Ushauri: Serikali ondoeni kituo cha daladala cha Ubungo River Side, kinasababisha foleni isiyo ya lazima

Ushauri: Serikali ondoeni kituo cha daladala cha Ubungo River Side, kinasababisha foleni isiyo ya lazima

Naomba kushauri serikali iondoe kituo cha daladala cha ubungo river side kwani kinasababisha foleni isiyo ya lazima.

Ubungo kuna flyover lakini foleni inayosababishwa na kituo cha riverside kama unatokea Buguruni inaondoa kabisa ladha ama raha ya uwepo wa ile flyover.

Kutokea Mwenge kwenda Ubungo hakuna kituo hivyo hakuna shida, shida iko Ubungo riverside ambako kuna vituo viko barabarani. Asubuhi ni shida na jioni ni shida.

Nashauri Serikali iondoe kile kituo ama ikiingize ndani ili kulazimisha daladala kuingia ndani badala ya kushushia watu barabarani.
Sasa ndugu kutoka mawasiliano hadi river hakuna kituo popote mpaka sasa abiria wanalazimika kuotea pale songas songas penyewe kumewekwa bango la katazo kuwa hakuna kituo sasa kituo cha river kikihamishwa abiria wataenda kupandia wapi?labda ungesema pale pale kisogezwe kwa ndani ( kule servise road) angalau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria za vituo vya njiani kama cha River side bus haitakiwi kusimama pale zaidi ya dk 3,sheria kama hizo zikifuatwa foleni itapungua pale
 
Sheria za vituo vya njiani kama cha river side bus haitakiwi kusimama pale zaidi ya dk 3,sheria kama hizo zikifuatwa foleni itapungua pale
Na zaidi haitakiwi kusimama barabarani bali anatakiwa kuingia katika ile nafasi waliyowekewa.
 
Kwahiyo unataka sisi tunaioshi Riverside tushukie buguruni tutembee kurudi Riverside? Mi nadhani kituo kiwepo ila barabara iwe expanded kiasi isiathiri movements
 
Unataka kusiwe na kituo kutoka mabibo hostel mpaka pale ofisi za tcra? Ungeshauri kiongezwe ukubwa ungeeleweka na usingeanzia Riverside, ungeanzia vituo vya Buguruni ukitoka tazara au kile cha pale Chama.........vituo vidogo....

NB:Eneo la Riverside haiwezekani ikakosa kituo.
 
Kuna baharia mmoja anavaaga kofia la pikipiki muda wote. Aisee. Na mwingine bonge black hivi.
Yule polis 👮 anapenda sana rushwa. Nilisha mpa makaratasi badala ya hela. Eti fire extinguisher haitoi povu
 
Dereva daladala ni mojawapo kati ya watu hovyo sana kujali matumizi sahihi ya barabara na vituo. Sehem zote penye vituo vikubwa ni hivyo hivyo, kufuta kituo sio haki utanyima huduma wakazi husika.

Vituo vingi ni vidogo vilitengwa kwa ajili ya kushusha kupakia na kuondoka sio kutega abiria. Miundombinu ipanuliwe vituoni lakini kikubwa sana ni ustaarabu wa madereva, la hasha ni kujenga usafiri wa kisasa kama BRT ili daladala zihamie nje ya mji.
 
Sema kituo kipanuliwe, machinga wasogezwe ili gari ziwe zinaingia ndani ya kituo. Mbona vituo vingi viko barabarani na haviathiri magari mengine.

Usishauri kitu kwa kujiangalia wewe tu, kile kituo kina abiria wengi sana wakashukie na kupandia wapi daladala??
Kituo kipanuliwe walau kiwe kama pale mnazi mmoja.
 
Mamaako atakuja na kauli "naomba tanroads na polisi muone cha kufanya pale riberside"
 
Na zaidi haitakiwi kusimama barabarani bali anatakiwa kuingia katika ile nafasi waliyowekewa.
Tumia akili

During rush hours unafika unakuta kituo chote kimejaa daladala, sasa utaingiaje. Inakulazimu ushushie/upakie abiria ukiwa main road.
 
Kinachofanga foleni pale ni ile zebra pale chini kabla haaujafikia petrol station na magari yanayogeuka kupakia abiria kituo cha upande wa pili

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uongo.

Haiwezekani magari kugeuka pale.

Gari ikitaka kugeuka (kukatisha route) lazima anyooke hadi Ubungo mataa, akate kona ndio arudi Riverside
 
Acha uongo.

Haiwezekani magari kugeuka pale.

Gari ikitaka kugeuka (kukatisha route) lazima anyooke hadi Ubungo mataa, akate kona ndio arudi Riverside
Unabisha nini mi namaanisha mtu akitoka ubungo kama anaingia njia panda ya mzee wa upako kuna wanaogukia pale pale mengine yanaingia sheli na ku geuka .
Mi ndio nasemea hayo pusi wewe[emoji1787][emoji1787]
 
Umevuta bangi?

Yaani mtu atoke Simu2000 na abiria wa Mnazi Mmoja, eti afike Riverside akatishe route!

Kwamba mtu atoke Makumbusho na abiria wa Kimanga, eti afike Riverside akatishe route!

Kwamba Eicher itoke Mbezi mwisho na abiria wa Mbagala ifike Riverside abiria wako nyomi ikatishe route!

Kwamba mtu atoke Kawe na abiria wa Segerea, afike Riverside akatishe route!

Kwamba mtu atoke Simu2000 na abiria wa G'mboto, gari imeshona nyomi, afike Riverside akatishe route!

Toa kituo river side bakisha hostel
 
Back
Top Bottom