Ushauri: Serikali yetu ibadili maisha ya wananchi wake

Ushauri: Serikali yetu ibadili maisha ya wananchi wake

chinatown

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
1,232
Reaction score
1,105
Nimebehatika kukaa kama sio kuishi sehemu tofauti tofauti duniani.nimeona na kujifunza kadhaa wa kadhaa jinsi serikali nyingine za ulaya ,marekani,na asia zinavyofanya kwa ajili ya wananchi wake.

Maisha yetu ni duni kwa sababu tu ya mipango yetu mibovu ambayo serikali yetu inafanya.Tasafu au aina hii ya mipango haiwezi kuinua maisha ya mtanzania, raia apewe nyavu na sio samaki

kipato cha mtanzania mmoja mmoja ni kidogo sana,kila mtu aliyeajiriwa anafikiria kuiba kuiba kuiba hii sio sawa hivi viongozi hamuoni namna nyingine ya kumuwezesha mwananchi akawa na kipato? kwa nini mpaka leo kima cha chini cha mtanzania ni tsh 350,000/hii pesa inatosha nini kwa mwananchi? Embu tuwe na hofu ya Mungu basi kama mna mawazo ya kufikiria wenza wa viongozi kulipwa kwa nini hamfikiri kuwaongezea wananchi vipato vyao?

Wabunge wanapata s/allowance zaidi ya tsh 300,000/ kwa kikao kimoja ambayo ni pesa ya mshahara wa mtu wa kima cha chini,

Viongozi embu badilikeni hivyo vitasafu vyenu haviwezi inua maisha ya Mtanzania na vilevile tafuteni njia itakayoondoa wizi makazini,watu wanaiba kukidhi mahitaji yao japo wanasiasa wanaiba kwa sababu ya tamaa ya kushindana
 
Yaani, utadhani Wabunge si binadamu wa kawaida; maana posho ya siku ni mshahara wa mtu!
Baada ya miaka 5 anapata 'kiinua miguu' takribani milioni 250; wakati huyu wa 'kikokotoo' anaambulia milioni 30.
Si udini, ukabila au vyama vya siasa; bali hili pengo kati ya walionacho na wasionacho, iko siku litavuruga amani ya nchi..!
 
Ukiondoa nchi za north afrika hakuna nchi chini ya jangwa la Sahara imefanikiwa kufanya hivyo na hili linafikirisha sana
 
wakikusikia niko pale
saa hizi wanafikiria mbinu za uchaguzi
Na hii ni kwa sababu siasa sasa imekuwa ni ajira rasmi,tena inayolipa kuliko other proffesions... udiwani,ubunge etc zilitakiwa kuwa ni shughuli za kujitolea na ingefaa kuwe na kanuni kwamba anayetaka nafasi hizo awe ana shughuli au kazi maalumu na asitegemee siasa. Pia kusingekuwa na mshahara kabisa,iwe tuu wakifika kwenye vikao vya Baraza la madiwani au bunge wawe wanalipwa nauli au mafuta na posho ya kujikimu. Hii ingefanya wale wanaotegemea siasa kama ajira wasingeikimbilia tena.
 
Back
Top Bottom