Ushauri tafadhali - Toyota Vitz, Duet, Allex, RunX, Suzuki SWIFT,

nimependa michango yako, inaelekea ww ni mtaaalam wa magar
 
Kwa kiasi chake mkuu. Karibu sana

Mkuu nimepata bonge la shule nilikuwa na mpango wa kununua swift below 2005 itabidi nijipange vp kuhusu toyota alteza? Au toyota progress vipuli vinapatikana kwa bei nzuri?
 
I think Jamii forum is more than an ordinary University
I real Enjoy thread za namna hii kulikoni zile za "JAMANI NIMEAMKA WIFE KANUNA" Nifanyeje?
Big up all
 
off all the list, hakuna gari apo. chukua toyota corrola,sprinter au Corsa. (cc 1300)
Lazima ukue kimtazamo, we kama hujaona waache wenzio wanaojua wamshauri, this is uncivilized habits achana nayo, inawezekana aliyeomba ushauri huko ndo uwezo wake ulipo. Ebu kuwa kidogo.
 
Mkuu nimepata bonge la shule nilikuwa na mpango wa kununua swift below 2005 itabidi nijipange vp kuhusu toyota alteza? Au toyota progress vipuli vinapatikana kwa bei nzuri?

Mkuu, inategemea na mfuko wako.

Ila mara kumi Altezza, hiyo Progress ni moto wa kuotea mbali. Engine size ya Progress inaanzia 2,500 hadi 3,000cc. Ni six cylinder, halina mzaa kwenye foleni. Kama wewe ni mtu wa budget lazima litakushinda - litakua linapigwa vumbi tu nyumbani.

Altezza kuna zenye 2,000cc, 2,500cc hadi 3,000cc - so inategema umechagua lipi.

Body parts kwa zote mbili ni gharama. Ila kama ukichukua lenye engine ya 3S (Altezza) ulaji wa mafuta sio mbaya sana.

Altezza hata me mwenyewe naipenda. Ila ni gharama kidogo mkuu kulinunua na kulihudumia pia. Ila kama mfuko unaruhusu, we vuta kitu nyumbani.
 

Mkuu Ramthods nakupa big up sana maana hapo penye red umegusa wengi mno. Hebu tupe (twaomba mkuu) shule zaidi hususani inayowalenga watu ambao wanaangukia kwenye red; unawashauri waanze na gari gani?
Asante
 
Jf ni zaidi ya univasty. While ninayoipata hapa sijawahi pata kabisa!
 

i do second.... Toyota starlet ni ngumu... Its a car for economy... Hata ubora wake ni mathubuti... Si gari nyingine zapasuka kama mabox... Yenyewe huwa inabonyea na hivyo waweza kunyoosha...,
nawasilisha hoja... Ni pm nikupe namna ya kugo abt one..
 

kwa nini reflect sio nzuri ndugu yangu??
 
Bajaji is the best aisee, kama ni ishu ya mafuta I suggest u go to this stuff
 
kukwepa haya yote we nunua gari mpya kabisa, achana na mitumba ukinunua unapewa na 2yrs guarantee ama kilometa 160,000 ikileta shida u get a replacement
 
Wadau vipi ulaji mafuta wa Ipsum ya 1999 engine 3S-FE? kuna mtu anataka kuniuzia odormeter 90000km?
 
Wadau vipi ulaji mafuta wa Ipsum ya 1999 engine 3S-FE? kuna mtu anataka kuniuzia odormeter 90000km?

Usiangalie odometer angalia body coz injini ziko nyingi tu zinauzwa
 
Jamani hivi hizi Toyota PASSO zikoje? Zimenivutia bei nzuri na ni za miaka ya karibuni 2004-2006

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…