Ushauri tafadhali kabla sijazirejesha hizi 10mil benki

kzba

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
1,355
Reaction score
789
Nilikopa 15mil katika taasisi moja ya kifedha kama miaka 3 iliopita nikaomba wanikate makato makubwa ili nilipe kwa muda mfupi it was like 493000 kwa mwezi.

Sasa haya makato ni makubwa mno nimefanya mishe nimepata kama 10mil hv lengo langu nikafute hilo deni coz naamin balance yangu huko bank haiwezi kuzidi hyo pesa kwa muda walionika hzo pesa.

Sasa naomba ushahuri wowote wa kujenga kabla sijarudisha huu mpunga
Hivi siwezi zungusha kwa namna yeyote huu mpunga ukazaa ili unipunguzie machungu kidogo wadau au nizidabo ili maisha yaendelee?

Note: Me sio mfanya biashara na sina uzoefu wowote wa jambo hilo
 
mkuu uko mkoa gani?
............
Tuanzie hapa kwanza,
.........
Ungekuwa unajua ununuzi wa hisa DSE, basi ungekuwa mbali kiaina.
 
Hizo mil 10 tafuta mradi uzifanyie unaweza ukawa unaingiza zaid ya hiyo hela unayokatwa benk kwa mwezi. . fungu mradi ufanye tu
 
Nishahuri mdau mambo ya kuanza kutofautisha wanaume wa dar na wa mikoani hayana tija mkuu
 
Nishahuri mdau mambo ya kuanza kutofautisha wanaume wa dar na wa mikoani hayana tija mkuu
mkuu mbona sijasema kama ulivyonifikiria?

mimi nimekuuliza tu kwa wema ili nikushauri kulingana na mazingira uliyopo!

haya bwana sawa...
 
kama wewe sio mfanyabiashara.. na hujawai kufanya biashara yeyote maishani mwako.

mimi nakushauri peleka hizo hela bank kafute deni lako lote kama ulivyowaza.

biashara ni risk na ili zifanikiwe zinahitaji experience. sasa wewe experience hauna na bado hutaki hasara hata iweje...

peleka bank tu mkuu nenda kafute deni..

watu watakushauri na pm nyingiii.. ili wafaidike tu wao... hakuna mfanyabiashara wa kumfaidisha mwenzake... kabla yeye hajafaidika
 
Hali ya uchumi haiko vizuri kwa mtu mmoja mmoja(uchumi wa taifa uko fresh) sasa upepo wa biashara umebadilika sana.naomba rudisha mkopo wa watu sababu wewe huna uzoefu wa biashara inaweza kukucost kwa kipindi hiki na baadae ukashindwa kurudisha mkopo. Vumilia hali ikae sawa baada ya miezi kadhaa hata ukienda kukopa tena utakopeshwa sababu wewe ni mteja mzuri na muaminifu kwa historia yako ya kurudisha mkopo kwa wakati.
 
Mradi gani sasa mdau isije pesa yangu ikapotelea serikalini na haya makodi aisee
Ni kweli mkuu. . biashara inahitaji experience lakini je ukikaa tu hiv jiv unahis experience utaitoa wapi? ?
Pia hela bila kuirisk huwez kupata nyingine kwa mfani mtu unanunua basi leo kesho linapata ajali, riski ni kawaida tu kwenye biashara
(Nimefanya biashara kidogo now ni muajiriwa)

Sasa mkuu lazima uangalia na mazingira uliyopo ni biashara ipi inatoka, pia lazima iwe biashara ambayo utaweza kuisimamia mwenyewe yaan isiwe na muingiliano na kazi zako. .
Kwa mfano hapo biashara ya mobile phone accesories inalipa sanaaaa. Na katika kuwekeza haizid 5 milion. Maana yangu ni kwamba unafungua duka la wastan la phone accesories then hiyo tano unaweka akiba au unafanyia kingine
Naongelea phone accesory ka kua ndio biashara niliowah kufanya na ninaifahamu vizuri na hata machimbo ya bidhaa zake nayajua, sjawai kufanya biashara tofaut na hiyo. .
Sasa hii biashara inategemea upo maeneo gan/mazingira gan mkuu.
 
Kwanza tuanzie kwenye hizo M15 ulizokopa ulizifanyia nini? Ulinunulia gari, ulijengea au ulizilia bata?
 
Kama huna uhakika wa nn cha kufanya nenda karudshe bank ili ubakie na kipato chako cha zaman uachane na makato ya benk kama una wazo tofaut unaweza rudsha hata 5m bank ukabak na hyo nyengne
 
Kama una mil 10 na mpaka sasa huna wazo lolote la nini cha kuzifanyia, na huna uzoefu na mambo ya biashara, kuliko kujiingiza katika hasara, ni bora ukalipa deni na hizo laki 4.9 kila mwezi ujiwekee na kuanza kufanya biashara ndogo, hata ikitokea bahati mbaya mambo yameenda vibaya, huna deni na mtu.
 
Well said mdau
 
Hiyo milioni kumi wape kina Pogba weekend wakicheza na Leicester udouble mzigo wako ila kama tu roho yako imekufa ganzi maana hawakawii kukuangusha kwa mara ya nne mfululizo.
 
Kama una moyo wa kiume basi weka mzigo kwa Kanjhi(betting) upate faida fasta ila usiweke yote weka kama ml mbili
 
Nishahuri mdau mambo ya kuanza kutofautisha wanaume wa dar na wa mikoani hayana tija mkuu
Ohooooo.......[emoji69] [emoji69] [emoji69]
Vijana wamesha kutupia kijembe comrade....[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hiyo milioni kumi wape kina Pogba weekend wakicheza na Leicester udouble mzigo wako ila kama tu roho yako imekufa ganzi maana hawakawii kukuangusha kwa mara ya nne mfululizo.
Afanyeje?.. Maana nimejaribu kusoma, hata kwa kugeuzageuza nimeshindwa kukuelewa ulichoshauri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…