma niliyoandika hukuona njia mbadala niliyopendekeza, au unataka mpaka nitaje "mabwawa ya kutunzia maji yasipotee bure kila mara mvua zinaponyesha"? Hiyo siyo njia mbadala wa hiyo 'desanization' anayopendekeza yeye, ambayo hata hakueleza gharama zake ziko vipi?

Unataka nitoe mifano ya mabwawa ya kutunzia maji, au nchi zinazotumia njia hizo?

Katika akili yako huwezi kujiongeza, ukaona kwamba mazingira ya Qatar, mfano alioutoa ni tofauti sana na haya ya kwetu? Qatar wanapata mvua kiasi gani kwa mwaka, au unataka kusema kesho na sisi tutakuwa jangwani kama wao?

Mwisho, kama wewe ni mwalimu, utakuwa mwalimu wa hovyop sana kwa wanafunzi wako.
 
Hakuna cha mazingira ndugu yangu, yaani kama taifa litashindwaje kuendesha mradi wa $575, mvua na mabwawa haviwezi kutufanya tuwe na reserves za maji ya kutosha kutumika katika nyakati kama hizi. Kwa sasa ujue kuna viwanda vimesitisha production kwa sababu ya uhaba wa maji. Maji hayajawahi kuwa na mbadala kama umeme kwamba unaweza tumia generator, kibatali, mshumaa, solar n.k
 
Tatizo letu tunaishi kwa fikra ya leo bila kufikiria future, haya mambo lazima yaanze sasa kama mkakati wa mbeleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…