Brooklyn
JF-Expert Member
- Mar 17, 2009
- 1,459
- 286
Wadau mliobobea kwenye sheria za kimataifa na mambo ya bima naombeni msaada. Mimi ni mfanyabiashara wa magari, kwa bahati mbaya siku ya 11/3/11 ambapo tsunami iliyosababishwa na tetemeko la ardhi lilipoikumba Japani, meli niliyoambiwa itabeba mizigo yangu ilipangiwa kuondoka bandari ya Kobe. Nimejaribu kuwasiliana na exporter simpati wala email hajajibu bado. Bill of lading bado nilikuwa sijatumiwa ingawa tayari nilitumiwa shipping order kwa ajiri ya confirmation ya details zangu. Swali langu ni kwamba je iwapo kama meli imepotea ama mizigo kuharibika nitafidiwa mali yangu? Je kuna mwenye habari zozote juu ya kupotea kwa meli za mizigo? Je bandari ya Kobe nayo imekumbwa na tsunami? Note my incoterms is C&F.